Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2006

Elimu sio cheti na cheti sio elimu

Hivi kwenda shule maana yake nini? Usomi ndio nini? Ni wingi wa "mawe" ya mhusika au ndio nini vile.Usomi ni mpaka uwe na makaratasi mengi au ni maarifa? Nadhani kuna hitilifu ya mtazamo kuhusu dhana ya usomi. Watu wanatambiana kwa wingi wa makaratasi yanayoitwa cheti, shahada...uzamifu sijui nini na nini. Wanaona raha kuitwa Dakta nanilii! Nina mashaka na aina ya usomi wa Watanzania tulio wengi. Tunasoma kwa sifa tu lakini hatusaidii chochote katika kuipeleka mbele jamii yetu. Watu wanasoma wapate makaratasi yatakayowapa utajiri. Makaratasi yakayowapa heshima. Saluti. Na mengine mengine. Huu ndio mtazamo wa waungwana tulio wengi. Mtizamo kinyume kabisa. Sioni maana ya tunuku za makaratasi haya manake yametuletea kero katika jamii. Mosi, watu wamekuwa hawana biashara nyingine "mashuleni" zaidi ya kusomea majalada hayo. Matokeo yake ni zao la wasomi vihiyo wasio na loloooote! Wasomi wanaomaliaza masomo na kusahau kama kuna kusoma. Wanaanza hata kusoma udaku. Vil