Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Waandishi

Vitabu Nilivyosoma kwa Mwaka 2017!

Picha

Kitabu Kipya cha Malezi na Makuzi

Picha
Malezi ya sasa yamekumbwa na changamoto nyingi na kusababisha watu kushindwa kuwasaidia watoto na vijana wao ili kufanikiwa. Mmomonyoko wa maadili umekuwa chanzo kikubwa cha matatizo yanayomkumba kijana na jamii kwa ujumla. Matatizo hayo ni kama vile ukosefu wa ajira, kushindwa kufikia ndoto za maisha, migogoro katika familia, pamoja na watu kushindwa kuwa na utulivu na amani.

Vitabu 49 Nilivyovisoma Mwaka 2016

Picha
Namshukuru Mungu nimeweza kusoma vitabu 49 kwa mwaka 2016. Nimejifunza mengi. Kusoma ni kama kupata nafasi ya kufanya mazungumzo na watu wa kila namna ya uelewa ambao kwa hali ya kawaida usingeweza kuwasikia vijiweni.  Msisitizo wangu umekuwa kwenye vitabu vinavyochambua tabia katika maeneo mbalimbali ya maisha. Hata hivyo, vipo vichache vya masuala ya imani, falsafa na dini. Sijawa msomaji wa riwaya/novel. Nikutie moyo wewe mwenye ratiba ngumu kwa siku. Unaweza kufanya maamuzi ya kusoma ikiwa utaamua kuweka ratiba yako vizuri. Nijitolee mfano mimi mwenyewe.

Miaka miwili ya Kuwa 'Mama' Ina Mafunzo Makubwa Kwangu...

Picha
Nilipoamua kuchukua uamuzi wa kubadilishana majukumu na mke wangu sikujua ni kwa jinsi gani uamuzi huo ungenibadilisha mimi na kunipa mtazamo mpya kabisa katika maisha. Baada ya kuzaliwa Baraka siku kama ya leo mwaka 2012 tuliamua kubadilishana majukumu ya familia; mimi nibaki na kuangalia watoto na kutunza nyumba na mahitaji yake yote na mke wangu aendelee kufanya kazi na kusaidia wakati wowote anaoweza.

Mwaka unakatika....Tumesonga mbele ama nyuma???

Picha
Nashukuru kwa blogs na tovuti mpya ambazo zinachipuka na kuendeleza nia njema ya kuigusa jamii. Ningependa tuanze kwa kujiuliza, 'Je! Tunasonga mbele ama nyuma katika harakati zetu?' ...kwa ujumla, haijalishi ni sababu gani ilikufanya u-blog, mwisho wa safari sote tunajikuta na zao moja ama "mlaji" mmoja ambaye ni JAMII.

[VIDEO]: Mazungumzo na Liberatus Mwang'ombe na Solomon Chris baada ya Uchaguzi DMV

Picha
Mubelwa Bandio kati akiwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi za Mwenyekiti wa Jumuiya DMV Liberatus Mwang'ombe (L) na mgombea nafasi ya Katibu Msaidizi Solomon Chris (R0 wakati wa mahojiano Agosti 9, 2014, Jumuiya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia nchini Marekani ilifanya uchaguzi wake mkuu. Matokeo yake yamekuwa yakipingwa na waliokuwa wagombea wa uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali. Wamaketi na Vijimambo Blog na Kwanza Production kueleza sababu hasa za kupinga matokeo hayo siku ya Jumatano ya Agosti 13, 2014. Karibu uungane nasi kusikia wanachopinga

Unauelezaje utamaduni wa kusainiwa kitabu na mwandishi?

Picha
Profesa Mbele anaeleza vizuri kuhusu utamaduni wa kusainiwa vitabu katika blogu yake:  "...Suala hili la kusaini au kusainiwa vitabu linastahili  kutafakariwa. Naamini lina vipengele kadhaa muhimu, kama vile kiutamaduni, kisoshiolojia, kisaikolojia, na kifalsafa. Hata katika maduka ya vitabu hapa Marekani, aghalabu utaona vimepangwa vitabu vya mwandishi vikiwa na ujumbe "Signed copy." Jambo hili linaisukuma akili yangu kutaka kulielewa zaidi. Ningependa kujifunza zaidi kuhusu suala hili, kwa kusoma maandishi mbali mbali na kufanya tafakari mwenyewe..."  Msomaji wa kitabu cha Profesa Mbele, akifurahia nakala ya kitabu. Picha: @hapakwetu Unaweza kusoma zaidi kwenye blogu yake hapa . Kama mmoja wa wasomaji waliowahi kupata bahati ya kusainiwa kitabu na mwandishi mwenyewe, mmoja wapo akiwa Profesa Mbele, mwandishi wa kitabu kizuri cha " Africans and Americans Embracing Cultural Differences ", nikiri kabisa kwamba suala hili lina muujiza wa aina...

Shukrani za pekee kwa Prof. Mbele kwa zawadi ya thamani!

Picha
'Africans and Americans Embracing Cultural Difference', ni kitabu kizuri nilichokisoma kwa mara ya kwanza Aprili, 2009 nilipokiona katika duka la vitabu KIMAHAMA, Arusha. Ilikuwa ni baada ya kukisikia kikisemwa na rafiki yangu mmoja. Ni miaka mitano imepita, lakini kitabu hiki hakikuwahi kuizoea maktaba yangu tangu wakati huo. Kusoma kitabu chenye saini ya mwandishi, si jambo linalowatokea wengi. Ni muujiza ulionitokea. Picha: Jielewe Kwanza, kwa rafiki zangu wasomaji waliofika kwangu kwa mazungumzo ya vitabu na waandishi, kitabu hiki hakikukosekana kwenye mazungumzo hayo. Na kila aliyesikia sifa zake, alipenda kuthibitisha ikiwa nilisema  kweli kwa kukiazima. Kiliazimwa na wasomi, wasafiri, waongozaji wa watalii (tour guide), wapenda maarifa, kutaja kwa uchache. Ni bahati mbaya sana kwamba hakikuwa kinapatikana katika baadhi ya maeneo. Hivyo, kiliazimwa, na kuazimwa, tena na tena kwa muda wa miaka miwili. Mwaka 2011, kiliondoka rasmi kwenye maktaba yangu. Nilikuja k...

Nilipozungumza na blogu ya Maneno Matamu: “Kiswahili ni alama ya Uafrika wangu.”

Picha
Yafuatayo ni mahojiano yangu na blogu ya Maneno Matamu kuhusu, pamoja na mambo mengine, suala la lugha za Kiafrika na nafasi ya blogu katika kukuza lugha hizo katika enzi hizi. Ulianza kuandika blogu mwaka 2005. Uliamuaje kushiriki katika mtandao wa Internet namna hii? Nakumbuka nikiwa mwanafunzi nilikuwa mfuatialiaji mzuri wa makala za mwandishi maarufu,   Ndesanjo Macha   (ambaye sasa ni Mhariri wa Global Voices eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara). Yeye ni mwanablogu wa kwanza wa Kiswahili. Na kwa kweli niilivutiwa sana na aina yake ya uandishi, mijadala aliyokuwa akiiendesha kwenye blogu yake pamoja na matumizi mazuri ya lugha. Kwa hiyo hamasa ya kublogu ilitokana na  blogu yake . Blogu kwangu niliiona kama fursa nzuri na rahisi ya kujadili masuala ninayoyaelewa vizuri ya kiutambuzi na sayansi. Mule niliona ingekuwa rahisi kupata jukwaa la kubadilishana mawazo na watu bila kikwazo chochote na pia p...

Nilipokutana na Mshairi Serina wa Upande Mwingine

Picha
Katika mkutano wa wanablogu na waandishi wa habari za kiraia uliofanyika Nairobi, Kenya, nimebahatika kukutana na mwanablogu niliyekuwa na hamu sana ya kuonana naye. Naye si mwingine bali, dada Serina Kalande, anayetuandikia kwenye blogu ya Upande mwingine . Na Serina Kalande, wa Upande mwingine. Picha: Deogratias simba Ni dada mkarimu, mpole, mwanana na mwema sana kuzungumza naye. Serina, asante kwa baraka ya kukuona.

Blogging Revolution: Shubiri kwa wajiitao serikali

Picha
Kitabu kizuri kinachoangazia mabadiliko ya kijamii na kisiasa yaliyoletwa na matumizi ya zana za uandishi wa kiraia hususani blogu.  Kinatazama namna blogu zilivyochangia Mapinduzi yanayoendelea katika nchi za kiarabu –maarufu kama Arab Spring – na jinsi ambavyo blogu hizi zinaanza kuwatia hofu watu wanaojiita serikali.

Umemsoma Dambisa Moyo?

Picha
Kama una mpango wa kusoma kitabu kimoja tu mwaka huu, napendekeza hiki cha Dambisa Moyo kiitwacho "How the West was Lost". Ukikisoma utaelewa zaidi kwa nini hawa watawala wanaoitwa "The darling of the west" wanaopigana vikumbo kuhudhuria mkutano wa G8, wamepotea njia. Anacho kingine alichokiandika kabla ya hiki, kiitwacho cha Dead End, bado nakitafuta. Naambiwa ni moto.

Take the Risk cha Ben Carson

Picha
Ndio kwanza nimeanza kukisoma. Take the Risk: learning to identify, Choose and Live with accepatable Risk. Kimeandikwa na Mganga Ben Carson kwa msaada wa Gregg Lewis na kuchapishwa na Zondervan Publishing House mwaka 2008. Kitabu kinaanza na masimulizi ya upasuaji mgumu uliofanyika Julai 2003 kuwatenganisha Ladan na Laleh, mapacha waliozaliwa wakiwa wameungana sehemu ya vichwa vyao. Mapacha hao hata hivyo walifariki dunia wakiwa na umri wa miaka 29 wakati upasuaji huo ukiendelea huko Singapore. Katika kitabu hiki, mwandishi anajaribu kutupatia somo lilitokana na Upasuaji huo. Ladan na Laleh raia wa Iran muda mfupi kabla ya upasuaji huo uliofanyika Julai 2003.

Uliwahi kukisoma hiki?

Picha

Padre karugendo na mijadala ya Imani

Picha
Kitabu hiki nilikisoma mara ya kwanza mwaka jana. Yeye mwenyewe alinielekeza mahali pa kukipata baada ya kuwa amesoma mjadala uliomhusu kwenye blogu hii baada ya kusemekana kuwa Padre Karugendo alikuwa "amevuliwa" upadre. Nilijifunza mengi kuhusu dini. Pengine unaweza kujiuliza; Kwa nini aliandika kitabu hiki? Pamoja na kukieleza kisa kizima kilichosababisha yeye "kufutwa" upadre kupitia tangazo la gazetini, Padre Karugendo anasema katika uk. 22: "...lengo zima la kutafakari kwangu na kukushirikisha wewe msomaji, ni kutaka kujenga utamaduni kama ule wa kule zilikotoka dini hizi za kigeni. Utamaduni wa kuamini kitu unachokifahamu vizuri, unachokitafakari, kinachogusa maisha yako ya jana, leo na kesho. Imani inayojenga historia yetu - historia ya Mungu na watu wake wa taifa la Tanzania!" Pamoja na hilo, Padre karugendo anasema kwa sauti kubwa kabisa kwamba, "Si haki Maaskofu kukemea ufisadi ndani ya serikali na kuacha ufisadi unaoendelea ndani y...

Ninachokisoma sasa...

Picha

Pesa bila kufisidi mali ya umma...

Picha
Pesa bila unyonyaji inawezekana? Ninakisoma hiki hivi sasa kwa mara ya pili, cha Napoleon Hill.

Pendekezo la kitabu

Picha
Kama unataka kujielewa, kitafute hiki.

Tunapenda ushirikina kuliko vitabu - Prof. Mbele

Picha
"...Umaafuru wa kitabu hiki (Rich Dad Poor Dad) nilianza kuusikia huku Marekani, miaka michache iliyopita. Ni kati ya vitabu vingi ambayo vinasomwa na hao wenzetu, wakati jamii yetu ya Tanzania inaendelea kuzama katika giza au tunangojea kiongozi wa nchi au serikali ituletee maendeleo, na tukijitahidi sana, tunatumia ushirikina. Tuko tayari kulipa laki nyingi kwenye mambo ya ushirikina, eti tupate mafanikio, badala ya kununua vitabu na kuvisoma. Sasa basi, pamoja na vibuyu vyetu, wenzetu wa-Kenya, ambao wamezingatia elimu tangu zamani, wanaingia nchini mwetu na kujichukulia ajira au kuanzisha miradi. Sisi bado tunahangaika na vibuyu badala ya vitabu. Tutakoma, maana wahenga walisema kuwa asiyefunzwa na mamake hufunzwa na ulimwengu. Na bora iwe hivyo, labda hatimaye tutapata akili. Uzembe ulivyokithiri miongoni mwa wa-Tanzania, utawasikia wakilalamika mbona kitabu hiki hakijaandikwa kwa ki-Swahili? Wakishauliza hivi, wanaamini wametoa hoja nzito, badala ya kutambua kuwa wana...

Pendekezo la kitabu: Rich Dad Poor Day

Picha
Kama hujawahi kukisoma hiki, kuna mengi unayakosa. Harakisha kukitafuta! Nakisoma kwa mara ya tatu sasa, sijakichoka!