Uislam: Ndoa na mali havihusiani?
Jana nilikuwa nikitazama kipindi cha kiislamu kwenye televisheni ya Chaneli 10. Suala la mali katika ndoa za dini hiyo lilikuwa likijadiliwa. Kwamba Kiislam, mali katika ndoa si suala la wanandoa kwa pamoja. Kwamba mali anazoingia nazo mwanandoa kwenye ndoa, zinabaki kuwa zake mwenyewe. Na wakiachana, kila mmoja anaondoka na alichokuja nacho. Hata ndani ya ndoa, mali zinapatikana 'separately' kwa maana ya kwamba kila anachopata mwanandoa hicho ni haki yake yeye mwenyewe. Wakitengana, kila mtu anaondoka na vyake. Katika kufakari hayo, nilijaribu kumfikiria mwanamke na nafasi yake katika ndoa. Nikamwona kama kiumbe anayenyanyaswa na dini. Kwa nini? Wanaume wengi hutafuta mali kwanza ndio waoe, na hata wanapooa, huwaoa wanawake watakaowategemea wao. Katika hali hii nini salama ya mwanamke katika dini inayoruhusu talaka? Hizi si dalili za wazi za ukandamizaji wa jinsia ya kike?

Ntakitafuta hicho Mkuu!
JibuFutaIla MKUU una ukimya fulani siku hizi MKUU!
Just sayin'.....!
Ni kweli mtakatifu Kitururu. Kuna mambo hayajakaa sawa bado.
JibuFutaElimu ya watanzania iliwafanya wananchi wachukie vitabu sababu toka shule za misingi hadi vyuo vikuu vitabu vinaelezea matukio ya ukoloni, historia zisizokuwa na mizizi ya mtu kuwa mbunifu na mfumo mbovu wa hatima ya elimu kuwa mwenye akili ni yule anayefaulu mtihani wa mwisho.
JibuFutaChachu ya kusoma vitabu ijengwe kutoka mashuleni, watu wanaona bora atembee mtaani kuuza mitumba ya CD/DVD apate riziki kuliko kusoma vitabu mwisho wa siku alale njaa.
NAKUKARIBISHA HUKU PIA, http://www.amosmsengi.blogspot.com/
Kaka habari za siku, naona hata namba zako za simu hasa TIGO haipatikani........
JibuFutaKuhusu kitabu, ni kweli kinaonekana ni kizuri, lakini naomba wakati mwingine uwe unatuelekeza vinapopatikana vitabu hivyo..... ni wazo tu mkuu
Pamoja daima
Amos asante sana kwa maoni yako murua. Karibu kwenye uwanja wa kublogu.
JibuFutaKoero, asante kwa wazo zuri.