Kikao cha tathmini na mipango ya familia


Wiki hii mimi na familia yangu tulikuwa na kikao cha ‘halmashauri kuu’ ya mwaka. Kikao chenyewe kililenga kujitathmini sisi kama familia na kujiwekea malengo ya pamoja kwa mwaka 2023. Kikao hiki kinatarajiwa kufuatiwa na kikao cha 'Kamati Kuu.'


Maandalizi ya kikao hiki cha 'banguabongo' yalifanyika kwa kupeana dondoo za kufanyia kazi agenda za kikao. Hatimaye siku ikawadia. Jioni ya Jumapili ya Desemba 25, 2022. Tukiwa eneo tulivu mbali nyumbani, baada ya mwenyekiti wa kikao kueleza kwa nini tumekutana, shughuli yenyewe ikaanza.


Agenda ya kwanza ilisomwa na mtoto wetu wa kwanza, “Kitu gani ulichofanya mwaka huu kinakufanya ujisikie fahari?” Tukatakiwa kuandika kwenye vikaratasi vidogo tulivyokuwa tumegawiwa tayari. “Tumieni vikaratasi vya kijani. Mambo matano makubwa yaliyokufanya ukajisikia fahari kwa mwaka huu.” Baada ya kila mmoja kuorodhesha mambo yake matano yaliyomwendea vyema mwaka huu, mtoto wa pili akakusanya vikaratasi vyenye majibu na kuvibandika kwenye ubao tuliokuwa nao kikaoni. 


Uzuri wa zoezi hili ni kuwasaidia wajumbe wa 'Kamati Kuu' kuelewa ilipo fahari ya kila mwanafamilia. Kinachomfanya mtu ajisikie farahi kina maana kubwa kwake. Familia ni kituo cha kwanza kulea hali ya mtu kujisikia fahari.


Kadhalika, ipo haja ya kuwepo mazingira ya uhuru wa mtu kusema anachofikiri. Demokrasia inaanzia nyumbani. Hata hivyo, mazingira haya ya uhuru wa mawazo hayaanzii siku ya kikao. Kazi ya 'Kamati Kuu' ni kuyajenga mazingira hayo mapema kabla ya kikao. 


Katarasi za kijani zilionesha kila mmoja wetu, kwa sehemu yake, alikuwa na vitu vya maana vya kumshukuru Mungu kwavyo. Basi. Tukamshukuru Mungu kwa matendo makuu aliyoyafanya kwa kila mjumbe iwe kwa kumtimizia mipango yake au basi tu kwa mema yaliyomtokea.


Kisha mtoto wetu wa pili alisoma agenda ya pili, “Mipango gani haijaenda sawa mwaka huu? Kitu gani ulichofanya (ulichoshindwa kufanya) mwaka huu na kinakufanya ujisikie aibu kwa namna fulani?” Shughuli nzito kidogo lakini tunaifanya kwa mizaha ya hapa na pale. Saa nyingine mambo mazito hayajadiliwi kwa sura zisizoruhusu vicheko.


“Inaweza kuwa ni tabia fulani iliyokufanya ujisikie kufedheheka. Tumieni vikatarasi vyekundu,” anatukumbusha. Huwezi kusimamia mipango ikiwa huogopi fedheha. Unapojiwekea mipango yako lazima kujiwekea pia mazingira ya kuepuka fedheha. Kwa ngazi ya familia, saa nyingine, unapowaambia wenzio mipango yako unajiwekea mazingira ya kupambana usijekufedheheka wakati wa kutoa ripoti ya mwaka.


Baada ya kila mmoja kuorodhesha, mtoto wa kwanza alivikusanya vikaratasi vyote na kuvibandika kwenye ubao kama ilivyokuwa kwenye agenda ya kwanza. Tukasoma kikaratasi kimoja baada ya kingine. Tulipeana tahadharani. Ikiwa kuna yale ambayo mtu anafikiri ni ya binafsi sana halazimiki kuyasema.


Kuzungumzia aibu zetu halijawahi kuwa jambo jepesi. Kuna majibu hayakuwa ya moja kwa moja, au yaliandikwa kwa lugha ya kuelekeza lawama kwa wengine. Hivyo ilibidi kueleweshana ili kila mmoja ajielekeze kwenye mapungufu yake mwenyewe. Hapa tulikuwa tunajiwekea mazingira ya kujiwekea mipango kwa mwaka unaoanza. Ukifahamu kitu usichopenda kitokee, kitu kitakachokufanya ufedheheke, utakuwa makini zaidi katika kusimamia unachotaka kitokee.  



PICHA: Msoma agenda akiwa kazini 


Baada ya kujadili vitu vilivyotufanya tusijisikie ‘fahari’ tukahamia kwenye agenda ya tatu.  Ilikuwa zamu ya mke wangu ambaye ni 'Mjumbe wa Kamati Kuu.' Agenda ikasomwa kwa sauti, “Vitu gani ungetamani kuvifanya kuanzia sasa? Unatamani nini kizuri kitokee mwaka huu tunaouanza kwa mfano, miaka miwili ijayo, mitano na hata miaka kumi ijayo utakapokuwa sekondari au chuo?” Tukagawiwa vikaratasi vya njano. “Unaweza kuandika mambo mengi upendavyo hata 30 ukitaka na wala si lazima uwe na hakika navyo.” Tukaorodhesha ndoto nyingi kadri tulivyoweza. Kwa kawaida ndoto huwa hazina ukomo. Unaota tu.


“Ukimaliza kuorodhesha sasa uweke namba mbele ya kila ndoto yako. Kama unataka kifanyike ndani ya mwaka mmoja, andika moja. Ukiona ni cha miaka miwili weka, mbili, cha miaka mitano, andika tano na kadhalika.” Tukafanya hivyo.


Nikapewa kazi ya kuvikusanya vikaratasi hivi. Nikavibandika kwenye ubao na kuvisoma. Nilifurahi kuona kila mtu bila kujali umri wake ana ndoto zake. Ndoto hizi ni muhimu ziheshimiwe. Hakuna ndoto ndogo. Hakuna ndoto ya kupuuzwa. Kila mjumbe wa 'Halmashauri Kuu' ana haki ya kuota ndoto. 


Kama kuna kosa tunaweza kufanya kwenye ngazi ya familia ni kupuuza au kuzima ndoto ya mtu. Hatukupenda kuwa aina hiyo ya familia. Tunatambua tofauti yetu sisi wanadamu na viumbe wengine ni ndoto. Kinachotupa nguvu ya kupambana na maisha ni ndoto zetu. Mwanadamu akikosa ndoto anakuwa kitu cha ajabu. Hata mtoto wa miaka sita ukimuelewesha vizuri anaweza kabisa kukwambia anatamani nini na ukamsaidia kuitengeneza vizuri ndoto yake. Hiyo ndiyo kazi ya 'Kamati Kuu' ya familia itakayokaa kesho.


Basi. Ulifuata mjadala mrefu wa kuunganisha mawazo yetu ili angalau yazungumze lugha moja. Changamoto kubwa kwenye familia ni kila mtu kuota ndoto yake isiyo na ushirikiano na ndoto za wengine. Hatukutaka ndoto za wajumbe zipigane. Ikabidi kwanza kila mmoja achangue malengo yake makubwa zaidi kwa umuhimu kisha tukayaweka kwenye makundi ya pamoja kwa kuzingatia mfanano wake. Zoezi hili lilitengeneza malengo ya kielimu, kikazi, kifamilia, kiroho, burudani na kadhalika.


Kisha tukafanya kazi ya kutafakari malengo hayo kwa kujibu swali, “Kwa nini?” Kama mwenye ndoto kaandika, “Kufaulu vizuri mtihani wa darasa la saba,” anatakiwa kujibu kwa nini unataka kufaulu. Baada ya hapo tulizitafakari hizo, “Kwa nini” na tukapata namna ya kuunganisha malengo yetu. Tulitumia muda mrefu kwenye hatua hii lakini ilitusaidia kuelewana.


Agenda ya mwisho nikaisoma mimi, “Ili kutimiza malengo haya, unahitaji kuwa mtu wa namna gani? Unahitaji kuacha tabia zipi na kujifunza tabia zipi mpya?”

PICHA: Ndoto za mjumbe 


Hapa tukajikita kwenye gharama ya kutimiza ndoto zetu. Sababu moja wapo ya ndoto nyingi kutokutimia ni hulka ya kukwepa gharama. Kwa kutumia vikaratasi vya bluu, tulijitazama kwa jicho la mabadiliko ya kitabia na kimtazamo kama gharama inayohitajika kujitengeneza tufananie malengo tuliyojiwekea.


Katika kujadiliana, tukaona haja ya kujifunza mambo mapya, kujenga nidhamu, bidii na uwajibikaji. Tuliona haja ya uwazi, kuomba msaada, na kusaidiana kila inapobidi na kujisikia fahari kumsaidia mwenzako kufikia malengo yake. Maeneo haya tuliyapandisha hadhi ya kuwa tabia na miiko ya familia. Tukaahidi kusimamia miiko hiyo kama sheria zinazotuongoza kutimiza malengo yetu.


Hatujawahi kuwa na kikao cha mtindo huu. Kikao hiki ni cha kwanza. Lakini tuliondoka hapo tukiwa tumechora ramani ya wapi tunakoelekea kama familia.  Katika hatua hii, niliona vile watoto walivyofurahi kujua wao ni sehemu muhimu ya mipango yetu sisi wazazi wao. Kazi yetu sisi wazazi ni kuyachambua matamanio hayo yawe na sura ya kutekelezeka. Tulikubaliana kuwa na vikao vya kila mwezi kujifanyia tathmini. 


Niandikie: bwaya@learninginspire.co.tz


Maoni

  1. Utaratibu huu ni mzuri sana Bwaya. Assnte kwa kutushirikisha hili.

    JibuFuta
    Majibu
    1. Asante sana Albert kwa kuisoma pia.

      Futa
  2. Nimefurahishwa sana kukutana na makala hii imenipatia kitu kipya kabisa na nimeona umuhimu wa kushiriki pamoja mipango ya familia

    JibuFuta
    Majibu
    1. Asante sana kwa kujifunza jambo.

      Futa
  3. Makala hii haijaniacha jinsi nilivyo. Hakika nimejifunza

    JibuFuta
    Majibu
    1. Hongera sana kwa kujifunza jambo

      Futa
  4. Nimetoka kujifunza kwa undani hili swala na hapa nimepata mfano mzuri sana.
    Kumbe sio wazazi tu wanapaswa kuweka malengo ila ni familia nzima inapaswa kushiriki ili kujenga tabia nzuri kwao hata baadae! Kazi nzuri ndugu!🙌🏿

    JibuFuta
    Majibu
    1. Karibu sana ndugu. Naamini nawe utaona inavyokuza uwajibikaji wa pamoja. Usisite kutushirikisha uzoefu wako kikao kitakapokaa.

      Futa
  5. Asante sana nami nitashirikisna na mume wangu tuweze kuangalia namna ya kuendesha baraza letu umetufungua macho. Ubarikiwe

    JibuFuta
    Majibu
    1. Karibu sana. Usisite kutushirikisha uzoefu wako baada ya Baraza la Wadhamini kukaa.

      Futa
  6. Umetisha sana na wewe una huduma na kipawa Cha ajabu sana mtumishi Bwaya na Mungu akubariki sana kutushirikisha Jielewe. Mungu awape mwanzo mwema wa Mwaka 2023. George Bisani

    JibuFuta
  7. Hakika Mungu anakutumia kuponya watu wake, asante sana nimejifunza jambo jipya leo ktk makala hii, kweli vikao vya familia ni muhimu sana. Be blessed

    JibuFuta
  8. Barikiwa sana umenifunza kitu Cha pekee kwakweli 👌 Mungu akutunze uendelee kufumbua wengi zaidi na Zaid mwl.

    JibuFuta
  9. Nimependa sana andiko lako limeniongezea kitu kwenye maisha yangu. Binafsi niliwahi kijiwekea malengo kama haya lakini changamoto kubwa inakuja kwenye utekelezaji na kikwazo siku zote ni bajeti ya kutekeleza kile ulichopanga. Naomba mawazo kutoka kwako na kwa wengine juu ya njia za kutatua changamoto ya ukosefu au uhaba wa bajeti

    JibuFuta
  10. Appreciate haya madini ndio hitaji la wengi lakini wengi wetu hatupati Kwa wakati mwafaka

    JibuFuta
  11. Habari zenu. Ilikuwa ngumu sana kwangu wakati mpenzi wangu aliniacha kwa mwanamke mwingine. Niliharibiwa kihisia, nilivunjika moyo na sikujua la kufanya ili kumrudisha. Nilihangaika kwa miezi mingi na niliendelea kutafuta msaada kutoka kila mahali hadi nilipopata kujua kuhusu DR DAWN. Niliwasiliana naye na kumweleza shida zangu. Alikuwa tayari kunisaidia na kunisisitiza nifuate taratibu ili aweze kurejesha penzi kati yangu na mtu wangu na pia kuhakikisha tunarudiana wote wawili. Nilipata mahitaji yote na ilifanya kazi hiyo. Baada ya saa 48, nilipata ujumbe kutoka kwa mpenzi wangu akiniuliza tarehe. Sasa tuko pamoja tena na shukrani zote kwa DR DAWN. Anaweza kukusaidia kumrudisha mpenzi wako,
    Anaweza kukusaidia na uchawi wa ujauzito,

    Anaweza kukusaidia kuponya aina yoyote ya ugonjwa.

    ikiwa uko tayari kuamini na kubaki na matumaini. Watumie barua pepe tu kupitia: dawnacuna314@gmail.com
    WhatsApp: +2349046229159

    JibuFuta
  12. 75r17 สล็อต เว็บไซต์ตรง ฝากถอนไว ไม่มีอย่างน้อยปัจจุบัน ให้บริการลงทะเบียนเป็นสมาชิก เล่นเกมพนันครบวงจรสูงที่สุด pgslot โดยเปิดให้เล่นให้บริการแต่ว่าเกมสล็อตแตกง่ายที่สุด

    JibuFuta
  13. Riches 909 เข้าสู่ระบบ พร้อมที่จะเดินทางสู่ความรุ่งเรืองและความสำเร็จหรือยัง? ค้นพบความลับของ PGSLOT และสามารถเปิดโอกาสในการเปลี่ยนชีวิตไปสู่ขั้นตอนใหม่!ส่วนใหญ่คนจะต้องการที่จะเป็นเช่นนั้น

    JibuFuta
  14. olxtoto เป็นการมีความสัมพันธ์ที่ร้ายแรงกับคนอ่าน pg slot เว็บให้ความใส่ใจกับข้อคิดเห็นแล้วก็คำวิพากษ์วิจารณ์ของนักอ่านอ่านสามารถมีส่วนร่วมสำหรับเพื่อการอภิปรายและก็แบ่งปัน

    JibuFuta
  15. ufa wallet slot สำรวจโลกของยูฟ่าวอลเล็ตสล็อตที่ทำให้ความบันเทิงรวมถึงความตื่นเต้น! ค้นพบเคล็ดลับที่ดีที่สุด PG วิธีการและกลยุทธ์ในการเพิ่มประสบการณ์ในการเล่นเกมของคุณในขณะ

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?

Pay $900? I quit blogging