Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2014

Mahusiano ya kimapenzi yanavyoweza kuanzishwa bila kutarajiwa

Picha
Unaweza kushangaa lakini ndio ukweli wenyewe kwamba upo uwezekano mkubwa kabisa wa kuanzisha na kuendeleza mahusiano na mtu yeyote bila kujali mwonekano wake, tabia yake na imani yake. Katika makala haya tunaeleza kanuni za kimaumbile zinazoongoza mahusiano ya watu wawili ambao mara nyingi watu hao hukutana kwa njia ya nasibu.

Waajiri wanajifunza nini kupitia Mradi wa ILO unaotambua na kukuza ujuzi usio rasmi?

Picha
Shirika la Kazi Duniani hapa nchini, ILO, kwa ushirikiano na wadau wengine wa kazi na ajira hapa nchini wameanzisha mafunzo ya aina yake yanayolenga kutambua na kukuza ujuzi usiorasmi hivyo kuchangia kutatua changamoto hiyo. Kupitia mafunzo maalum yanayoitwa uanagenzi (apprenticeship), ambayo kwa sehemu kubwa hutolewa mahali pa kazi, mwajiriwa mwenye ujuzi usiotambuliwa rasmi anawekewa mazingira rafiki yanayowezesha ujuzi wake kutambuliwa rasmi na inapobidi, kuwezeshwa kupata mafunzo yanayoimarisha ujuzi alionao ili kufanya kazi zenye staha na kwa ufanisi wakati huo huo akiendelea na kazi.

Makundi Makuu Matano ya Waislamu

Mchekeshaji mwenye asili ya Pakistani, Sami Shah, anachambua makundi makuu matano ya wa-Islam.  Pengine hujawahi kuyasikia kama mimi na ungependa kujua umeangukia kundi lipi. Bonyeza hapa kusoma makala hiyo , ambayo kimsingi imekusudiwa kukufanya ucheke na kufurahi wakati huo huo, ukitafakari kwa kina kile hasa kinachokuchekesha.

Dhana ya 'mapenzi' kwa mtazamo wa kisaikolojia

Picha
Makala haya yanasaili namna mtazamo wa awali wa watu wanaoamua kuingia katika uhusiano wa kimapenzi unavyoweza kuathiri kwa kiasi kikubwa namna wawili hao watakavyohusiana. Na tunaonesha namna kiwango cha mapenzi kati yao kinatengemea masuala matatu makuu; Ukaribu wa kihisia, tamaa ya mwili na maamuzi yao.

Mambo Yanayoweza Kumvutia Mwanamume kwa Mwenzi Wake -2

Picha
Tuliona katika makala yaliyopita kuwa mwanaume anahitaji sana kutambuliwa uwezo wake. Huna sababu ya kumwambia mwanaume unampenda. Lugha ya upendo anayoielewa zaidi ni kusifiwa uwezo wake. Sambamba na hili la kwanza, tuliona mwanaume anayo njaa ya heshima. Heshima ni kumtii na kumstahi hata pale anapokuwa mkosaji kwa lugha, maneno na tabia. 

Mambo Yanayoweza Kumvutia Mwanamume kwa Mwenzi Wake -1

Picha
Swali hili huulizwa na karibu wanawake wote wanaotamani kuwa na uhusiano wa kudumu na wanaume. Kwamba mambo yepi hasa yanayoweza kumvutia mwanaume pale anapoanzisha uhusiano na mwanamke. Ingawa zipo tofauti ndogo ndogo miongoni mwa wanaume, kwa ujumla, uchambuzi wa tafiti mbalimbali za mahusiano unabainisha mambo kadhaa yanayowaunganisha wanaume wengi kimahitaji. Tuyatazame katika mfululizo wa makala hizi.

Kushinda Vikwazo vya Jitihada za Kumpa Mwenzi Anachostahili

Picha
KUYAELEWA mahitaji ya kihisia ya mwanamke ni suala moja, lakini kuuishi uelewa huo ni jambo jingine kabisa. Yapo mambo mengi tunayoyafahamu na tunajua kuyaelewa lakini hatuyaishi. Tujua kwa kina lakini hakuna tunalolitenda. Matokeo yake tunatenda tusiyoyajua na tunayoyajua hayatusaidii kubadili maisha yetu. Katika makala haya, ningependa kusimulia changamoto nilizokumbana nazo katika kupambana na utamaduni niliokulia wa kupuuza mahitaji ya msingi ya mwanamke.

Kama mwanaume, uko tayari kulipa gharama za mahusiano bora?

Picha
UNAPOWASIKILIZA wanaume wengi wakizungumzia kile wanachodhani wao kinawagusa wanawake kwenye mahusiano, utashangaa orodha ya vitu hutawala mazungumzo. Kwa mwanaume wa kawaida, mwanamke anahitaji vitu ili akupende. Utasikia, "Ah, mwanamke pesa. Ukiwa na hela zako bwana, basi." Imani ni kwamba wanawake wanahitaji sana vitu na hivyo ndivyo vinavyowavuta na kuwabakiza kwenye mahusiano. Pamoja na ukweli fulani kwamba vitu navyo vina nafasi yake kwenye mahusiano, hasa kwenye kizazi hiki cha sasa kinachotanguliza thamani ya fedha kuliko kitu kingine chochote, bado huwezi kuthamanisha moyo wa mwanamke na fedha, ingawa ni kweli anazihitaji. Kudhani kwamba baada ya kuhakikisha mwanamke amepata kila anachokihitaji kwa maana ya vitu, basi unaweza kuendelea na shughuli nyingine kwa kuamini umemaliza kazi, ni kutokuelewa mahitaji halisi ya kihisia ya mwanamke. Najua wapo wanawake wasiohitaji kingine chochote kwa mwanaume zaidi ya fedha na vitu. Mahitaji ya kihisia tunayoyaz

Msingi wa mahusiano si matarajio bali kutambua na 'kushibisha' mahitaji ya kihisia ya mwenzi wako

Picha
NI VIGUMU kwa kijana aliye kwenye kilele cha msisimko wa mapenzi hii leo kudhania bashasha hiyo inaweza kabisa kugeuka kuwa hasira, uchungu, na kushuhudia ile shauku ya kuongea, kusikiliza, kutaniana na mpenzi wake huweza kupotea so naturally kwa jinsi hiyo hiyo mapenzi yalivyoanza. Aliyewahi kusema upo mstari mwembamba mno unaotenga mapenzi na chuki, alilitambua hili. Kwa jinsi msisimko wa mwanzo wa kimapenzi unavyokuwa-ga mkubwa, huwa haingii akili kwa kijana anaposikia kwamba wapo wanandoa huweza kuchelewa kurudi nyumbani katika jitihada za kujaribu kuyakimbia matatizo na wenzi wao. Kijana anashindwa kuelewa inakuwaje watu wawili wanaopendana kwa dhati, wanaweza kufikia mahali pa kutamani kuzungumzia matatizo yao kwa uwazi, lakini wasiweze, wakatamani kuwa karibu kihisia, wasiweze. Haya yote pamoja na kuwa mabaya kuyasikia, huweza kumpata mtu yeyote, tena mwenye mapenzi mazito, hatua kwa hatua. Mahusiano ni suala zito lakini linalowezekana Tunapoyasema haya, hatukusudii kum

Namna mahitaji ya kihisia ya wenzi yanavyosababisha misuguano ya kimahusiano na ndoa

Picha
PAMOJA na dini nyingi kubwa kupiga marufuku talaka kwa waumini wake, takwimu rasmi za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) zinaonyesha kwamba talaka nchini zimeongezeka kwa asilimia 49 katika kipindi cha mwaka 2007 hadi 2009. Kwa upande wa Zanzibar pekee, tunaambiwa, asilimia 95 ya migogoro 1,753 ya ndoa iliyosajiliwa kwenye Mahakama ya Kadhi nchini humo iliishia kwa talaka. Hali inatisha, au sio? Katika hali halisi, shauri ya utamaduni wa kuyaonea aibu masuala ya kuachana, hali inaweza kuwa mbaya zaidi. Watu wengi wanaweza kuwa wanaugulia maumivu ya ndoa na kuamua ama kufa na tai shingoni, au kutafuta 'michepuko' ya hapa na pale katika jitihada za kupunguza maumivu. Katika nchi za Ulaya, ambako kidogo kuna uhuru wa mtu kufanya atakalo ikiwa ni pamoja na kuomba talaka, hali ni tete zaidi. Kwa mfano, tunaambiwa, wakati idadi ya ndoa zinazofungwa mwaka 2010 ilipungua kwa asilimia 39 barani humo, talaka zimeongozeka kwa asimilia 200 katika kipindi cha mwaka 1979 mpa