Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Global Voices

Wafilipino Walivyomficha Papa Francis Hali Mbaya ya Haki za Kijamii Nchini Humo

Picha
Makundi ya haki za kijamii yalizuiwa na Polisi kukaribia msafara wa Papa Francis. Picha kutoka kwenye ukurasa wa facebook wa Kathy Yamzon

Siku ya Blogu Oktoba 16: Shiriki Kujadili Dhana ya Kutokuwepo kwa Usawa

Picha
Tangu 2007, Siku ya Wajibu wa Blogu Duniani imekuwa ikitumika kuwaweka pamoja wanablogu kutoka duniani kote ili kujadili mada muhimu zinazokuwa zimewekwa mezani. Siku hiyo, wanablogu kwa pamoja, huwa utaratibu wa kuvamia anga la blogu kwa kuchapisha maelfu ya posti kuhusu masuala ya maji, mabadiliko ya tabia nchi, umasikini, chakula na nguvu ya pamoja. Kwa mara nyingine mwaka huu, Global Voices Online inayo fahari kuwa mshirika rasmi wa siku hiyo.

Makundi Makuu Matano ya Waislamu

Mchekeshaji mwenye asili ya Pakistani, Sami Shah, anachambua makundi makuu matano ya wa-Islam.  Pengine hujawahi kuyasikia kama mimi na ungependa kujua umeangukia kundi lipi. Bonyeza hapa kusoma makala hiyo , ambayo kimsingi imekusudiwa kukufanya ucheke na kufurahi wakati huo huo, ukitafakari kwa kina kile hasa kinachokuchekesha.

Unaweza kuwa mzazi bora zaidi kwa kujifunza kwa wazazi wako

NI UKWELI kwamba katika suala la malezi, hakuna kitu unachoweza kukiita 'the obvious'. Hakuna uzoefu. Na tunahitaji kujifunza kwa wengine. Ndivyo anavyofanya mzazi mmoja nchini Panama, Joel Silva Díaz , anayeandika uzoefu wake wa kimalezi katika blogu yake . Lengo lake ni kushirikisha wasomaje wake kile anachodhani kinaweza kuwasaida watu wenye kiu ya kujifunza. Anasema,  Sikumbuki kuwa na mazungumzo ya zaidi ya mistari mitano na baba yangu. Ni miaka kumi na zaidi imepita. Kwa matukio ya hapa na pale kati yangu na baba yangu, naweza kusema tu ni kwamba angalau nilikuwa na baba. [...] Na hicho ndicho ninachotaka kukifanya vizuri zaidi, nataka kuwa baba anayefanya bila hata kutambua, nataka kuwakumbatia, kuwabusu, kuwapa fursa bora za kufanya maamuzi bora na kuwasaidia wanapokuwa hawajafanya chema, sichelewi kuwonyesha upendo na kuwajali, hata kama kuna nyakati naweza kweli kuwafinya. [...] Kama mzazi, nisingependa  niwe mtu wa kuwachungulia wanangu kila baada ya ma...

Mitaa ya Nairobi, 'Usomini UoN'

Picha
Chuo Kikuu cha Nairobi, kinachosemekana kuwa moja wapo ya vyuo bora Afrika Mitaa ya Chuo Kikuu cha Nairobi Ndani ya Chuo, karibu na duka la vitabu Bustani za wazi katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Nairobu Kama ni kweli, sehemu hii haihusiki basi sawa sawa Sijui nielekee wapi, huku au kule? Alama ya utambulisho wa Chuo Kikuu cha Nairobi

Ya Santiago na nguvu za Kiraia

Mkutano uliokusanya wanablogu, wanahabari, wanaharakati na wanateknolojia watokao katika nchi mbalimbali umemalizika. Siku mbili za mwanzo zilihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali kutoka hapa Chile na sehemu nyinginezo ikiwa ni pamoja na Kampuni za google, Yahoo, You tube na wengineo. Kilichokuwa muhimu sana katika siku hizo mbili za mwanzo, ni kutizama mifano ya namna uandishi wa kiraia (mablogu, twita, facebook, simu nk) ulivyoweza kushika kasi katika nchi mbalimbali zinazoendelea. Unaweza kusoma muhtasari hapa kuona namna blogu zinavyoleta mageuzi nchini Madagaska kupitia jumuiya ya wanablogu iitwayo Foko . Nilizungumza na Lova Rakotomalala juzi na nilishangazwa na jinsi jamaa wanavyoweza kufanya mambo makubwa katika mazingira magumu yanayofanana na yetu. Madagaska wamekuwa mfano mzuri wa nguvu ya uandishi wa kiraia. Siku zile mbili za mkutano zilitupa ushahidi wa wazi wazi wa namna uandishi wa kiraia unavyopamba moto katika nchi zinazoendelea. Bofya hapa uone mifano mic...

Mkutano wa wanablogu Santiago

Picha
Nimepata fursa ya kukuhudhuria mkutano wa wanablogu wa jumuiya ya Global Voices unaofanyika kwenye Ukumbi wa Maktaba ya Taifa, Santiago Chile. Moja ya vivutio vya mkutano huo ni kukutana na mwanablogu wa kitanzania aishiye Australia Bw. Joe Nambiza Tungaraza na Njeri Wangari mwanablogu wa mashairi wa Kenya .

Tangazo la Mkutano Mkuu wa Uanahabari wa Kiraia wa Global Voices 2010

Picha
Mkutano wa wanablogu wa Global Voices, utafanyika Mjini Santiago mwezi Mei tarehe 6 na 7 mwaka huu. Nimezipata habari hizo kupitia ukurasa wa kiswahili wa mradi wa Lingua Swahili . Nimetamani kama na sisi tungekuwa tunapanga kukutana siku fulani mwaka huu! Inawezekana! Ni muhimu tuanze kufikiri kukutana uso kwa uso hata kama matanga ya ile Jumuiya yetu hajapita bado.

Global Voices: Dunia inaongea, unasikiliza?

Picha
Nimeamua kukata shauri na kujiunga na Jamii ya wanablogu wa Global Voices katika ukurasa wa Kiswahili . Ninajitolea kuusogeza ujumbe karibu na wasomaji wa kiswahili kwa kutafsiri makala zinazoandikwa na wanablogu wengine. Global Voices kimsingi ni jamii ya wanablogu kama 200 waliopo duniani kote ambao wanafanya kazi kwa pamoja kukuletea tafsiri na ripoti za yanayojiri kwenye ulimwengu wa blogu na uandishi wa kiraia. Global voices inapaza sauti ambazo kwa kawaida huwa hazisikiki katika vyombo vya habari vya kimataifa. Bonyeza hapa kusoma zaidi kuhusu jamii hiyo, halafu ukaribie kuchangia maoni kwenye ukurasa huo wa Kiswahili na kubadilishana mawazo na wanablogu wengine. Ndesanjo Macha , mtu aliyefanya kazi kubwa kutangaza teknolojia ya blogu kwa lugha ya kiswahili nchini na mmoja wa wahariri waandamizi wa Jamii hiyo, alikuwa na na haya ya kusema.