Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mwandishi mwalikwa

Wafilipino Walivyomficha Papa Francis Hali Mbaya ya Haki za Kijamii Nchini Humo

Picha
Makundi ya haki za kijamii yalizuiwa na Polisi kukaribia msafara wa Papa Francis. Picha kutoka kwenye ukurasa wa facebook wa Kathy Yamzon

Miaka miwili ya Kuwa 'Mama' Ina Mafunzo Makubwa Kwangu...

Picha
Nilipoamua kuchukua uamuzi wa kubadilishana majukumu na mke wangu sikujua ni kwa jinsi gani uamuzi huo ungenibadilisha mimi na kunipa mtazamo mpya kabisa katika maisha. Baada ya kuzaliwa Baraka siku kama ya leo mwaka 2012 tuliamua kubadilishana majukumu ya familia; mimi nibaki na kuangalia watoto na kutunza nyumba na mahitaji yake yote na mke wangu aendelee kufanya kazi na kusaidia wakati wowote anaoweza.

Mwaka unakatika....Tumesonga mbele ama nyuma???

Picha
Nashukuru kwa blogs na tovuti mpya ambazo zinachipuka na kuendeleza nia njema ya kuigusa jamii. Ningependa tuanze kwa kujiuliza, 'Je! Tunasonga mbele ama nyuma katika harakati zetu?' ...kwa ujumla, haijalishi ni sababu gani ilikufanya u-blog, mwisho wa safari sote tunajikuta na zao moja ama "mlaji" mmoja ambaye ni JAMII.

Mahusiano ya kimapenzi yanavyoweza kuanzishwa bila kutarajiwa

Picha
Unaweza kushangaa lakini ndio ukweli wenyewe kwamba upo uwezekano mkubwa kabisa wa kuanzisha na kuendeleza mahusiano na mtu yeyote bila kujali mwonekano wake, tabia yake na imani yake. Katika makala haya tunaeleza kanuni za kimaumbile zinazoongoza mahusiano ya watu wawili ambao mara nyingi watu hao hukutana kwa njia ya nasibu.

Makundi Makuu Matano ya Waislamu

Mchekeshaji mwenye asili ya Pakistani, Sami Shah, anachambua makundi makuu matano ya wa-Islam.  Pengine hujawahi kuyasikia kama mimi na ungependa kujua umeangukia kundi lipi. Bonyeza hapa kusoma makala hiyo , ambayo kimsingi imekusudiwa kukufanya ucheke na kufurahi wakati huo huo, ukitafakari kwa kina kile hasa kinachokuchekesha.

[VIDEO]: Mazungumzo na Liberatus Mwang'ombe na Solomon Chris baada ya Uchaguzi DMV

Picha
Mubelwa Bandio kati akiwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi za Mwenyekiti wa Jumuiya DMV Liberatus Mwang'ombe (L) na mgombea nafasi ya Katibu Msaidizi Solomon Chris (R0 wakati wa mahojiano Agosti 9, 2014, Jumuiya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia nchini Marekani ilifanya uchaguzi wake mkuu. Matokeo yake yamekuwa yakipingwa na waliokuwa wagombea wa uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali. Wamaketi na Vijimambo Blog na Kwanza Production kueleza sababu hasa za kupinga matokeo hayo siku ya Jumatano ya Agosti 13, 2014. Karibu uungane nasi kusikia wanachopinga

Hotuba ya Mhe Kikwete akizungumza na wa-Tanzania waishio Washington DC

Picha
Karibu kusikiliza hotuba ya Mhe. Dk Jakaya M Kikwete alipozungumza na waTanzania usiku wa Agosti 2, 2014 kwenye hotel ya Marriot, jijini Washington DC nchini Marekani. Kwa hisani ya Mubelwa Bandio.

Kanuni muhimu za kuwa baba anayejua wajibu wake

Da'Subi wa blogu maarufu ya habari wavuti.com ameweka makala yenye kanuni muhimu kwa wale wanaotaka kuwa akina baba bora. Makala hiyo iliandikwa awali kwa Kiingereza na Leo Babauta ambaye amekuwa baba kwa miaka 21 na ana watoto sita. Leo anayataja mambo matano muhimu ikiwa unataka kuwa baba anayejua wajibu wake kwa watoto wake. Hapa tumeyaeleza kwa ufupi kwa lugha ya Kiswahili: Upendo. Huu ndio wajibu mkuu kuliko wajibu wowote unaoweza kuwa nao kama baba. Anasema kuwapa chakula, malazi, mavazi ili wakue, si kazi ngumu. Kazi ni kumfanya mtoto ajisikie kupendwa, hali ambayo ndiyo itakayofinyanga tabia yake ukubwani. Kipimo cha mafanikio ni ikiwa unaweza kumfanya mwanao ajisikie kupendwa, Kuwa mfano. Maisha unayoishi yana maana kubwa kwa wanao kuliko maneno unayowaambia. Unachofanya ndicho kinachochukuliwa serious. Ukizoea kuwaadhibu, ndicho wanachojifunza. Ukiwabana sana, hawajifunzi kutushirikisha walivyonavyo. Kama unataka wanao wale chakula bora, anza wewe. Ukitaka wasome...

Mahojiano na washiriki wa maonyesho ya Utamaduni wa Kenya Washington DC

Picha
Kati ya Juni 25 na Julai 6, jiji la Washington DC lilikuwa mwenyeji wa maonyesho ya kila mwaka ya yanayohusu maisha a watu na jamii mbalimbali. Mwaka huu, nchi ya Kenya ilishirikishwa, wakionyesha utamaduni wao na changamoto za kuzidumisha katika zama hizi za sayansi na teknolojia. Kwanza Production ilipata fursa ya kutembelea maonyesho hayo na kuzungumza na baadhi ya washiriki wa maonyesho hayo ambapo walieleza mengi ya kufurahisha. KARIBU UUNGANE NASI Zaidi ya washiriki 100 kutoka nchini Kenya waLIkuja hapa jijini kuonyesha mambo mbalimbali kama kutengeneza vyungu kwa ufinyanzi, uchongaji vinyago, mapambo ya shanga, useremala, nakshi za majengo, ujenzi wa majahazi, mapishi , muziki na mengine yanayotunza utamaduni wa nchi hiyo Maelezo ya ujenzi na sehemu za JAHAZI (DHOW) toka kwa Ali Skanda aliyetoka Lamu Kenya Na mtangazaji mkongwe abdushakur Aboud mbele ya Jahazi lililoletwa kwenye makumbusho ya hapa Washington DC kutoka Lamu nchini Kenya Mtaalamu wa ...

Nilipozungumza na blogu ya Maneno Matamu: “Kiswahili ni alama ya Uafrika wangu.”

Picha
Yafuatayo ni mahojiano yangu na blogu ya Maneno Matamu kuhusu, pamoja na mambo mengine, suala la lugha za Kiafrika na nafasi ya blogu katika kukuza lugha hizo katika enzi hizi. Ulianza kuandika blogu mwaka 2005. Uliamuaje kushiriki katika mtandao wa Internet namna hii? Nakumbuka nikiwa mwanafunzi nilikuwa mfuatialiaji mzuri wa makala za mwandishi maarufu,   Ndesanjo Macha   (ambaye sasa ni Mhariri wa Global Voices eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara). Yeye ni mwanablogu wa kwanza wa Kiswahili. Na kwa kweli niilivutiwa sana na aina yake ya uandishi, mijadala aliyokuwa akiiendesha kwenye blogu yake pamoja na matumizi mazuri ya lugha. Kwa hiyo hamasa ya kublogu ilitokana na  blogu yake . Blogu kwangu niliiona kama fursa nzuri na rahisi ya kujadili masuala ninayoyaelewa vizuri ya kiutambuzi na sayansi. Mule niliona ingekuwa rahisi kupata jukwaa la kubadilishana mawazo na watu bila kikwazo chochote na pia p...

Umemsoma Dambisa Moyo?

Picha
Kama una mpango wa kusoma kitabu kimoja tu mwaka huu, napendekeza hiki cha Dambisa Moyo kiitwacho "How the West was Lost". Ukikisoma utaelewa zaidi kwa nini hawa watawala wanaoitwa "The darling of the west" wanaopigana vikumbo kuhudhuria mkutano wa G8, wamepotea njia. Anacho kingine alichokiandika kabla ya hiki, kiitwacho cha Dead End, bado nakitafuta. Naambiwa ni moto.

Tunapenda ushirikina kuliko vitabu - Prof. Mbele

Picha
"...Umaafuru wa kitabu hiki (Rich Dad Poor Dad) nilianza kuusikia huku Marekani, miaka michache iliyopita. Ni kati ya vitabu vingi ambayo vinasomwa na hao wenzetu, wakati jamii yetu ya Tanzania inaendelea kuzama katika giza au tunangojea kiongozi wa nchi au serikali ituletee maendeleo, na tukijitahidi sana, tunatumia ushirikina. Tuko tayari kulipa laki nyingi kwenye mambo ya ushirikina, eti tupate mafanikio, badala ya kununua vitabu na kuvisoma. Sasa basi, pamoja na vibuyu vyetu, wenzetu wa-Kenya, ambao wamezingatia elimu tangu zamani, wanaingia nchini mwetu na kujichukulia ajira au kuanzisha miradi. Sisi bado tunahangaika na vibuyu badala ya vitabu. Tutakoma, maana wahenga walisema kuwa asiyefunzwa na mamake hufunzwa na ulimwengu. Na bora iwe hivyo, labda hatimaye tutapata akili. Uzembe ulivyokithiri miongoni mwa wa-Tanzania, utawasikia wakilalamika mbona kitabu hiki hakijaandikwa kwa ki-Swahili? Wakishauliza hivi, wanaamini wametoa hoja nzito, badala ya kutambua kuwa wana...

Ujumbe wa wiki hii

Picha
NAANDIKA makala hii kwa moyo wa upendo, mtu unayempenda ni lazima umwambie ukweli. Ukimficha ukweli unakuwa humpendi; ni kweli ukweli unauma na mara nyingi hatupendi kabisa kusikia ukweli; hata hivyo hakuna wa kutengua kwamba msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Kwa vile Mungu hatukutani naye uso kwa uso, bali tunakutana naye kupitia kwa binadamu wenzetu; ni haki kusema kwamba msema kweli ni mpenzi wa watu? Naandika kutoa ushauri na hasa maoni yangu ambayo ni ya nia njema kwa taifa letu la Tanzania. (Picha ya Kijiji cha Mjengwa) Hii ni aina ya barua ya wazi kwa wale wanaotamani kuendelea kutawala wakati miaka ya kustaafu inakaribia. Labda kuna haja ya kuongeza miaka hii ya kustaafu. Miaka sitini ya sasa watu wanakuwa bado wana nguvu na kutaka kuendelea kutumika au kula “utamu” wa uongozi. Kwa vile sasa hivi umri huu haujasogezwa mbele, kuna haja kuwakumbusha ndugu zetu ambao bado wana “Ambition” ya kutaka kuendelea na mbio hizi za hata kukalia viti muhimu kama urais na uspika, kwa...

Mjadala wa dini na sayansi unaendelea...

Najaribu kupangilia mambo yangu niweze kujadili masuala ya dini wakati wowote kuanzia sasa. Wadau wa masuala haya ninawakaribisha nyote. Jana nilianza kwa kujiuliza swali kuu: Je, ni dini inaiogopa sayansi ama sayansi ndiyo inayoiogopa dini? Mdau wa mjadala huo, Profesa Matondo alikuwa na mchango huu wa kusisimua: ' ''Hili ni suala zito ambalo limehangaisha mafilosofa kwa muda mrefu sana. Kuna mambo ambayo sayansi haijaweza kuyaeleza. Dini kwa upande wake, kwa vile haihitaji vithibitisho kama vile sayansi, inaweza kujibu kila kitu kwa mwenye imani. Kuna mzozo mkubwa sana unaendelea hapa Marekani kuhusu ufundishaji wa nadharia ya Evolution ya Charles Darwin. Walokole wa hapa Marekani wanataka ama ifutiliwe mbali kufundishwa mashuleni au uumbaji (creationism) wa Mungu pia nao ufundishwe kama nadharia mbadala (alternative theory). Wanasayansi wanabisha kwamba uumbaji hauwezi kuthibitishwa kisayansi kama kweli ulitokea na kwa hivyo hauwezi kufundishwa mashuleni. Sij...

Je! Yesu ni Mungu?

Haya ni maoni ya mdau asiyependa jina lake lijulikane. Nimeyatundika hapa kwa sababu ya uzito wa anachokisema. Tafadhali soma na kama unaweza changia maoni yako tuelimike. Nimshukuru sana kwa kutumia muda wake kuandika maoni yake na hapa namnukuu: MAKANISA ya Kikristo yanafunza ya kuwa Yesu Kristo si kama kuwa ni Mwana wa Mungu tu, bali hakika ni Mungu khasa. Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni mmoja. Watatu katika mmoja, na mmoja katika watatu. Wote ni wa milele, wote ni sawa. Yesu ni Mungu, na Mungu ni Yesu. Hiyo ni imani ya Kikristo, ambayo inaaminiwa na karibu Wakristo wote. Hebu tuifunue Biblia tutazame inasema nini katika jambo hili? Mt Paulo katika barua yake ya kwanza kuwapelekea Wakorintho aliandika: Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi. 1 Wakorintho 15.15 Juu ya kuwa Paulo anaambiwa ya kuwa akiamini kuwa Masihi (yaani Kristo) na Mwenyezi Mungu ni ki...

Soma maoni marefu ya Silas Jeremia

Msomaji aliyejitambulisha kama Silas Jeremia amenitumia waraka mrefu kupitia barua pepe leo. Aliniandikia SMS akiniarifu kuwa ameshindwa kuweka maoni yake kwenye blogu (Nadhani ni kwa sababu mchango wenyewe ulikuwa mrefu kuzidi kiasi cha meneno yanayoruhusiwa kuwa maoni kwenye blogger.) Nami nikamwelekeza kutumia barua pepe ambayo ni njia rahisi kwake. Kwa kuheshimu mchango wake, kama wasomaji wengine, nimeona ni vyema niu –paste mchango wake hapa kusudi upate hadhira inayohusika kwa majadiliano zaidi: " Naomba kutoa maoni yangu kujibu hoja za upotoshaji zilizoletwa na msomaji wako. Kwanza kama yeye alivyojitambulisha kwa hoja zake kuwa ni Mwislamu, mimi ni Mkristo. Nitajibu hoja zake moja baada ya nyingine ili aelewe kama atakuwa tayari. 1. Walioendesha biashara ya utumwa walikuwa Waarabu wa kiislamu. Hawa walikuja Afrika mashariki kufanya biashara mbaya kabisa ya utumwa na kueneza dini yao. Watumwa walisombwa kutoka Afrika kwenda Uarabuni mahali panaposadikika kuwa chan...

Nuru anakuuliza: "...Sura yako hasa ni ipi?"

Kuna kitu ambacho huwa ninajiuliza kila mara, hivi mimi sura yangu ni ipi? Huwezi ukakubali kwa haraka hadi utakapojifanyia uchunguzi ndipo utakapogundua hauna sura moja. Unapokuwa unaongea na mpenzi wako unakuwa na sura gani? Unapokuwa unaongea na wazazi wako unakuwa na sura gani? Unapokuwa umefurahi unakuwa na sura gani? Unapokuwa umekasirika unakuwa nasura gani? Unapoongea na bosi wako Je? Unapoandika email au kuchangia maoni je? Haya ni maswali ambayo huwa ninajiuliza mara kwa mara. Je sura yangu ni ipi na nifanye nini ili niijue sura yangu halisi? (c) Nuru Shabani, 2009

Kutoka kwa Da'Subi, unaelewa picha hii ilivyo?

Picha
Ukiiangalia kwa makini picha hii, utaamua mwenyewe ikiwa hawa jamaa wanajenga darini ama sakafuni? HIyo ngazi iliyowekwa ina kazi gani? Huu ni mfano mzuri wa jinsi akili zetu zinavyofanya kazi. Unakifikiri kinatokana na ulichokiingiza ubongoni mwako kabla.

Matokeo ya utafiti wa Mwaipopo

Mwaipopo, mwanablogu wa Sauti ya baragumu ameonyesha mfano wa namna wanablogu tunavyoweza kuyachunguza mambo na kisha kupata michango yenye uzito unaovutia. Mfano huu ni wa kuigwa na kila mpenda mijadala. Nataraji kwamba wasomaji watakumbuka lile swali la lugha nililokuwa nimeliuliza kuonyesha ugumu uliopo katika kulitafsiri kwenda kwenye kiingereza ambacho hakitapoteza maana. Tulipata majibu mengi. Ndipo Mwaipopo kwa msukumo wa kupenda utafiti, akafanya uchunguzi na haya ndiyo majibu yake: " Jamani sikuishia hapo. Nilikuwa nafanya kautafiti kadogo ili nije tena...Swali hili liliponitoa jasho nikaona nimuulize rafiki yangu mzungu. Nae kaiona shida. Bahati njema anajuajua kidogo Kiswahili cha kuendea kariakoo. Kama mjuavyo mimi ni linguist. Niliwahi kusoma translation course. Hili ni tatizo miongoni mwa matatizo ya fasili - maneno ama miundo yenye kuegemea katika utamaduni wa lugha husika. hata hivyo panapo nia ya kutafsiri lazima njia itafutwe. hasa ni kwa nia ya kujif...

Je, kuna Mungu? - Mchango wa Nuru Shabani

Kuna wachangiaji wananiandikia kwa barua pepe. Sijui ni kwa nini wanataka tujadiliane sirini. Nadhani tukijadili waziwazi inapendeza zaidi kwa faida ya wasomaji wengine. Hapa ninao mchango wa Nuru Shabani kupitia kisanduku cha maoni. Kwa kuheshimu mchango wa msomaji huyu, naomba niupandishe hapa uusome. "...Ningependa kuungana na Kamala kuwa hakuna kitu kinachoitwa Mungu,kama wengi tulivyoambiwa. Zamani kabla hawajaja wakoloni(wazungu na waarabu) hakukuwa na kitu kinachoitwa Mungu,wao waliamini ktk Nguvu kuu.Ndiyo maana utakuta wengine waliamini ktk miti wengine katika majabali,na kikubwa ndugu zangu ieleweke wengi wa watu wa zamani waliamini zaidi katika kanuni za kimaumbile ndiyo ilikuwa msingi wao. Kwa mtazamo wangu wengi hatumwelewi mungu sana tunachofanya ni kujenga hofu kwa Mungu,linapokuja suala la kutaka kumjua huyo mungu kwa undani utaambiwa unakufuru,sasa mi huwa ninajiuliza iweje utake kujua asili za aliyetuumba uambiwe unakufuru? Haingii akilini umuulize mzazi w...