Matokeo ya utafiti wa Mwaipopo

Mwaipopo, mwanablogu wa Sauti ya baragumu ameonyesha mfano wa namna wanablogu tunavyoweza kuyachunguza mambo na kisha kupata michango yenye uzito unaovutia. Mfano huu ni wa kuigwa na kila mpenda mijadala.

Nataraji kwamba wasomaji watakumbuka lile swali la lugha nililokuwa nimeliuliza kuonyesha ugumu uliopo katika kulitafsiri kwenda kwenye kiingereza ambacho hakitapoteza maana. Tulipata majibu mengi.

Ndipo Mwaipopo kwa msukumo wa kupenda utafiti, akafanya uchunguzi na haya ndiyo majibu yake:

" Jamani sikuishia hapo. Nilikuwa nafanya kautafiti kadogo ili nije tena...Swali hili liliponitoa jasho nikaona nimuulize rafiki yangu mzungu. Nae kaiona shida. Bahati njema anajuajua kidogo Kiswahili cha kuendea kariakoo.


Kama mjuavyo mimi ni linguist. Niliwahi kusoma translation course. Hili ni tatizo miongoni mwa matatizo ya fasili - maneno ama miundo yenye kuegemea katika utamaduni wa lugha husika. hata hivyo panapo nia ya kutafsiri lazima njia itafutwe. hasa ni kwa nia ya kujifunza kuliko kujifanya kujua.

Nilimuuliza mzungu wangu huyu hivi:

I have a question that seemingly gives many of us a headache. it is about asking for one's ordinal number of your birth. Suppose you are 4 in total from the same mother and you don't know exactly whether you are 1st, 2nd, 3rd or 4th (imagination) and you want to ask say your parents as to what is your ordinal number. In Kiswahili we have a version of it which is: "MAMA, MIMI NI WA MWANAO WA NGAPI KUZALIWA?" We cant get one sentence that is a correct translation of the same. My friends and I end up with funny sentences. Do we have one sentence to ask for that?

Akanijibu:

In answer to your question, I would say there are several ways to ask. "Mom, what child am I?" Or "which child am I?" But those questions wouldn't exactly prompt someone to answer with the order of your birth. Alternatively you could ask "Am I the first born?" In which hopefully unless it was true that you were the first born child, your mother would say, no you're the second or third child, etc.

I can see your problem, as I would translate that question to "Mama, I am of which birth?" or "I am how many born?"

Does that solve any problems or win any bets?

Nami nauliza vipi inasaidia saidia? Maswali haya yanaleta changamoto

Alamsiki binuur"

Haya wasomaji. Mnaonaje matokeo haya? Binafsi nimependa sana namna Mwaipopo alivyoshughulikia utata huu. Kumbe blogu zaweza kuwa chanzo cha maarifa kuliko porojo. Inawezekana.

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3