Kwa wageni: Ujumbe wa Mwenyekiti wetu

Waraka wa mwenyekiti wa Jumuiya ya wanablogu Tanzania (JUMUWATA) kwa wanablogu wote:

"Wapendwa katika jina la Watanzania. Amani iwe juu yenu. Natumai wote muwazima.

Hii ni kuwataarifu rasmi kuwa, baada ya kimya cha muda mrefu sana, mahangaiko ya hapa na pale na mambo mengine, hatimaye ndugu, kijana, mpiganaji, muungwana na mpigikaji mwenzenu nimerejea ulingoni. Najua kuna ambao walikuwa wangali wakinisaka katika www.msangimdogo.blogspot.com na najua kuwa kuna wale ambao watakuwa huenda ni wapya kabisa katika taarifa hizi.la nyote kwa ujumla, napenda kuwataarifu rasmi kwa, maskani yangu kwa sasa ni hapa. Kuna kitabu cha wageni pale, makala zangu zilizotangulia ambazo zilitoka katika sehemu mbalimbali nilizozurura nakadhalika. Ila hatimaye, nimeamua kutulia hapo.

Nawakaribisheni sanjari na kuwaomba mwafikishie ujumbe huu Blogaz wenzenu ambao mnawafahamu, pamoja na kutiwekea taarifa hizi katika blogi zenu kwa wale watakaoweza. Mwisho kabisa, naomba wale ambao viungo vyao (link za blogi zao), haziko katika blogi yangu, wanitumie kwa mail ili niweze kuviweka pale, maana nataka kila mtu niwe na anwani ya kuingia kwenye maskani yake kwa urahisi. na kwa wale ambao wana nembo, pia wanaweza kunitumia ili zikae pale kama zilivyo za dada katabazi, Bongo Celebs nk.

Amani iwe juu yenu

Msangi, Ramadhani S.

Maoni

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3