Kwa nini watu huongopa?

Kusema uongo ni kutokusema ukweli. Kupindisha uhalisia wa mambo, basi. Kwa namna moja ama nyingine, sisi kama binadamu tumewahi kuongopa. Tumewahi kuwaongopea marafiki. Wazazi. Waalimu wetu. Wakubwa zetu. Na watu wengine wanaotuzunguka. Na pengine tumewahi hata kujiongopea nafsi zatu wenyewe kwa namna moja ama nyingine.

Na uongo huwa na sababu bila shaka. Haiwezekani kusema uongo bila sababu. Kwa sababu kwa hakika kila mtu hupenda kusema ukweli. Sasa ni kwa nini watu hudanganya hapo ndiko lilipo swali langu.

Katika kulijibu swali hili, msomaji anaweza kurudi nyuma kadiri awezavyo, kukumbuka matukio yote ya uongo aliyowahi kukumbana nayo, halafu achunguze, ni kwa sababu gani alisema uongo? Alipenda kudanganya ama alilazimika? Kipi hasa kilisababisha aseme aindishe ukweli wa mambo? Je, uongo huo ulimpa faida ya nafsi ama hasara?

Lakini pia kuna jambo la kukumbuka. Wapo watu ni waongo wazuri kiasi kwamba hawawezi tena kujua kuwa wao ni waongo (unakuwa mwongo mpaka unauona uongo kama ukweli!) Je, kwa nini watu wengine hudanganya zaidi kuliko wengine?

Jielewe.

Maoni

 1. Kuna msemo mmoja kule kwetu wanasema, uongo ukisemwa sana bila kukanushwa, basi hufudhu na kuwa ukweli.
  Hilo ni kweli.
  lakini kaka Bwaya uongo unakubalika kama ukitumika kwa nia nzuri.
  Ngoja niache na wengine wachangie, halafu nitarudi kufafanua baadae kwa nini uongo wakti mwingine inabidi ukubalike.

  JibuFuta
 2. Niliandika siku chache zilizopita. Niliandika, ukweli, una tatizo gani?
  Nashukuru maoni niliyoyapata yamenipa uwezo wa kuchangia leo.
  Watu wengi tunapenda kutumia uongo, tena kwa gharama yoyote.
  Mi nadhani uongo huweza kulipamba jambo hata likamvuta mtu kusadiki.
  Hebu fikiria huu mfano, mke wa mtu amekutana na mshikaji wake wa nje pale Buguruni baada ya kutoka kazini pale Ilala. Anachelewa kurudi nyumbani pale Tabata. Mumewe anawaka kwanini amechelewa kurudi. Kwa sauti laini anajibu kulikuwa na foleni kubwa Mandela Road sababu ya ukarabati wa barabara unaoendelea.
  Jamaa anajikuta akiusadiki huo uongo. Bibie baada ya kushinda leo, anauhalalisha uongo huo, kila siku atashinda.
  Ulikuwa mfano tafadhali.
  Najaribu kusema nini? Sijui. Labda nataka kusema nimejifunza katika maisha kuwa uongo ni kanuni ya watu wasiojiamini.
  Watu wasiojiamini huwa na mashaka na matendo yao. Ili wasinyoshewe vidole huuhalalisha uongo ili uwe nyenzo yao.
  Pengine tuseme, kuna tatizo. Kama wengine wanavyosadiki, watu wanautumia uongo wakidhani wanazilinda personality zao. Mwisho wa siku...wahenga walinena, "lila na fila havitangamani"
  Ni hayo tu!

  JibuFuta
 3. OOOOPSSS!!!!!KAAAAZI KWELI KWELI,
  HAYA WADAU WENGINE MWASEMAJE?
  MIMI BADO NATAFAKARI MAONI YA MTANGA.

  JibuFuta
 4. uongo ni kama kaujinga fulani. sisi kama binadamu ndio ukweli na ukweli umo ndani mwetu.

  sema uongo mara mia lakini ipo siku utakamatwa tu. wakati unaongopa huwa unajiona mjanja lakini wakati wa kukamatwa unatoa jicho kama bibi harusi aliyebanwa na ushuzi huku akilazimika kutabasamu.

  si unaona mafisadi wote? enzi zile walifurahi kudanganya umma. sasa wakati umefika wa ukweli kuchukua mkondo wake ili walipe gharama za uongo wao. sio mafisadi tu hata wewe ukijikagua utagundua jinsi uongo ulivyokugharimu baada ya ukweli kushika nafasi yake tukufu

  JibuFuta
 5. HIVI KAMALA, WEWE SIO MUONGO KWELI!!!?????

  JibuFuta
 6. Uongo ni kanuni ya wasiojiamini.Watu wasiojiamini huwa na mashaka na matendo yao, na hivyo kuutumia uongo kuzilinda personality zao. Nakubaliana na wazo hili. Athari za uongo kama zilivyoainishwa na Kamala, ninakubaliana nazo.

  Hebu na tusome mawazo ya Kaluse kama alivyotuahidi: Kwa nini mara nyingine uongo inabidi utumike?

  * Zingatio: Katika mazingira hayo ya kusema uongo kwa nia nzuri, itapendeza ukituonyesha kinagaubaga kwanini usitumike ukweli.

  JibuFuta
 7. Uongo ni matumizi ya nguvu za kibinadamu za kubuni wengine wanatakanini. Ukikosea kudanganya, unaitwa muongo.Ukipatia novo yako itaitwa hadithi nzuri kwa ubunifu wako wa nini ni stori nzuri kwa akusomaye.

  Upngo ni ugonjwa pia kama imaginations zinatawala halihalisi.

  JibuFuta
 8. Kubuni wengine wanataka nini. Sawa. Kwa nini tunapojua wengine wanataka nini, tusiseme ukweli kutimiza matarajio yao, isipokuwa kwa matumizi ya uongo? Why should we lie?

  JibuFuta
 9. Nimependa mjadala huu bwana Bwaya. Nitachangia siku nyingine ila kwa sasa nikupongeze kwa kazi nzuri nimeipitia blogu yako naona itanileta hapa mara kwa mara. Unasoma falsafa au saikoloji?

  JibuFuta
 10. Nimepita kukusalimi tu. na pia kusema asante kwa kunitembelea

  JibuFuta
 11. uwongo mbona mtamu sana ,kwani unampomhadaa mshikaji au mpenzio kwamba simu haina chaji au kuna wageni usije leo nyumbani au geto? alaaaa kumbe uongo ni sanaa kama siasa za bongo useme kwenu unabenzi wakati jumba la udongo? hhhhaaa kuna mama mmoja upanga yaani kila siku ni uwongo kwa mume wake lakini ukimtazama unashangaa mwenyewe anajisfu kwamba anadanganya kusidi. KUMBE UWONGO UNAFAIDA zake waulize waliopo juu na chini kama sauti zao zinafika kwa pamoja. Uwongo ni nini? basi kaka Simon umeua bendi kabisa

  JibuFuta
 12. kuna mwanafalsafa aliyewah kusema kwamba ukweli huanza kwa kudharauliwa na kuchekwa, baadaye ukataliwa lakini muda wake ukifika, kila mtu huupokea kwa msahangao. daima ukweli haukwepeki.

  kaluse mimi nadhani kuna wakati ambao huwa nadanganya.labada swali liwe kwa jinsia mbili kwamba kati ya wanawake na wanaume ni nani hudanganya zaidi.

  bwaya kuna nyakati za kusema uongo au kuzunguka ukweli na kuuacha bila kuutaja ili wenyewe wajue. kwa mfano kuna tajiri anayedai anatishiwa maisha yake, ukienda kumwambia kwamba hata yeye akifa wengine wataendelea kuishi, atachukia na kufanya vibaya labda. ni bora uzunguke ukweli huo wa kwamba hatoishi milele na yawezekana afe kupitia hivyo vitisho. ni ukweli mgumu kutamka.

  naogopa asisome hapa, akatafuta ninaposihi, hii ni hatari ya kusema ukweli pia bila kuuzunguka au kudanganya kwambayeye ni mtu muhimu na hastahiri kufa au tumsalimie salamu ya watu fulani ya uishi milele tajiri wetu naye ajibu, nitaishi

  JibuFuta
 13. Ukijifunza kusema ukweli, basi unajipunguzia kazi ya kulazimika kukumbuka ulichowahi kusema kabla. Tufanyeje ili tuweze kuona fahari kuutumia?

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Fumbo mfumbie mwerevu

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Pay $900? I quit blogging