Elimu tu inatosha kupambana na UKIMWI?

Kuna jambo la msingi la kutazama taratibu kuhusu kampeni kabambe za kupambana na UKIMWI.

Kampeni hizi zinalenga kuelimisha watu kuhusu namna ya kupambana na janga hili ambalo nina hakika linamtisha kila adhaniwaye kuwa na akili timamu. Na kwa kiasi fulani elimu hii imesambaa. Watu wanayo elimu hii. Kuhusu elimu tumefanikiwa. Makofi tafadhali. We tazama barabara. Kuta. Miti. Redio. Luninga. Kila eneo mabango ya kuelimisha kupitia ujumbe wa aina tofauti tofauti.

Ajabu yenyewe ni kwamba kasi ya kuenea kwa UKIMWI inazidi kasi ya kusambaza ujumbe. Na inasikitisha kwamba hata hao wanaoitwa waelimishaji, nao wanashindwa kuitumia vyema elimu hiyo kijikinga na UKIMWI. Narudia. Waelimishaji wenyewe, hawajaweza kuitumia elimu hiyo nzuri wanayoigawa kwa wanajamii. UKIMWI unawaanza wenyewe.

Kwamba watu wanaojua kusoma wanapita kwenye barabara zenye mabango yenye kuonya kuhusu tabia ya ngono na kuhimiza matumizi ya kondomu, wanapanga mikakati kwenye baa yenye mango hayo hayo, wanaingia kutenda uasherati kwenye chumba chenye mabango yale yale. Hali hii unaweza kuielezeaje?

Hivi elimu tu ya kujikinga na UKIMWI inatosha kutunusuru?

Maoni

 1. watu tunatakiwa kubadilika kuwa waminifu katika ndoa zetu hapo kidogo sana tutavuta siku za kuishi

  JibuFuta
 2. watu tunatakiwa kubadilika kuwa waminifu katika ndoa zetu hapo kidogo sana tutavuta siku za kuishi

  JibuFuta
 3. hakuna mapambano ya ukimwi bali dili kwa wajanja na kuwapoteza watu kifikra ili wafikirie ngono tu na Ukimwi.
  sasa wameleta na dawa za kuongeza siku, sijui kama wanauhakika mtu alipaswa kuishi siku ngapi na wanaongeza mpaka lini.

  kuna ka-ujinga kanakoendelea pale vijana wa bongo wanapofundishwa jinsi ya kujikinga na ukimwi katika ngono wakati hakuna mtu hata mmoja aliyewahi kuwafundisha vijana hao ngono. sijui wanauhakika gani kama vijana wanaofundishwa ngono salama wanaufahamu wa kutosha juu ya ngono na taratibu zake.

  mabango mengi niyaonayo barabarani yanahamsha hisia zaidi za kufanya ngono.

  dini zetu zinazuia watu kutumia kondomu. sijui sana kama dini hizi zinajua zinalolitenda. viongozi wa dini nao wanaambukizwa kama kawa, lakini pia dini zinawaambia wafuasi wake kuwa wakitumia kondo watakuwa wameua, uchizi huu? eti ukimwaga shahawa kwenye kondom utakuwa umeua wakati sio kila bao linatungisha mimba.

  kisayansi inaonyesha kwamba kila bao atoalo mwana mume, lina mbegu zaidi ya milion 600 zinazoweza kutungisha mimba na kati ya hizo ni kamoja tu kanakoweza kuchomoza na kupachika mimba, je zilizobaki zinaenda wapi kama sio kufa? yaani kuzuia kambegu kamoja kasiingie kwa kondom, na kuruhusu kamoja kaingie bila kondom kati ya mamilioni, kuna tofauti gani?
  imani bwana, haihitaji kufikiri kwa makini.

  lakini sisi kama taifa tutauogopa ukimwi mpaka lini? ni bora tuishi vizuri kama taifa kwa kutimiza malengo yetu tukijua kabisa kwamba ipo siku tutakufaa, kwa ukimwi na bila ukimwi.

  Ukiangali TV zinazotumika kutangaza juu ya ukimwi, asilimia kubwa ya maonyesho yake yana uhusiano na ngono, je tunapambana na nini hapa?

  nimechoka kutaipu, bye

  JibuFuta
 4. Dah! umenena sawa.Na hii wanayotuhamasiaha kupima ngoma inasaidia kupunguza maambukizo?

  JibuFuta
 5. Ni kweli uaminifu katika ndoa ni jambo muhimu sana.

  JibuFuta
 6. @Fita na Yasinta, mnachokizungumza ndicho ninachokiuliza. Tunakubaliana kuwa uaminifu unaweza kusaidia kupambana na tatizo hili. Lakini je kuelewa ukweli huo pekeyake inatosha? Wangapi pamoja na kwamba wanaelewa kuwa uaminifu ni muhimu bado hawezi kuwa waaminifu? Je, twaweza kuwa waaminifu kwa kupata elimu tu pekeyake?

  @Kamala, inawezekana kuwa hatufanyi kampeni za kuwasaidia wapenda ngono (kupunguza idadi yao) na badala yake, tunafanya kampeni za kutengenza wapenda ngono. Hili ni jambo la kutazama kwa makini. Asante kwa changamoto kuhusu kondomu. Lakini nikuulize, hivi kusisitiza matumizi ya kondomu kunasaidia kuondoa tatizo? Naona kama ni aina ya kukimbia tatizo kwa kuhangaika na matawi wakati mzizi wa tatizo unabaki pale pale!

  @ Edigio: Kuna rafiki yangu moja wa pale Muhimbili yeye anaamini kuwa kupima hakumsaidii mtu zaidi ya kumwathiri zaidi. Kwamba kujua tu unavyo virusi vya UKIMWI hakukusaidii kama ambavyo kutokujua kwamba unavyo kunavyokusaidia. Kwa mujibu wa huyu bwana kampeni za kupima UKIMWI zina malengo ya takwimu zaidi kuliko kuwasaidia wanaogundulika kuwa na UKIMWI. Lakini bado tunaweza kuhoji fikra za namna hii, mbona wanapewa ARVs? Usipojua kuwa unao utapata wapi muda wa kutafuta dawa za kusukuma maisha?

  JibuFuta
 7. tutawapunguzaje wapenda ngono wakati ngono ni kitu muhimu sana katika maisha ya watu? sisi wote tupo hapa hii leo kwa sababu watu wawilikwa nyakati fulani walitapeni, wakafikiri, wakapenda na wakatenda ngono. unapoongelea kupunguza wapenda ngono waweza kuwa unaongelea kupunguza uzaliano!

  ngono ni muhimu ili viumbe viwepo. sidhani kama kuna asiyefanya ngono katika mtandao huu.

  swala ni jinsi ya kuwa na wapenda ngono au wafanya ngono bila kuambukizwa na virusi hatari vya ukimwi.

  vinginevyo tuachane na propaganda za kujifanya tunachukia ngono wakati sisi wenyewe ndo tunafanya ngono kuliko tuwatuhumuo.

  inakuwaje mapadri wanaambukizwa virusi, wanafumaniwa, kulawiti nk wakati wao wanazuia watu kufanya ngono na inajulikana kwamba wao hawafanyi?

  tunahitaji kufikiri kwa bidii

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Pay $900? I quit blogging

Fumbo mfumbie mwerevu