Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Misingi ya Tabia

Ukiigiza Ukatili, Unakaribisha Tabia ya Ukatili

Picha
Kuna wakati unaweza kufikiri unaigiza msimamo na kejeli kwa maumivu ya mtu, unakuwa na maoni yasiyo na haya kwa mateso ya wenzako ukijua unawafurahisha watu fulani lakini hayo maigizo ya kukosa huruma kwa mwenzako yana uwezekano wa kugeuka tabia kweli na ukawa mtu katili kweli kweli. Michezo, dini na siasa visikuchochee kujiona una haki ya kubeza masaibu wanayopitia wenzako kwa sababu mdogo mdogo mizaha hugeuka ukweli.   Mwaka 1971, Philip Zimbardo, mshunuzi na mwalimu wa Chuo Kikuu cha Stanford, alifanya utafiti maarufu kama  #StanfordPrisonExperiment  akilenga kuchunguza nguvu ya mazingira kwenye tabia.    Utafiti ulivyofanyika   Zimbardo alitengeneza gereza la kuigiza hapo chuoni likiwa na seli, mahali mfungwa angekaa mwenyewe, mahali pa wanyarapa kuishi, mahali wafungwa wangetoka na kuteswa na wanyapara. Washiriki walifanyiwa mchujo wa haiba kuona kama ni watu wenye utimamu wa tabia na hisia.    Kwa njia ya nasibu (random assignment) wanafunzi...

Jifunze Uhusiano wa Malezi na Vilema vya Haiba (Personality Disorders)

Picha
Kizazi chetu kinakabiliwa na magonjwa mengi yasiyoonekana. Tunaumwa, na wakati mwingine taabani, lakini hatujui kuwa tunaumwa. Tunatembea, tunakutana na watu, tunapiga picha zenye nyuso zilizochangamka, tunaonekana kufurahia maisha lakini tunateseka na mahangaiko mengi tusiyoweza kuyasema.   Tazama kiwango chetu cha ukatili. Haiwezi kuwa kawaida, kwa mfano, kuona mwenzako anaumizwa na wala hujali. Unamuumiza mtu na bado unashangaa kwa nini analalamika. Unamtesa mwenzako kihisia na bado unamdhihaki anapougulia maumivu. Unajiuliza, tumefikaje mahali mwanadamu unaweza kumtesa mwenzako, ukamsababishia maumivu na hujisikii kujutia.    Mbaya, wakati mwingine, kiwango hiki cha ukatili kinakuwa kama nyenzo ya kupata tunachokitaka. Tunataka madaraka, tunataka umaarufu, mali na kila kinachotufanya kujione tunnawazidi wengine. Tunakuwa waraibu wa ukatili dhidi ya binadamu wenzetu na hatujisikii kujutia. Tazama kiwango chetu cha ubinafsi. Kwa nini tumepoteza uwezo wa kuafikiria hisia...

Hulka ya Mwanadamu Kujikweza na Kukwepa Wajibu

Picha
Umewahi kujiuliza kwa nini mtu akifanikiwa jambo (biashara, kazi, elimu, siasa nk) anataka aonekane ana bidii, ana uwezo na kitu cha tofauti kinachomtofautisha na wengine? Kwa nini, kwa mfano, ikitokea kinyume, mtu akashindwa, akafanya vibaya, hutaka ionekane kuna watu wanamkwamisha, kuna upinzani, kuna wabaya wake na inakuwa nadra kukubali huenda tabia zake mwenyewe zinamgharimu? Mwaka 1978, washunuzi Berglas na Jones waliwatumia wanafunzi wa chuo kuichunguza dhana hii. Makundi mawili ya wanafunzi yalipewa 'puzzle'— fumbo linalohitaji akili kulifumbua. Kundi A walipewa fumbo rahisi. Halikuhitaji kufikiri sana. Kundi B wakapewa fumbo gumu (lisilowezekana hata ukeshe nalo). Makundi yote yalipewa maelekezo kuwa wakihitaji kuboresha uelewa ili wafumbue fumbo wanaweza kuomba kidonge kinachoitwa Actavil lakini wakiona wanahitaji kidonge cha Pandocrin kinachopunguza uelewa pia wangeweza kuomba. Wakati zoezi kiliendelea, 80% ya washiriki wa kundi A (wenye fumbo rahisi) waliomba kido...

Malengo Yanavyoweza Kubadili Tabia ya Mtoto

Picha
Mwanangu wa miaka saba alikuwa na tatizo la kupenda sana kununua vitu vitamu. Kila siku alikuwa ombaomba wa chochote kinachomtosha kwenda dukani. Sikupenda tabia hii. Mbali na kuharibu meno yake, kulikuwa na tatizo la kutokujizuia. Ilifika mahali tunagombana kwa sababu tu hajapata chochote kukidhi hamu yake ya kununua ‘ice cream’, ‘chocolate’ na vinavyofanana na hivyo. Jitihada za kubadili tabia hii ya kupenda vitu visivyo na faida kwake hazikuzaa matunda.

Tunatofautiana sana...

Picha
PICHA: Verastic Mwanamke, kwa asili yake, anajisikia vizuri kusema matatizo yake kwa mtu wake wa karibu anayemwamini –kama, mathalani, mume wake. Ile tu kujua kuna mwanaume yuko tayari kusikia yanayousibu moyo wake kunamfanya ajisikie salama.

Mambo Sita Mwanao Anayohitaji Kuyasikia

Picha
PICHA: houstonpress.com Watoto wadogo ni watu kamili wenye hisia kama sisi watu wazima. Hata kama wakati mwingine hawawezi kusema wazi wazi, ukweli ni kwamba akili zao ni kama dodoki linalonyonya kimya kimya yale wanayoona tukiyasema na kuyatenda. Unaweza, kwa mfano, kusema jambo dogo kwa mtoto tena bila kumaanisha lakini jambo hilo likawa sumu itakayoharibu kabisa maisha ya mwanao. Unaweza kuwa na nia njema ya kumlazimisha kufanya kitu fulani sahihi kabisa, lakini kwa sababu hujaweza kuelewa na kujali hisia zake, jambo hilo likakosa nafasi kwenye moyo wa mtoto. 

Hisia Zilizojeruhiwa Zinavyoweza Kujenga Ukatili Usiotarajiwa

Picha
PICHA: Pride News Magazine Baraka amekuwa akilalamikiwa kwa tabia yake ya udokozi tangu akiwa darasa la tatu. Ingawa alikuwa mdogo kwa umbo, jina lake maarufu lilikuwa ‘Baraka kibaka.’ Mbali ya kuwa kibaka, baraka alikuwa mgomvi aliyepambana na karibu kila mwanafunzi shuleni.

Mazingira Yanayoweza Kuanzisha Mapenzi Yasiyotarajiwa Kazini

Picha
Dorcas, msichana wa miaka 30 anayefanya kazi kama Afisa Mikopo kwenye benki moja mjini, hakuwahi kufikiri ingetokea siku moja ‘achepuke’ kimapenzi na Johnson ambaye ni mfanyakazi mwenzake. Miaka mitatu iliyopita wakati anaanza kazi kwenye benki hiyo, Dorcas alikuwa na msimamo thabiti na aliheshimu ndoa yake.