Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Maamuzi

ChatGPT Inapoaminika Kuliko Mzazi

Picha
Jioni moja wiki iliyopita nilikuwa Instabul. Huu ni mgahawa mmoja maarufu jijini Dar es salaam. Hapa nafanya nazungumza na Damari, mwanafunzi wa shahada katika taasisi moja ya elimu ya juu jijini Dar es salaam. Sikumwuuliza umri lakini nakadiria ana miaka 21. Kikao chetu kimezaliwa na kipindi nilichokuwa nimekifanya asubuhi hiyo kwenye kituo kimoja cha televisheni.   Tulizungumza kwa kirefu suala alilokuwa nalo na tufikia muafaka. Kisha nilimwuuliza swali ambalo huwa nawauliza ‘wadogo’ zake ninapokuwa naendesha mafunzo ya malezi shuleni.  "Nani ni rafiki yako wa karibu?" Nalenga kujua anamwamini nani.  Hakufikiri mara mbili akanijibu, "ChatGPT!” Sikuzuia mshangao. Jambo hili, kwa hakika, lilinisumbua. Sikuwahi kufikiri ChatGPT ingewahi kuwa rafiki wa mtu. Kama huifahamu, ChatGPT ni programu tumizi inayotumia teknolojia ya akili mnemba. Imentegenezwa kuwezesha mazungumzo yanayolingana na unachoulizia.    “Umesema ChatGPT ndio rafiki yako?” “Ndio. Rafiki ninayemwa...

Madhara ya Kutoa Ushauri Kienyeji na Kuugeuza Unasihi kuwa Ushauri

Picha
Utamaduni wa (kutoa na kuomba) ushauri umejengeka kwenye misingi ya hekima ya wazee walioona mengi, uzoefu wa mtu mzima unaompa uhalali wa kutoa mwongozo wa kufuata kwa anayemzidi.  Hata tunaposikia unasihi (counselling), aghalabu, mawazo yetu yanaenda kwenye taaluma ya kushauri watu na kuwaambia cha kufanya ili kutatua matatizo yanayowakabili. Wapo, tena wengi, wanaotafsiri ‘counselling’ kama ushauri. Counselling sio ushauri. Katika makala haya, ninajenga hoja kuwa kutoa ushauri ni jambo la hatari na kwamba linaweza kusababisha madhara makubwa kwa anayeshauriwa lakini pia hata anayeshauri.  Kadhalika, ninalenga kuonesha, japo kwa ufupi kuwa hata kwenye unasihi msingi wa kwanza wa kuzingatia kwa mtoa huduma (aliyefuzu) ni kuepuka kabisa kutoa ushauri kwa mtu. Nakusudia kuonesha nini hasa huwa ni malengo ya unasihi. stefanamer/Getty Images Ushauri ni nini?  Unaposema unamshauri mtu unakuwa na maana gani?  Ushauri, kwa kifupi, ni maelekezo mahususi unayompa mtu, maamuz...

Changamoto za kuwanyima watoto kufurahia utoto wao

Picha
  Tunaishi kwenye dunia inayopitia mabadiliko mengi. Mabadiliko haya ya kijamii na kiuchumi, kwa kiasi kikubwa, yamezidisha matarajio tuliyonayo kwa maisha. Ukiacha matarajio mengi tuliyonayo kwetu binafsi, kuna matarajio mengi hata kwa wenzi wetu. Mke, kwa mfano, anatarajia mume awe kila kitu anachokifahamu kuhusu mwanamume. Mume ana kazi ya kuwa mcha Mungu, mtu wa sala, mtafutaji na mchapa kazi hodari, mcheshi, rafiki msikivu, kiongozi bora,     baba mzuri na mume mzuri asiyechelewa kurudi nyumbani. Matarajio haya makubwa yana faida zake lakini pia yana upande wa pili unaochanga migogoro mingi katika familia.   PICHA:  Wikimedia Commons   Hatuishii kuwa na matarajio makubwa kwa wenza wetu. Tunazidisha pia matarajio kwa watoto wetu kiasi cha kuwanyima fursa ya kufurahia utoto wao. Hebu fikiria mtoto asiyeruhusiwa kufanya makosa. Kila analojaribu kufanya, anapodadisi mazingira yake,  anakuwa anatafsirika kama mtoto asiye na nidhamu na adabu kwa wa...

Uamuzi wa Kuachana na Blogu

Picha
Mkutano wa Global Voices, mtandao wa wanablogu, uliofanyika Cebu, Ufilipino, 2015 PICHA: Global Voices Nilianza kublogu katikati ya mwaka 2005. Wakati huo ilikuwa nadra kusikia mtu anaongelea blogu.  Ndesanjo Macha ndiye hasa aliyenifanya nikavutiwa kuanza kublogu. Wakati huo alikuwa mwandishi wa safu ya Gumzo la Wiki iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi kila Jumapili. Historia ya blogu hapa nchini haikamiliki bila kumtaja Ndesanjo Macha. Kimsingi, Ndesanjo ndiye mwanablogu wa kwanza kublogu kwa Kiswahili. Huo ulikuwa mwaka 2004. Nilipata bahati ya kukutana naye mara mbili kwenye mikutano ya waandishi wa kiraia kupitia mtandao wa wanablogu uitwao Global Voices. Mara ya kwanza ilikuwa jijini Nairobi, 2012 . Mara ya pili ikatokea jijini Cebu,Ufilipino, 2015 . Nakumbuka mwaka 2010 nikiwa nahudhuria mkutano wa wanablogu uliofanyika  Santiago de Chile , nilistushwa na masimulizi ya baadhi ya washiriki waliokuwa wakiongelea 'kuminywa kwa uhuru wa kujieleza kwenye...

Tumetengwa na Watu ili Tuunganishwe na Teknolojia?

Picha
PICHA:  The Brown Daily Herald Ukisoma gazeti au kitabu, kuna mahali utakutana na ishara kuwa umefika mwisho hivyo utaliweka gazeti au kitabu chini, na kuendelea na mambo mengine. Vivyo hivyo unapoangalia filamu, unapofuatilia kipindi au taarifa ya habari kwenye radio au televisheni. Kuna mahali utafika utakutana na ishara kuwa sasa umefikia mwisho. Kipindi kimeisha, taarifa unayofuatilia imeisha, basi unapata nafasi ya kufanya maamuzi ya ama usibiri kingine au uendelee na mambo mengine.