Uamuzi wa Kuachana na Blogu


Mkutano wa Global Voices, mtandao wa wanablogu, uliofanyika Cebu, Ufilipino, 2015 PICHA: Global Voices


Nilianza kublogu katikati ya mwaka 2005. Wakati huo ilikuwa nadra kusikia mtu anaongelea blogu.  Ndesanjo Macha ndiye hasa aliyenifanya nikavutiwa kuanza kublogu. Wakati huo alikuwa mwandishi wa safu ya Gumzo la Wiki iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi kila Jumapili.

Historia ya blogu hapa nchini haikamiliki bila kumtaja Ndesanjo Macha. Kimsingi, Ndesanjo ndiye mwanablogu wa kwanza kublogu kwa Kiswahili. Huo ulikuwa mwaka 2004. Nilipata bahati ya kukutana naye mara mbili kwenye mikutano ya waandishi wa kiraia kupitia mtandao wa wanablogu uitwao Global Voices. Mara ya kwanza ilikuwa jijini Nairobi, 2012. Mara ya pili ikatokea jijini Cebu,Ufilipino, 2015.

Nakumbuka mwaka 2010 nikiwa nahudhuria mkutano wa wanablogu uliofanyika Santiago de Chile, nilistushwa na masimulizi ya baadhi ya washiriki waliokuwa wakiongelea 'kuminywa kwa uhuru wa kujieleza kwenye nchi zao.' Habari hizo za blogu kuleta 'usumbufu' katika baadhi ya nchi hazikuniingia akilini. Nilishangaa inawezekanaje ‘vijiblogu’ viwe tishio kiasi kile hasa kwa sababu hapa kwetu nilizichukulia blogu kama jukwaa la kuelimishana. Nayakumbuka majina ya Jeff Msangi, Evarist ChahaliProf. Joseph Mbele, Prof.Masangu Matondo, Boniface Makene, John Mwaipopo, Fadhy Mtanga  na wengine ambao kila ukipitia blogu zao, ilikuwa ni sawa na kushinda Maktaba ukifyonza maarifa.

Kwangu mimi, nilianza kublogu kama burudani. Nilipenda kujieleza kupitia maandishi kwa hivyo blogu ikawa jukwaa muafaka la kuandika yale niliyokutana nayo kwenye pilika zangu za kila siku, niliyoyasoma kwenye vitabu na hata mambo niliyokuwa nikijifunza darasani. Kwa hiyo niliichukulia blogu kama uwanja wa kujieleza bila kuingiliwa na mtu. 

Miaka michache baadae, mwaka 2009, blogu ikanikutanisha na Global Voices. Hapo mambo yakaanza kubadilika. Nikakutana na watu mbalimbali duniani kupitia kijiblogu changu ambacho, hata hivyo, hakijawahi kuniingizia hata senti.

Kwa muda wote wa zaidi ya muongo mmoja wa blogu nimejifunza kuwa blogu ni shule isiyolipiwa chochote. Blogu ni darasa la bure. Unapokuwa mwanablogu, huwi mwalimu pekee bali mwanafunzi wa wasomaji wako.  Kila nikipitia makala zilizowahi kuandika tangu nikiwa kinda, mwaka 2005, ninakuwa mithili ya mtu anayejitazama anavyokua hatua kwa hatua. Uelewa wangu, mtazamo wangu, mawazo yangu, namna yangu ya kuwasilisha kile ninachojifunza imeendelea kubadilika kadri ninavyojadiliana na watu mbalimbali kupitia blogu. 

Hata hivyo, shughuli ya kublogu si nyepesi. Hata kidogo. Inahitaji moyo na uvumilivu.  Wengi tulioanza kublogu nao katikati ya miaka ya 2000, waliachana nazo muda mfupi baadae. Nawaelewa. Hata mimi kuna nyakati ninashindwa kuandika. Lakini siku zote faraja ninayoipata ni kuona ninachangia maudhui mtandaoni. Nafarijika kwa sababu ninahudumia kundi kubwa la wananchi wanaotumia mtandao kujifunza. 

Kwa kutambua kuwa wananchi hawa wengi wao hawajui Kiingereza kinachotumiwa zaidi mtandaoni, nilichagua kublogu kwa Kiswahili wanachokielewa. Nimekuwa nikiichukulia blogu yangu kama huduma kwa wananchi. Hilo limekuwa muhimu zaidi kwangu kuliko kuifanya blogu kuwa ‘kiamba’ cha kuniingizia fedha.


Nikiwa na Mwanablogu wa Naijeria, Nwachukwu Egbunike, tulipokutana Cebu, Ufilipino 2015. 


Kazi hii, isiyoniingizia hata shilingi mia, imenikutanisha na maelfu ya wasomaji. Hawa ni watu wenye kutafuta maarifa mtandaoni kwa sababu wanaweza angalau kumudu kujiunga na 'kifurushi' kupitia simu zao za kiganjani. 

Inawezekana hawawezi kununua magazeti kama mimi. Hawawezi kununua vitabu kama mimi. Pengine wanapotazama televisheni na radio wanakutana na mazungumzo yasiyokidhi mahitaji yao. Hawa, kwa kweli, wanahitaji watu wanaojitolea muda na raslimali zao kuweka maudhui mtandaoni. Mamlaka zinapaswa kuliona hili.


Miaka zaidi ya 10 niliyoblogu, karibu kila siku, ninasoma ujumbe wa watu nisiowafahamu. Wengine wanahitaji ushauri kuhusu yale ninayoyaandika. Hawa wote wanajikuta kwenye blogu yangu kupitia aina ya maudhui wanayoyatafuta mtandaoni. Kama mwalimu, hili linanipa faraja sana kuwa kazi yangu ya blogu inafikia watu wengi. 

Nikifikiri hayo yote, nashindwa kuelewa mantiki ya serikali kutaka nianze kulipa kodi kwa sababu tu niliamua kuchangia maudhui yanayowasaidia vijana kujifunza mambo yanayowahusu. Sielewi kwa nini nitozwe milioni mbili kwa sababu tu niliamua kutumia muda wangu na raslimali zangu kuelimisha jamii bure. 

Kama suala ni kukusanya kodi, pengine ingeleta maana kuwalenga wale waliozigeuza blogu kuwa vyanzo vya mapato. Lakini kuweka sharti la kila mwanablogu –bila kujali anaitumiaje blogu yake –kulipa kodi, ni suala linalofikirisha. Tena sana. Kuna sentensi nyingi nimeziandika na kuzifuta hapa lakini itoshe tu kusema, ujumbe umetufikia. Tumewaelewa. Kwa hiyo ninaacha kublogu kupinga uamuzi huu. 

Maoni

 1. Ninablogu pia ambayo kimsingi sikuianzisha kwa kutengeneza pesa, nilianzisha kama sehemu ya mchango wa kuwa na maudhui ya mtandao nchini. Vitu ninavyoandika ni maisha ya kila siku na vitu nivyojifunza kupitia kusoma na kukutana na watu. Serikali kuniambia nitoe 2M kwa kitu ambacho haniingizii pesa bado sijaelewa dhumuni lake.

  Hongera kwa kazi nzuri, inasikitisha kwamba kubanwa kwa uhuru wa kujieza kunafanya vijana waliokuwa wanajifunza kutoka kwako kukosa mwalimu.

  JibuFuta
 2. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

  JibuFuta
 3. Pole sana kaka. Mimi pia ni blogger (lakini bado mchanga sana, nilianza 2016) na kiukweli nimekatishwa tamaa sana na uamuzi wa serikali kututoza kodi, nimekata tamaa kabisa. Nilianza kibadilisha "passion" yangu ya ku-blog kuwa ajira yangu lakini kwa hali hii siwezi kufanya chochote, nashindwa hata kufuata "posting schedule" yangu! Inauma sana.... (https://www.mogriculture.com)

  JibuFuta
 4. Cari BANDAR JUDI TERBAIK yang aman dan terpercaya ?
  Solusinya hanya di sahabatpoker
  Bonus Refferal 15%
  Bonus Turn Over 0,5%
  Hanya dengan minimal deposit 20ribu sudah bisa bermain 8 game sekaligus lohh..
  "NEW AGEN BANDAR 66"
  Ayo daftar dan gabung sekarang juga,,
  WHATSAPP : +855967136164
  PIN BB : 2B13CFDA
  PIN BB : E34BB179
  LINE ID : @fjq9439d
  LINE ID : sweetycandys

  http://sahabatpk99.com
  http://sahabatpk99.net
  http://sahabatpk99.info
  http://sahabatpk99.org

  JibuFuta
 5. Welcome to our SAHABATQQ
  Hanya di SAHABATQQ anda bisa lebih mudah menang

  POKER*DOMINO99 JUDI ONLINE TERBAIK MEJASAHABAT,NET

  Minimal deposit 20.000,- sudah bisa bermain disemua jenis game
  Untuk pendaftaran silahkan klik kolom daftar atau link di bawah ini boss
  http://mejasahabat,net/Register,aspx?lang=id

  * Promo Bonus ROLLINGAN 0.3% ( 5 hari sekali )
  * Nikmati Bonus Refferal 15 % ( Setiap putaran kemenangan refferal )
  * Bonus Ekstra Refferal 5 % ( 1 bulan sekali )

  Contact Us :
  * Pin BBM Android CS 1: SHBT99
  * Pin BBM Blackberry CS 2 : 2AE48042
  * Pin BBM Blackberry CS 3 : 2BD6A2E3
  * Whatsapp : +85581734021
  * Line : sahabatqq
  * Wechat : sahabatqq

  JibuFuta
 6. PERMAINAN ONLINE TERBESAR DI INDONESIA

  Website paling ternama dan paling terpercaya di Asia ^^
  Sistem pelayanan 24 Jam Non-Stop bersama dengan CS Berpengalaman respon tercepat :)
  Memiliki 8 Jenis game yang sangat digemari oleh seluruh peminat poker / domino

  - Adu Q
  - Bandar Q
  - Bandar Sakong
  - Bandar Poker
  - Poker
  - Domino 99
  - Capsa Susun
  - BANDAR66 / ADU BALAK ( GAME TERBARU )

  Permainan Judi online yang menggunakan uang asli dan mendapatkan uang asli ^^
  * Minimal Deposit : 20.000
  * Minimal Withdraw : 20.000
  * Deposit dan Withdraw 24 jam Non stop ( Kecuali Bank offline / gangguan )
  * Bonus REFFERAL 15 % Seumur hidup tanpa syarat
  * Bonus ROLLINGAN 0.3 % Dibagikan 5 hari 1 kali
  * Proses Deposit & Withdraw PALING CEPAT
  * Sistem keamanan Terbaru & Terjamin
  * Poker Online Terpercaya
  * Live chat yang Responsive
  * Support lebih banyak bank LOKAL


  Contact Us
  Website SahabatQQ
  WA 1 : +85515769793
  WA 2 : +855972076840
  Telegram 1 :+85515769793
  Telegram 2 : +855972076840
  LINE : SAHABATQQ
  TWITTER : SahabatQQ
  Kami Siap Melayani anda 24 jam Nonstop
  daftar sahabatqq
  Kontak SahabatQQ : Kontak SahabatQQ

  JibuFuta
 7. Bagi para penggemar yang ingin bermain Slot Online Deposit Pulsa Tanpa Potongan yang bisa dimainkan dengan sangat mudah dan dimanapun kapanpun kalian inginkan bisa langsung mengunjungi situs IDN89 yang sudah terpercaya melalui https://188.166.252.208/

  JibuFuta
 8. Bonus Welcome New Member 15% Untuk Semua Permainan

  - Bonus Dapat di Claim Seluruh Permainan di Situs BVGaming Kecuali Poker.
  - Untuk Claim Bonus Welcome New Member Minimal Deposit 200.000
  - Maksimal Bonus Dapat Di Claim Adalah 1.000.000
  - Bonus Dapat Langsung Claim Melalui Sistem Ketika Isi Form Deposit.
  - Syarat Withdraw Adalah Mencapai Turnover x10 Dari Nominal Deposit & Bonus
  Contoh : Deposit 1.000.000 + Bonus 150.000 = 1.150.000 x 10 = 11.150.000
  - Jika Tidak Mencapai Turnover, Maka Withdraw Tidak Dapat Dilakukan.
  - Tidak Dapat Digabungkan dengan Promo Rollingan & Cashback & Pindah Jenis Permainan Lain.
  - Tidak diperbolehkan double bet (bet kanan & kiri atau over-under dalam 1 pertandingan)
  - Bonus tidak berlaku jika terdapat persamaan IP address, nama rekening, no tlp dan email dengan member lain yang sudah terdaftar.
  - Pihak BVgaming Berhak Membatalkan Bonus Apabila Mendapati Kecurangan.

  Ayookkk banyak permainan slot di situs online judi kami dan terjamin sudah resmi

  Untuk informasi selengkapnya mari hubungin CS kami di BVGaming (24 jam online)

  WhatsApp: 0812 1495 2061

  JibuFuta
 9. เว็บ สล็อต ออนไลน์อันดับ 1 ในทวีปเอเชีย เป็นเว็บออนไลน์ ที่ดีเยี่ยมที่1ของไทย พีจี สล็อต ระบบน่าไว้วางใจ เล่นได้ จ่ายจริง ไม่มีต่ำ ฝาก-ถอน เร็วทันใจเล่นง่ายไม่ยุ่งยาก ทำเงิน ได้จริง

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3