Mambo Yanayokuza Motisha kwa Wafanyakazi
Pengine umewahi kufanya kitu kwa sababu tu ulilazimika kukifanya. Moyoni hukusikia msukumo wowote isipokuwa hofu ya kushindwa kufikia matarajio ya mtu mwingine. Lakini pia inawezekana umewahi kufanya kitu bila kusukumwa wala kufuatiliwa. Ndani yako unakuwa na furaha na msukumo unaokuhamasisha kutekeleza jambo si kwa sababu ya hofu iliyotengenezwa na wengine bali shauku ya kufikia kiwango kinachokupa kuridhika.