'Africans and Americans Embracing Cultural Difference', ni kitabu kizuri nilichokisoma kwa mara ya kwanza Aprili, 2009 nilipokiona katika duka la vitabu KIMAHAMA, Arusha. Ilikuwa ni baada ya kukisikia kikisemwa na rafiki yangu mmoja. Ni miaka mitano imepita, lakini kitabu hiki hakikuwahi kuizoea maktaba yangu tangu wakati huo. Kusoma kitabu chenye saini ya mwandishi, si jambo linalowatokea wengi. Ni muujiza ulionitokea. Picha: Jielewe Kwanza, kwa rafiki zangu wasomaji waliofika kwangu kwa mazungumzo ya vitabu na waandishi, kitabu hiki hakikukosekana kwenye mazungumzo hayo. Na kila aliyesikia sifa zake, alipenda kuthibitisha ikiwa nilisema kweli kwa kukiazima. Kiliazimwa na wasomi, wasafiri, waongozaji wa watalii (tour guide), wapenda maarifa, kutaja kwa uchache. Ni bahati mbaya sana kwamba hakikuwa kinapatikana katika baadhi ya maeneo. Hivyo, kiliazimwa, na kuazimwa, tena na tena kwa muda wa miaka miwili. Mwaka 2011, kiliondoka rasmi kwenye maktaba yangu. Nilikuja k...