Tunapenda ushirikina kuliko vitabu - Prof. Mbele


"...Umaafuru wa kitabu hiki (Rich Dad Poor Dad) nilianza kuusikia huku Marekani, miaka michache iliyopita.

Ni kati ya vitabu vingi ambayo vinasomwa na hao wenzetu, wakati jamii yetu ya Tanzania inaendelea kuzama katika giza au tunangojea kiongozi wa nchi au serikali ituletee maendeleo, na tukijitahidi sana, tunatumia ushirikina. Tuko tayari kulipa laki nyingi kwenye mambo ya ushirikina, eti tupate mafanikio, badala ya kununua vitabu na kuvisoma.

Sasa basi, pamoja na vibuyu vyetu, wenzetu wa-Kenya, ambao wamezingatia elimu tangu zamani, wanaingia nchini mwetu na kujichukulia ajira au kuanzisha miradi. Sisi bado tunahangaika na vibuyu badala ya vitabu. Tutakoma, maana wahenga walisema kuwa asiyefunzwa na mamake hufunzwa na ulimwengu. Na bora iwe hivyo, labda hatimaye tutapata akili.

Uzembe ulivyokithiri miongoni mwa wa-Tanzania, utawasikia wakilalamika mbona kitabu hiki hakijaandikwa kwa ki-Swahili? Wakishauliza hivi, wanaamini wametoa hoja nzito, badala ya kutambua kuwa wanapaswa wajifunze ki-Ingereza na lugha zingine ili waweze kusoma maandishi hayo. Wao wanangoja tu waandikiwe kwa lugha hii wanayoijua. Dunia itawakomesha, kama nilivyosema katika mahojiano na Radio Mbao.

Hao wenzetu wanaosoma "Rich Dad Poor Dad" hawaendi kwa waganga kutafuta vibuyu, bali wakimaliza kitabu hicho, wanaenda kutafuta kingine. Kwa mtindo huu, hatutaweza kushindana nao..."

Anamaliza Profesa Mbele katika kisanduku cha maoni kwenye posti ya pendekezo la kitabu kwa wasomaji wa blogu hii. Asante sana Profesa kwa kutuonya waswahili.

Maoni

  1. Shukrani kwa kusambaza ujumbe wangu kupitia blogu hii murua. Mahojiano yangu na Radi Mbao ni haya hapa.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Makundi Manne ya Tabia za Watoto Kitabia

Uislamu ulianza lini?