Umaafuru wa kitabu hiki nilianza kuusikia huku Marekani, miaka michache iliyopita.
Ni kati ya vitabu vingi ambayo vinasomwa na hao wenzetu, wakati jamii yetu ya Tanzania inaendelea kuzama katika giza au tunangojea kiongozi wa nchi au serikali ituletee maendeleo, na tukijitahidi sana, tunatumia ushirikina. Tuko tayari kulipa laki nyingi kwenye mambo ya ushirikina, eti tupate mafanikio, badala ya kununua vitabu na kuvisoma.
Sasa basi, pamoja na vibuyu vyetu, wenzetu wa-Kenya, ambao wamezingatia elimu tangu zamani, wanaingia nchini mwetu na kujichukulia ajira au kuanzisha miradi. Sisi bado tunahangaika na vibuyu badala ya vitabu. Tutakoma, maana wahenga walisema kuwa asiyefunzwa na mamake hufunzwa na ulimwengu. Na bora iwe hivyo, labda hatimaye tutapata akili.
Uzembe ulivyokithiri miongoni mwa wa-Tanzania, utawasikia wakilalamika mbona kitabu hiki hakijaandikwa kwa ki-Swahili? Wakishauliza hivi, wanaamini wametoa hoja nzito, badala ya kutambua kuwa wanapaswa wajifunze ki-Ingereza na lugha zingine ili waweze kusoma maandishi hayo. Wao wanangoja tu waandikiwe kwa lugha hii wanayoijua. Dunia itawakomesha, kama nilivyosema katika mahojiano na Radio Mbao.
Hao wenzetu wanaosoma "Rich Dad Poor Dad" hawaendi kwa waganga kutafuta vibuyu, bali wakimaliza kitabu hicho, wanaenda kutafuta kingine. Kwa mtindo huu, hatutaweza kushindana nao.
SAIKOLOJIA, neno lililotoholewa kutoka neno la kiingereza psychology, si elimu inayoeleweka sana katika jamii yetu. Asili ya 'psychology' ni neno 'psyche' lenye maana ya nafsi. Katika makala haya, tunasaili kwa ufupi maana ya saikolojia kama taaluma na kuonesha nafasi ya taaluma hiyo ngeni katika jamii yetu katika kutatua matatizo ya kijamii na hivyo kuharakisha juhudi za watu kujiletea maendeleo yetu.
WANAUME wengi wanaamini wanawake, kwa kawaida, ‘wanapenda hela.’ Kwamba ukiweza kumhakikishia mwanamke 'uhakika wa kiuchumi' unakuwa umemaliza. Ingawa hatuwezi kupuuza ukweli kuwa uhakika wa 'kiuchumi' ni moja wapo ya mahitaji ya mwanamke, lakini si sahihi kuamini kuwa moyo wa mwanamke unaweza kuthamanishwa kwa fedha. Fikra hizi walizonazo wanaume [kuwa anachokihitaji mwanamke ni fedha] zimeleta matatizo mengi katika mahusiano na ndoa. Kwa mfano, wapo wanaume ambao baada ya kuhakikisha wenzi wao wamepata mahitaji ya msingi, basi wanawatelekeza kihisia. Hali hii husababisha upweke mkubwa kwa wanawake hawa wanaojikuta hawana mtu wa karibu kuwasikiliza isipokuwa vitu.
Sipendi kutumia kiingereza kwa sababu kwanza ninadhani kiswahili kinanitosha kabisa kuelezea kile ninachotaka kusema. Hata hivyo najua pia matumizi ya kiswahili chetu hayajawa katika kiwango kile kilichokusudiwa. Kuna maneno mengi yasiyoeleweka vizuri katika kiswahili cha kitabuni. Moja wapo ya maneno hayo ni hili ninalolitumia leo hii. Haiba. Pengine niweke msisitizo kwa faida ya wale wasiolifahamu neno hili vizuri. Personality. Wengine wanasema maana ya hichi kinachoitwa personality ni utu kwa kiswahili. Ni bahati mbaya kwamba niliyakimbia masomo ya lugha siku nyingi. Ila nimejiridhisha kwamba haiba ndiyo tafsiri muafaka kabisa. Haiba ni nini? Watu wengine watafikiria tunazungumzia mwonekano wa mtu kimavazi. Lakini haiba ni neno pana zaidi ya mwonekano wa mtu kwa nje. Haiba ni jumla ya tabia za mtu zinazotokana na kile anachofikiri, anachopenda, anavyojichukulia yeye mwenyewe, anavyowachukulia watu wengine na kadhalika. Haya yote hujenga mwonekano wa mtu unaopimika (tabia) kama vi...
PICHA: thesouthern.com Siku moja nikiwa kwenye maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanafunzi wa shahada za awali waliingia kufanya mtihani wa muhula wa mwisho wa masomo. Wakati wanaingia, mmoja wao alijigamba kwamba hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kukanyaga maktaba tangu amejiunga na chuo hicho miaka mitatu iliyopita. Nilishangaa inawezekanaje mwanafunzi wa chuo kikuu kujisifia jambo la fedheha kama hilo.
Ingawa ni kweli tunazaliwa na sehemu ya tabia tulizonazo, upo ukweli wa kiutafiti unaothibitisha kwamba mazingira ya kimalezi yana nafasi kubwa katika kujenga tabia za mtu. Ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili, mathalani, unatawaliwa zaidi na uasili ambao kwa kiasi kubwa hatuna mamlaka nao. Hata hivyo, ukuaji wa kihisia na kimahusiano unatawaliwa zaidi na mazingira ya kimalezi ambayo tayari tuliyaona kwenye makala iliyopita .
YAMEKUWEPO madai kwamba Uislam ulianza tangu kuumbwa kwa dunia. Na wapo watu wanaotuaminisha hayo. Ukweli ni kwamba Uislam ulianzishwa na Nabii Muhammad mwaka 622 BK huko Arabia. Kabla yake, dini zilizokuwepo zilikuwa ni Uyuda ambayo ni dini rasmi ya Wayahudi (Judaism) na Ukristo ambayo ni dini ya mataifa wasio Wayahudi ulioanza miaka kadhaa baada ya Yesu kuwa ameondoka mwaka 33BK. Yesu mwenyewe hakuanzisha Ukristo. Alisali katika misikiti ya Wayahudi. Masinagogi. Maelezo haya yana msingi wa kistoria na sio propaganda za kidini. Ndio ni propaganda kwa sababu dini zote zimekuwa na tabia ya kuonyesha kwamba zenyewe ndizo za kweli kuliko dini nyinginezo hata ikibidi kwa kuichezea historia. Na ni bahati mbaya kwamba Dini zimekuwa na tabia ya kufanana ya kuzima uwezo wa waumini wake kuhoji lolote kwa kuwajengea hofu ya kujitafutia laana. Qur’an inatupa maelezo yanayokinzana kuhusu lini hasa Uislamu ulianza. Baadhi ya mistari katika kitabu hicho zinadai kwamba ‘nabii’ Muhammad ndiye ...
Makala haya yanasaili namna mtazamo wa awali wa watu wanaoamua kuingia katika uhusiano wa kimapenzi unavyoweza kuathiri kwa kiasi kikubwa namna wawili hao watakavyohusiana. Na tunaonesha namna kiwango cha mapenzi kati yao kinatengemea masuala matatu makuu; Ukaribu wa kihisia, tamaa ya mwili na maamuzi yao.
Umaafuru wa kitabu hiki nilianza kuusikia huku Marekani, miaka michache iliyopita.
JibuFutaNi kati ya vitabu vingi ambayo vinasomwa na hao wenzetu, wakati jamii yetu ya Tanzania inaendelea kuzama katika giza au tunangojea kiongozi wa nchi au serikali ituletee maendeleo, na tukijitahidi sana, tunatumia ushirikina. Tuko tayari kulipa laki nyingi kwenye mambo ya ushirikina, eti tupate mafanikio, badala ya kununua vitabu na kuvisoma.
Sasa basi, pamoja na vibuyu vyetu, wenzetu wa-Kenya, ambao wamezingatia elimu tangu zamani, wanaingia nchini mwetu na kujichukulia ajira au kuanzisha miradi. Sisi bado tunahangaika na vibuyu badala ya vitabu. Tutakoma, maana wahenga walisema kuwa asiyefunzwa na mamake hufunzwa na ulimwengu. Na bora iwe hivyo, labda hatimaye tutapata akili.
Uzembe ulivyokithiri miongoni mwa wa-Tanzania, utawasikia wakilalamika mbona kitabu hiki hakijaandikwa kwa ki-Swahili? Wakishauliza hivi, wanaamini wametoa hoja nzito, badala ya kutambua kuwa wanapaswa wajifunze ki-Ingereza na lugha zingine ili waweze kusoma maandishi hayo. Wao wanangoja tu waandikiwe kwa lugha hii wanayoijua. Dunia itawakomesha, kama nilivyosema katika mahojiano na Radio Mbao.
Hao wenzetu wanaosoma "Rich Dad Poor Dad" hawaendi kwa waganga kutafuta vibuyu, bali wakimaliza kitabu hicho, wanaenda kutafuta kingine. Kwa mtindo huu, hatutaweza kushindana nao.