Umaafuru wa kitabu hiki nilianza kuusikia huku Marekani, miaka michache iliyopita.
Ni kati ya vitabu vingi ambayo vinasomwa na hao wenzetu, wakati jamii yetu ya Tanzania inaendelea kuzama katika giza au tunangojea kiongozi wa nchi au serikali ituletee maendeleo, na tukijitahidi sana, tunatumia ushirikina. Tuko tayari kulipa laki nyingi kwenye mambo ya ushirikina, eti tupate mafanikio, badala ya kununua vitabu na kuvisoma.
Sasa basi, pamoja na vibuyu vyetu, wenzetu wa-Kenya, ambao wamezingatia elimu tangu zamani, wanaingia nchini mwetu na kujichukulia ajira au kuanzisha miradi. Sisi bado tunahangaika na vibuyu badala ya vitabu. Tutakoma, maana wahenga walisema kuwa asiyefunzwa na mamake hufunzwa na ulimwengu. Na bora iwe hivyo, labda hatimaye tutapata akili.
Uzembe ulivyokithiri miongoni mwa wa-Tanzania, utawasikia wakilalamika mbona kitabu hiki hakijaandikwa kwa ki-Swahili? Wakishauliza hivi, wanaamini wametoa hoja nzito, badala ya kutambua kuwa wanapaswa wajifunze ki-Ingereza na lugha zingine ili waweze kusoma maandishi hayo. Wao wanangoja tu waandikiwe kwa lugha hii wanayoijua. Dunia itawakomesha, kama nilivyosema katika mahojiano na Radio Mbao.
Hao wenzetu wanaosoma "Rich Dad Poor Dad" hawaendi kwa waganga kutafuta vibuyu, bali wakimaliza kitabu hicho, wanaenda kutafuta kingine. Kwa mtindo huu, hatutaweza kushindana nao.
WANAUME wengi wanaamini wanawake, kwa kawaida, ‘wanapenda hela.’ Kwamba ukiweza kumhakikishia mwanamke 'uhakika wa kiuchumi' unakuwa umemaliza. Ingawa hatuwezi kupuuza ukweli kuwa uhakika wa 'kiuchumi' ni moja wapo ya mahitaji ya mwanamke, lakini si sahihi kuamini kuwa moyo wa mwanamke unaweza kuthamanishwa kwa fedha. Fikra hizi walizonazo wanaume [kuwa anachokihitaji mwanamke ni fedha] zimeleta matatizo mengi katika mahusiano na ndoa. Kwa mfano, wapo wanaume ambao baada ya kuhakikisha wenzi wao wamepata mahitaji ya msingi, basi wanawatelekeza kihisia. Hali hii husababisha upweke mkubwa kwa wanawake hawa wanaojikuta hawana mtu wa karibu kuwasikiliza isipokuwa vitu.
SAIKOLOJIA, neno lililotoholewa kutoka neno la kiingereza psychology, si elimu inayoeleweka sana katika jamii yetu. Asili ya 'psychology' ni neno 'psyche' lenye maana ya nafsi. Katika makala haya, tunasaili kwa ufupi maana ya saikolojia kama taaluma na kuonesha nafasi ya taaluma hiyo ngeni katika jamii yetu katika kutatua matatizo ya kijamii na hivyo kuharakisha juhudi za watu kujiletea maendeleo yetu.
YAMEKUWEPO madai kwamba Uislam ulianza tangu kuumbwa kwa dunia. Na wapo watu wanaotuaminisha hayo. Ukweli ni kwamba Uislam ulianzishwa na Nabii Muhammad mwaka 622 BK huko Arabia. Kabla yake, dini zilizokuwepo zilikuwa ni Uyuda ambayo ni dini rasmi ya Wayahudi (Judaism) na Ukristo ambayo ni dini ya mataifa wasio Wayahudi ulioanza miaka kadhaa baada ya Yesu kuwa ameondoka mwaka 33BK. Yesu mwenyewe hakuanzisha Ukristo. Alisali katika misikiti ya Wayahudi. Masinagogi. Maelezo haya yana msingi wa kistoria na sio propaganda za kidini. Ndio ni propaganda kwa sababu dini zote zimekuwa na tabia ya kuonyesha kwamba zenyewe ndizo za kweli kuliko dini nyinginezo hata ikibidi kwa kuichezea historia. Na ni bahati mbaya kwamba Dini zimekuwa na tabia ya kufanana ya kuzima uwezo wa waumini wake kuhoji lolote kwa kuwajengea hofu ya kujitafutia laana. Qur’an inatupa maelezo yanayokinzana kuhusu lini hasa Uislamu ulianza. Baadhi ya mistari katika kitabu hicho zinadai kwamba ‘nabii’ Muhammad ndiye ...
Barua ya kuomba kazi ni waraka ambao mara nyingi husomwa kabla ya waraka mwingine wowote unaoambatanishwa katika kuomba kazi. Ni vyema barua ya kuomba kazi ikaandaliwa kwa umakini, na kujaribu kugusa kwa ufupi mambo yaliyoonekana kwenye wasifu binafsi kumvutia mwajiri mtarajiwa.
PICHA: thesouthern.com Siku moja nikiwa kwenye maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanafunzi wa shahada za awali waliingia kufanya mtihani wa muhula wa mwisho wa masomo. Wakati wanaingia, mmoja wao alijigamba kwamba hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kukanyaga maktaba tangu amejiunga na chuo hicho miaka mitatu iliyopita. Nilishangaa inawezekanaje mwanafunzi wa chuo kikuu kujisifia jambo la fedheha kama hilo.
Makala haya yanasaili namna mtazamo wa awali wa watu wanaoamua kuingia katika uhusiano wa kimapenzi unavyoweza kuathiri kwa kiasi kikubwa namna wawili hao watakavyohusiana. Na tunaonesha namna kiwango cha mapenzi kati yao kinatengemea masuala matatu makuu; Ukaribu wa kihisia, tamaa ya mwili na maamuzi yao.
Changamoto kubwa inayowakabili vijana wanaotafuta kazi ni namna ya kupata taarifa sahihi zitakazowasaidia kupata kazi. Ingawa vipo vyanzo vingi vya kupata taarifa hizo, watafuta kazi wengi hutegemea matangazo rasmi ya ajira pekee kupitia vyombo vya habari. Hata hivyo, tafiti za kazi na ajira zinaonyesha kuwa nafasi nyingi za kazi hasa katika sekta binafsi hazitangazwi hadharani. Waajiri wana tabia ya kutafuta mtu anayeaminika kupitia vyanzo vinavyoaminika. Tafsiri yake ni kuwa kijana anayetegemea kupata taarifa za kazi kupitia matangazo rasmi, anapitwa na taarifa nyingi muhimu.
Umaafuru wa kitabu hiki nilianza kuusikia huku Marekani, miaka michache iliyopita.
JibuFutaNi kati ya vitabu vingi ambayo vinasomwa na hao wenzetu, wakati jamii yetu ya Tanzania inaendelea kuzama katika giza au tunangojea kiongozi wa nchi au serikali ituletee maendeleo, na tukijitahidi sana, tunatumia ushirikina. Tuko tayari kulipa laki nyingi kwenye mambo ya ushirikina, eti tupate mafanikio, badala ya kununua vitabu na kuvisoma.