Hivi makala hizi zinasomwa kweli?

Leo nilikuwa natembea tembea nyumbani kwa Ndesanjo Macha. Nimejifunza mambo mengi nyumbani kwake.
Makala nyingi zimejaa maudhui mazito ambayo kusema kweli yana nafasi kubwa katika kuibadilisha jamii ya kitanzania. Tatizo ni kuwa Watanzania wengi anaowaandikia hawana muda na makala ndefu kama zake. Wanataka makala za ngono, fupi fupi zenye masimulizi ya kimapenzi!
Makala kama zake, sina hakika kama kweli zinasomwa na wengi, hasa vijana ambao kama wangezisoma zingewasaidia.
Swali nililotoka nalo ni kwamba makala kama hizi zinawasaidia wanaozisoma? Hivi wanazisoma hata hivyo?

Maoni

  1. Zinasomwa Bwaya ingawa sio kwa kasi inayotakiwa.Utaratibu wa kujisomea mdogo sana miongoni mwa vijana wa siku hizi.Wengi wametekwa na video.Wanasahau umuhimu wa kujisomea.

    JibuFuta
  2. Timiza nafasi yako kwanza, suala la usomaji linaanza na wewe. Mabadiliko yanaanza kwako na kisha kuyapeleka kwa wengine. Safari hii ndivyo ilivyo haina kukata tamaa maana kumbuka huko nyuma huenda nawe ulikuwa miongoni mwa kundi la wasiosoma lakini sasa unasoma na kisha unahoji wengine. Hiyo inafafanua kasi ya mabadiliko. Hakuna kukata tamaa kasi ya kuamsha fikra ni ukombozi maridhawa unaohitajika Afrika. Cheza karata yako inawezekana!

    JibuFuta
  3. pia hamasisha na wengine kujiunga na kusoma. ikiwa wanaglobu wa ethiopia wamedurufu na nadhani mara 4 kwa sasa wamesidi milioni moja mara tu baada ya kunyanyaswa kwenye uchaguzi mkuu. itakuwa sisi? addis internet cafe bado ni za kutafuta sembuse sisi kila mtaa?

    nilikuwa na mawazo kuwa haya tunayoyaandika baadae yaingie kwenye vitabu vipya vya uraia kureplace vile vya darubini.

    cheers

    JibuFuta
  4. Najua wapo wanaopenda kusoma. Si wengi, lakini wapo kama anavyosema Jeff. Hoja yangu ni kwamba, kwa kuwa kasi ya kujisomea ni ndogo sana katika jamii yetu na kwa kuwa wachache wanaojisomea wanapenda kusoma udaku zaidi na habari zisizo na mchango wowote wa Maendeleo yao na taifa lao, na kwa kuwa ili tulete mabadiliko katika jamii tunamoishi; Hivi hakuna namna inayoweza kufanyika kuwafikia katika udaku huo huo huko huko wanakokupenda? Sababu ni kwamba kasi ni ndogo sana waungwana! Watu hawana mpango na hoja nzito nzito jamani!

    JibuFuta
  5. Msaki, ni kweli tunahitaji kuhamasisha vijana wenzetu wapende kusoma. Kazi ni kubwa maana siku hizi mtu anasoma anachojua kitaulizwa kwenye mitihani. Ndio maana ni wachache sana ,kama alivyowahi kusema Ndesanjo, wanazijua hata ilani za vyama vyetu, katiba na mambbo kma hayo. watu kama hawa, wavivu kama hivi itachukua muda kuwashawishi.
    Tujitahidi hata hivyo.

    JibuFuta
  6. Bwaya, kitendo cha makala zangu kusoma na mwalimu mtarajiwa ambaye atakuja kugusa akili na nafsi za watoto shuleni kinanipa furaha kubwa sana. Hata nikisoma na wewe tu nchi nzima, nitaendelea kuandika tena kwa hamasa kubwa. Kwangu nitajisikia kuwa ninafanikisha kazi ninayoamini kuwa ni sehemu ya harakati za ujenzi wa jamii mpya.

    JibuFuta
  7. bwaya,

    zinasomwa hata hivyo. mimi kila mtu niliyekuwa na anuani yake (karibu 300) niliwatumia habari hizi na wote wanazisoma.

    hapa nilipo nikitumika kwa sasa, watz woote wanasoma. sema sio wote wachangiaji kwa kuandika, huwa wannachangia kwenye vikao vya jioni. na kwa ufupi wamesema ni za msingi saaaaannaaaa!!

    kaza buti!

    JibuFuta
  8. Wasoma wachache, lakini bado wengi wao uelewa wa hizo makala unatia shaka. Ndesanjo anatumia nguvu nyingi kuweka hizo makala lakini sijui kama watu wanatumia nguvu japo kidogo kuzielewa.

    JibuFuta
  9. Wanablogu karibu wote, wanaandika masuala yanayotugusa sisi moja kwa moja. Ila kuna haya machache nitasema. kwanza matumizi hasi ya teknolojia ya mtandao wa intaneti ni tatizo kwa jamii kubwa sana ya Watanzania hasa vijana. Matumizi hasi kama vile kutumia mtandao kujadili zaidi masuala yanayohusiana na ngono, muziki wa magharibi, kutongozana n.k. tembelea www.darchat.com na www.darhotwire.com hiyo ni kwa uchache na ndio ambayo inawakusanya vijana wengi (naamini hivyo) kutwa nzima mpaka usiku wa manane. Pili hakuna 'promotion' ya kutosha kwa vijana kutumia mtandao wengi kwa wingi wetu.

    JibuFuta
  10. Wanablogu karibu wote, wanaandika masuala yanayotugusa sisi moja kwa moja. Ila kuna haya machache nitasema. kwanza matumizi hasi ya teknolojia ya mtandao wa intaneti ni tatizo kwa jamii kubwa sana ya Watanzania hasa vijana. Matumizi hasi kama vile kutumia mtandao kujadili zaidi masuala yanayohusiana na ngono, muziki wa magharibi, kutongozana n.k. tembelea www.darchat.com na www.darhotwire.com hiyo ni kwa uchache na ndio ambayo inawakusanya vijana wengi (naamini hivyo) kutwa nzima mpaka usiku wa manane. Pili hakuna 'promotion' ya kutosha kwa vijana kutumia mtandao wengi kwa wingi wetu.

    JibuFuta
  11. Pengine wale wenye kuweza kupata nafasi ya kuandika magazetini washawishi watu kutembelea blogu kama vile blog round ups za wiki halafu tuone itakuwaje.
    Sijasoma magazeti (ya kuchapa) ya nyumbani kwa siku nyingi, labda hili linafanywa tayari, kama bado halifanywi basi tuwatongoze vijana wapate kutembelea blogu zenye visa vingine zaidi ya mambo ya popular culture na falme nyingine za kibepari.

    JibuFuta
  12. Ni wakati muafaka wa kubadilika kifikra katika zama hizi za utandawazi ambao....piga ua umeathiri vijana wengi wa kizazi kipya, aidha ni muhimu kama alivyosema Mwandani kwa waandishi wa habari kujaribu Ku -kupromot Blogu na kuwavuta wasomaji waje huku waone nini kinachoendelea katika dunia ya mtandao wa habari na mawasiliano.

    JibuFuta
  13. Ni muhimu kwa waandishi wa habari kutangaza na kuwaonesha wasomaji namna ambavyo mtandao wa habari na mawasiliano ulivyobadilika, hili ni jukumu kwa watumiaji wa blogu, vinginevyo taarifa zetu zitakuwa zinatuzungukia wenyewe bila kufika kwa walengwa.

    JibuFuta
  14. Umesema wengi wanapenda makala zilizo na maudhui ya kimapenzi. Kweli kabisa. Mapenzi ni kiungo muhimu cha maisha kiasi kwamba watu watapenda habari, sinema ,riwaya au mchezo wa kuigizwa uliohanikizwa maswala ya mapenzi. Swala la mapenzi huwaondoa watu katika ulimwengu halisi na kuwasafirisha katika ulimwengu mwingine usio na matatizo.

    Ngano zisizo na maudhui ya mapenzi huwa zimejaa busara ndio, lakini mara nyingi huachiwa wanafilosofia kuzisoma.....

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Makundi Manne ya Tabia za Watoto Kitabia

Uislamu ulianza lini?