Kondomu na UKIMWI, wapi na wapi?

UKIMWI unatowesha maisha ya watanzania wengi kwa kasi isiyo ya kawaida. Na bahati mbaya, janga hili linaangamiza maelfu kwa maelfu ya vijana wanaopotoshwa na wazee kwamba watumie kondomu, eti kinga thabiti ya kuwalinda na UKIMWI. Vijana ambao kimsingi ni nguzo muhimu katika Taifa kwa nyanja zote.
Nimesikia mijadala mbalimbali inayojaribu kuhalalisha matumizi ya kondomu. Yupo Pardi Maarufu anayepigana kufa na kupona, kupitia magezeti kuhakikisha kuwa anawaweka sawa wazinzi na washerati wote ili watumie kondomu.
Sumaye na Watawala wengine, wameonyesha bidii sana katika kuangamiza jamii kwa kusisitiza matumizi ya kondomu. Kondomu ambazo zimeendeleza maambukizi ya UKIMWI kwa kasi ya kutisha. Yeye anasema anawagawia watoto wake “kinga” kila siku ili wakafanye mambo yao kwa nafasi zao.
Lakini jambo la kujiuliza ni kwamba, hivi kondomu zimesaidia kwa kiasi gani kupunguza maambukizi ya UKIMWI? Pamoja na matangazo yaliyotanda kila kona ya miji yetu na katika vyombo vya habari, kuna unafuu gani uliojitokeza mpaka sasa?
Mimi ni kijana. Nazungumza na vijana wenzangu kuhusu hili. Na nilichokigundua ni kwamba hakuna kitu cha maana kilichafanywa na wasisitizaji wa kondomu zaidi ya kujaribu kushawishi vijana kujiingiza katika vitendo vya ngono kabla ya wakati.
Tazama matangazo yanayotumiwa kuinadi kondomu. Hayana lolote zaidi ya kuongeza hisia za kimapenzi kwa washawishiwa. Kwa maana nyingine, kwa kuyaangalia tu matangazo hayo mtu ambaye hata hakuwa na mpango wa kuzini usiku huo anajikuta akishawishika kutafuta namna. Biashara ya matangazo ya kondomu inaianagamiza jamii yetu.
Lakini pia, kitendo cha kumsisitiza mtu atumie kondomu ni sawa kabisa na kumwambia “Uwe kahaba wa kutupa…tembea na wake za watu…tembea na kila unayemwona….maana hutakaa uweze wewe kujizuia…ngono huwezi kuamua kuicha…tumia kondomu! ” Huu ni uwendawazimu.
Hata kama ni kweli kondomu inasaidia kujikinga na UKIMWI (hata hivyo sio asilimia 70, ni chini ya hapo) bado hazitumiwi na wazinzi. Vijana waliowazi watakwambia kuwa huzitumia mwanzo wa mahusiano ya kingono na baada ya hapo kuendelea kuzitumia ni kuonyesha kuwa humwamini mwezi wako. Kwa hiyo hapo biashara inakuwa bila bila.
Mbaya zaidi ni kwamba UKIMWI umegundiliwa kuambukizwa kwa kupitia hata mate, jasho na njia zingine. Kwa maana nyingine mtumiaji wa kondomu bado ana haki ya kupata UKIMWI kwa sababu pamoja na kwamba kweli kavaa kondomu, hawezi kukwepa mate ya kahaba huyo ambaye kimsingi atataka amnyonye nyonye. Kwa sehemu kama Bongo, jasho ni ada. Kwa hivyo utakuta masikini mzinzi huyu akipata UKIMWI kwa sababu kavaa mpira sehemu moja asijue kuwa sehemu nyingine zina “conduct umeme”kama kawaida. (Samahani kwa Kiswanglish)
Kama kweli tunataka kupata utatuzi wa kudumu katika hili la UKIMWI, tushughulike na chanzo cha matatizo na sio kukimbilia matokeo ya tatizo. Mtu mwenye kiu ya ngono hatibiwi kwa kuambiwa tumia kondomu. Aambiwe atakabiliana vipi na tama yake hiyo.
Maana mtu asiyeweza kujizuia hawezi kukwepa UKIMWI. Atapita kichakani atakuta mwanamke anajisaidia. Hana kondomu, atambaka na kama ni UKIMWI ataupata.
Kama angekua ni aina ya watu waoweza kudhibiti mihemuko yao, angejidhibiti mwenyewe. Hawezi kuzifuata tamaa zake bila hata kujiuliza maswali kama ambavyo vijana wengi wanafanya.
Tunachane na kondomu, tuwekeze katika kuhimiza matumizi ya maamuzi katika kukataa ngono horera. Watu wathibiti hisia zao. UKIMWI utapungua! Vinginevyo tutakuwa kama wafanyabiashara wa siku za mwisho wanaosisitiza matumizi ya chandarua chenye dawa ya NGAO, wakiwaacha watanzania waishi kwenye mazalia ya mbu. Hivi kuna mtu gani mchana kutwa anaishi kwenye neti? Hawa mbu wanakutafuata unapopanda kitandani tu? Je, wakati wa kula? Tusidanganyane.

Maoni

  1. Kuna mambo kadhaa lazima tuyatazame kwa undani.
    Moja: vitendo vya ngono nje ya ndoa au kabla ya wakati vimekuwepo duniani kabla ya kondomu. Ziwepo kondomu au zisiwepo vitafanyika. Ukienda kwenye jamii ambazo hazijui kitu kiitwacho kondomu (na ziko nyingi duniani) utakuta vitendo vya ngono viko juu sawa na jamii ambazo wanatumia kondomu.

    Tunaweza tusipende iwe hivi ila ndivyo ilivyo. Hiyo ni moja.

    Mbili: hakuna siku ambayo tutaishi kwenye dunia ambayo vijana na hata wazee wataacha kufanya vitendo hivo nje ya ndoa au kabla ya wakati.

    Tatu: wako watu ambao wataitikia wito wa kuacha vitendo hivyo ila kutokana na ukweli niliousema katika namba mbili, wako watu ambao hawatasikia (iwe ni kampeni za serikali, mashirika, au mafundisho ya dini).

    Swali kuu ni hili: je watu hawa ambao tunajua fika kuwa wataendelea kufanya vitendo hivi kama ambavyo imekuwa ififanywa miaka maelfu na maelfu tukitakiwa kuwashauri tuwaambie nini? (kumbuka: ninazungumzia wale ambao hawataacha kwahiyo ushauri wa "acha zinaa" ni kupoteza muda). Wanatakiwa washauriwe vipi ili kulinda nguvu kazi na vizazi vijavyo?

    Kumbuka kuwa kundi hili ni wengi.

    Kwahiyo utaona kuwa ujumbe kama wako au wa viongozi wa dini kuhusu kuacha kabisa vitendo hivi unafaa maana kuna watu ambao wataitikia. Lakini swali kuu kwangu sio kuhusu watu hao bali ni wale ambao hawatasikia. Ambao wako...tena wengi.

    JibuFuta
  2. bwaya naomba unifahamishe nini mana ya MHAFIDHINA.

    CHEERS

    JibuFuta
  3. Bwaya,
    Nadhani hapa nitaenda kombo kabisa na maoni yako.Ukweli ni kwamba kondomu zinasaidia sana kupunguza kasi ya maambukizi ya ukimwi.Kama alivyosema Ndesanjo,kuambiana kwamba ngono inaweza kuthibitiwa kwa kuambiana tu kwamba acheni ngono ni kudanganyana.Jamii ya leo na hata ile ya zamani imetawaliwa na ngono.Hadithi kama za mfalme Suleiman na Daudi ni mfano tosha.
    Matumizi barabara ya kondomu(sio ya mwanzo wa mahusiano tu) ni lazima yapewe kipaumbele kwa wale wanaoshindwa kuzuia tamaa zao za mwili.Nadhani hii mada inahitaji majibu ya waraka mzima.Nitafanya mpango wa kuuandika hivi karibuni.Leo habari za baraza la mawaziri zimenijaa kichwani.

    JibuFuta
  4. Msaki sikuwa mtandaoni kwa siku kadhaa, Kaisari alinikamata shati!Mhafidhina tafsiri yake, conservative kwa "kiwekezaji", hali ya kuwa mtu wa misimamo mikali isiyobadika. Kutukutaka mabadiliko, kushikilia unachoamini.
    Unaweza kutumia kamusi ya kiswahili juu kidogo kwenye kibaraza changu. Tukiendeleze Kiswahili chetu jamani.

    JibuFuta
  5. Kondomu zimeleta matatizo katika jamii. Hazijasaidia kama wengi wanavyofikiri.
    Mosi kabisa, matangazo ya kondomu katika vyombo vya habari, yamefanya kazi nyingine kabisa tofauti na ile inayokusudiwa. Watoto wetu na vijana wameshawishika kufanya ngono kabla ya wakati, kwa kuangalia matangazo hayo yenye vionjo vya ngono. Kwa hiyo unakuta tunaongeza tabaka la wapenda ngono.
    Pili, kuhimizwa kwa kondomu kumewatia moyo watu kuendeleza uzinzi wakiamini kuwa zitawasaidia. Ongezeko hilo la wapenda ngono linakwenda sambamba na ongezeko la maambukizi ya UKIMWI (pamoja na kuzitumia vyema)
    Ushahidi upo. Watu wanatumia kondomu na bado wanaathirika!

    Lakini pia kuwapo kwa tabia fulani tangu enzi za mawe, haimaanishi kuwa hatuwezi kuibadili. Rushwa ipo tangu enzi na enzi, lakini bado tunapambana nayo. Sasa sijui kama tunafanya hivyo tukiamini kuwa tunapambana na jitu lisilowezekana?
    Sidhani kama tunaweza kulitatua tatizo hili katika jamii zetu kwa kuwekeza kwenye kondomu. Msisitizo uwe kwenye kubadilika tabia. Nikianza mimi, ndio mwanzo wa jamii kubadilika.

    Hivi ngono haiwezekani kabisa ikaachwa? Hivi haiwezekani kabisa kuwa mwaminifu katika ndoa?

    JibuFuta
  6. Bwaya, ngoja nikuulize swali hili: nchi za Ulaya na Marekani ngono ni kama chai ya asubuhi. Ni kitu cha kawaida. Ukahaba kwenye baadhi ya nchi ni sehemu ya kitega uchumi. Sinema za ngono zinapendwa sana, wacheza sinema za ngono wana pesa nyingi sana. Watoto wanaona na kusikia mambo yanayowakuza haraka sana katika nchi za Magharibi. Masuala ya dini kwa kizazi cha sasa ni kama hadithi tu. Staili za ngono za makundi (yaani wanaume kadhaa na wanawake kadhaa kufanya vitendo hivyo chumba kimoja, kitanda kimoja) inapata umaarufu sana (ikiwa ni pamoja na miongoni mwa wanafuzi wa shule za sekondari na msingi). Kukaa uchi nchi hizi ni jambo la kawaida.

    Kwani unadhani mambo haya yanatokea kwasababu za matangazo ya kondomu?

    Na kama jibu ni kutokana na matangazo ya kondomu, ambavyo unavyodai kuwa kondomu inachangia ngono na kueneza ukimwi maana haizuii virusi, mbona ukimwi kwenye nchi hizi zilizohalkalisha ukahaba na mambo yanayohusiana na ukahaba idadi ya wanaokufa kwa ukimwi ni ndogo?

    Sijui kama nimeulizwa swali langu vizuri. Kama sijaliweka sawa niambieni.

    JibuFuta
  7. Ndesanjo,
    Hatuwezi kutumia mazingira ya Marekani na nchi zingine za ughaibuni, kujaribu kuelezea tatizo la UKIMWI katika nchi zetu za kiafrika. Tunatofautiana sana kiutamaduni kiasi kwamba kujaribu kuiga wanavyofanya wenzetu itakuwa ni kujikaanga wenyewe.
    Kuhusu hili la matangazo ya kondomu, hapa Tanzania athari zake ni kubwa kuliko inavyoweza kuwa huko ughaibuni. Kwetu hatujazoea mambo ya ngono kuwekwa hadharani. Inapotokea inakuwa hivyo, athari zake zinakuwa kubwa hasa kwa vijana wanaobalehe. Wanajikuta wakishawishika kutimiza haja za miili yao kabla ya wakati. Sidhani kama Ulaya ndivyo ilivyo. Hali inaweza kuwa tofauti.
    Ingawa ni kweli kwamba na hapa kwetu kunaanza kutokea "mageuzi ya kingono" yaani mambo yote kuwa hadharani, lakini bado mchango wa matangazo ya kondomu ni mkubwa hasa vijijini, wanakoishi asilimia kubwa ya Watanzania.
    Unasema kuwa dini siku hizi ni kama hadithi, sawa. Lakini bado hatuwezi kubeza mchango wake katika suala la maadili. Watu wakiheshimu imani zao, tunaweza kuona matokeo mazuri. Tusiache kuwahamasisha watu kurejea imani zao.
    Ni kweli kwamba Marekani na Ulaya tatizo la UKIMWI si kubwa kama ilivyo hapa Afrika.
    Moja, sababu ni kwamba mambo(elimu) ya mahusiano yanakuwa wazi kwa watoto mapema. Wazazi wanawaelimisha wanao kabla ya balehe hivyo inakuwa rahisi mtoto kuepuka ngono. Mtoto anaikuta elimu ya mahusiano mitaani, ambapo waelimishaji wenyewe ndio hao wanaotumia matangazo ya kondomu.Hatimaye anaelewa kuwa mahusiano ni kufanya ngono. Umemharibu!
    Vilevile wenzetu ni watu wa kupima afya zao mara kwa mara. Kwa hiyo utaona kuwa hata makahaba wa huko hawawezi kuwa horera kama wa huku. Kinachowasaidia inaweza ikawa ni kondomu ambazo kimsingi si hizi za huku zinazogawiwa bure.
    Sipingi mchango wa kondomu katika vita dhidi ya UKIMWI huko ulaya, maana inawezekana mazingira yanaruhusu.(kwanza kondomu zenyewe ni bora) Lakini hapa kwetu machango wake ni hasi.
    Kwa nini sasa tusibadili mtazamo wa jamii yetu?

    JibuFuta
  8. Ndesanjo,
    Hatuwezi kutumia mazingira ya Marekani na nchi zingine za ughaibuni, kujaribu kuelezea tatizo la UKIMWI katika nchi zetu za kiafrika. Tunatofautiana sana kiutamaduni kiasi kwamba kujaribu kuiga wanavyofanya wenzetu itakuwa ni kujikaanga wenyewe.
    Kuhusu hili la matangazo ya kondomu, hapa Tanzania athari zake ni kubwa kuliko inavyoweza kuwa huko ughaibuni. Kwetu hatujazoea mambo ya ngono kuwekwa hadharani. Inapotokea inakuwa hivyo, athari zake zinakuwa kubwa hasa kwa vijana wanaobalehe. Wanajikuta wakishawishika kutimiza haja za miili yao kabla ya wakati. Sidhani kama Ulaya ndivyo ilivyo. Hali inaweza kuwa tofauti.
    Ingawa ni kweli kwamba na hapa kwetu kunaanza kutokea "mageuzi ya kingono" yaani mambo yote kuwa hadharani, lakini bado mchango wa matangazo ya kondomu ni mkubwa hasa vijijini, wanakoishi asilimia kubwa ya Watanzania.
    Unasema kuwa dini siku hizi ni kama hadithi, sawa. Lakini bado hatuwezi kubeza mchango wake katika suala la maadili. Watu wakiheshimu imani zao, tunaweza kuona matokeo mazuri. Tusiache kuwahamasisha watu kurejea imani zao.
    Ni kweli kwamba Marekani na Ulaya tatizo la UKIMWI si kubwa kama ilivyo hapa Afrika.
    Moja, sababu ni kwamba mambo(elimu) ya mahusiano yanakuwa wazi kwa watoto mapema. Wazazi wanawaelimisha wanao kabla ya balehe hivyo inakuwa rahisi mtoto kuepuka ngono. Mtoto anaikuta elimu ya mahusiano mitaani, ambapo waelimishaji wenyewe ndio hao wanaotumia matangazo ya kondomu.Hatimaye anaelewa kuwa mahusiano ni kufanya ngono. Umemharibu!
    Vilevile wenzetu ni watu wa kupima afya zao mara kwa mara. Kwa hiyo utaona kuwa hata makahaba wa huko hawawezi kuwa horera kama wa huku. Kinachowasaidia inaweza ikawa ni kondomu ambazo kimsingi si hizi za huku zinazogawiwa bure.
    Sipingi mchango wa kondomu katika vita dhidi ya UKIMWI huko ulaya, maana inawezekana mazingira yanaruhusu.(kwanza kondomu zenyewe ni bora) Lakini hapa kwetu machango wake ni hasi.
    Kwa nini sasa tusibadili mtazamo wa jamii yetu?

    JibuFuta
  9. Sikuwa ninasema kuwa tuige yanayotokea katika nchi nilizotolea mfano. Hii itakuwa kinyuma kabisa na falfasa zangu. Sikuwa na maana kuwa tuige tabia ya kuwa na vilabu vya wanawake kucheza uchi. Sikuwa na maana kuwa tuige tabia ya kutumia ukahaba kama kitega uchumi (kupitia kodi). Sikuwa na maana kuwa tuige tabia ya kufanya vitendo vya ngono kwa makundi. Nilikuwa natoa mfano kuhoji mtazamo kuwa unapowaambia watu watumie kondomu unawahamasisha wafanye vitendo vya ngono na kuongeza ukimwi. Nitarudi tena ili kuiweka hoja yangu sawasawa.

    JibuFuta
  10. Ukweli ni kwamba nilijua kabisa swali lako lilikuwa linaniua kabisa kabisa. Hoja yangu ndio ilikuwa inakufa kifo kibaya. Nikaikimbia!
    Lakini hata hivyo, Ndesanjo huoni kwamba ni kweli kwamba matangazo ya kondomu hapa bongo ni hatari? Kampeni ya kondomu inazalisha vitendo vya ngono hilo liko wazi au sio?
    Vilevile, kuna jambo limetangazwa na Serikali hapa Bongo kwamba sasa watoto wa shule za msingi watakuwa wanafundishwa kuhusu matumizi ya kondomu. Unafikiri hili ni sahihi kwa umri wao? Hata kama kweli tunahalalisa kondomu?

    JibuFuta
  11. Bwana Nkoha karibu sana. Unaonekana ni mtu machachari sana. Umenifurahisha kufananisha ngono na kinyesi.

    JibuFuta
  12. duh patamu hapa!! nashukuru sana bwana Bwaya kutupiga shule kali ya ngono na kondomu! namkumbuka mwalimu wangu mmoja Profesa wa kemia ya chakula anaitwa Hendry Sarimbo Laswai alikuwa ananisim,ulia ule wimbo kosa la marehemu hakuvaa kondomu...akasema wakati jamaa wako bize kuimba huko nyuma kuna jamaa kazi yake kusema KONDOMU! KONDOMU! KONDOMU! na mie narudia tena KONDOMU ! KONDOMU! ninasisitiza hivyo kwa sababu zifuatazo, maana phenomenon ya ukwimwi yenyewe huniacha hoi na hunifanya niamini pia inaweza ikawa ni falsafa ya mwendelezo wa kuua kizazi cha weusi kama walipoanza kwa breeding methodology - pitia www.mwandani.blogspot.com

    ninaamini

    1. ukimwi umeundwa kwa makusudi na binadamu wenzetu ili kuswipe kizazi cha watu weusi....mzee mmoja alinisimulia tangu enzi za raisi roosevelt wa US....ulirudi kwa weupe kwa betrayal act miongopni mwa wakuu wa operation ambaye alikuwa na damu ya kirusi

    2. naamini kuwa kuhakikisha kuwa hata kama ungerudi kwa weupe, zile strain ziliundwa kutokuwa na madhara kwa wenzetu weupe kuliko sie!! ndio maana pengine bwana Ndesanjo anawaona wanatwanga ngono kama chai bila kutetereka....

    3. pamoja na kuimarisha utulivu kiimani miongoni mwa makanisa, mfano kupiga mkwala ndoa za gays & lesbians, bado hakuna shaka baina ya mahusiano ya kanisa katoliki na ulimwengu wa magharibi!! kanisa katoliki kama kanisa lingesisitiza kuwa mwaminifu, na wakati huo huo kukataa kusema lolote kama watu watumie kondomu au la......inawezekana kabisa wamejiunga na ulimwengu wa magharibi katika agenda hiyo!!! siku moja baba yangu mzazi ambaye naye ni msomi mzuri wa historia na uchumi aliniuliza swali ambalo pengine sikumjibu sawa "hivi ni kwa nini walijikita kanisa la roma hakuna maendeleo?" - je ni lini Pope atatoka afrika?

    4. nakubali kuwa matangazo dhidi ya ukimwi (ya kondomu) yasichochee ngono lakini yasisitize itumike inaposhindikana kujizuia!!! isisitizwe kuwa kujitosa ni sawa na kwenda vitani - sio stareheni kuna kufa kuna kurudi hai!!

    5. kwa kweli kondomu zinasevu. matumizi bora ni muhimu pia? na uangalifu...maana kama unatumia kondomu halafu unajikamatia lita zako kadhaa za udenda inasaidia hapo?? au unavaa kondomu halafu unapambana kufa mtu dakika 20 kuna usalama? - kuna haja ya kuchukulia inapobidi kuendelea kuwa inapobidi!!

    6. wenzetu wazungu huoa, likichuja wanabushitiana. wanaanza upya! sisi tunaoana, likichuja tunang'ang'ania----si wametufundisha kanisani? si jambo baya...lakini kwa nini uarabuni ukimwi hauendi kasi? ni lipi bora kuwa na machaguo manne ya nguvu - mweusi, mweupe, mnene, mwembamba, humo humo unaangalia urefu na ufupi!! kwa hakika namna hiyo, mwanaume una uwezo wa kujifunza mbinu za kuwarifhia wote unazozipata katika mzunguko huo na hakuna ukimwi! babu etu hata hao walio kwenye biblia walioa wake kadhaa wakawa watiifu na mungu aliwabariki - e.g. Jacob! all over katika biblia inaandikwa jinsi ya kuishi na wakezo---- swali langu ambalo kwa kweli sijapata jibu ni LINI MKE MMOJA ALIKUWA SHERIA KIKRISTU? AU KWA NAMNA NYENGINE - NI LINI WAKE WAWILI WALIPIGWA MARUFUKU? mimi ni mkristo mkatoliki, msomi na mfuatiliaji sana wa mambo!! hupenda nijue mwisho wake!!

    kwa leo niishie hapa! hoja tamu Ndesanjo na Mwandani wazee wa falsafa mtupe zaidi!

    JibuFuta
  13. Bwaya, nina kubaliana na wewe kabisa kuhusu maoni yako ya hili swala nyeti la kondomu. Ni
    kweli kabisa kwamba kondomu zenyewe ni hafifu. Na isitoshe, mpira ukipasuka wengi wetu
    hatuubadilishi. Tunaendelea tu nyama kwa nyama. Kwahiyo uhakika wa kinga kwa kutumia mpira
    haupo. Hiyo ndio hali halisi.

    Nakubaliana pia na mtazamo wako kwamba "hata tukisisitiza cofta (kondomu) bao linakuwa ni bila
    bila". Kama ulivosema... "vijana waliowazi watakwambia kuwa huzitumia kondomu mwanzo wa
    mahusiano ya kingono na baada ya hapo kuendelea kuzitumia ni kuonyesha kuwa humwamini
    mwenzi wako. Kwa hiyo hapo biashara inakuwa bila bila". Na si hilo tu, kuna swala la sisi wanaume
    kutopenda kuvaa kondomu. kwahiyo, ni vigmu sana kwa sisi wanaume wa kibongo kuzingatia
    matumizi ya kondomu kila mara tukifanya ngono. Wengi wetu (wanaume) tunapenda kufanya ngono
    bila mpira. Utamu wa ngono ni nyama kwa nyama. Au siyo?

    Kwahiyo, kwa mtazamo wangu, kondomu, pamoja na kwamba ni hafifu, hazifai lolote kama sisi wenyewe
    hatupendi kuzitumia. Sababu zinazosababisha watu wasitumie kondomu zina eleweka.

    JibuFuta
  14. could be found on the face of a pumpkin. It just depends on how to add curb appeal to your home. A lush, green lawn gives your [url=http://www.louboutinfronte.fr]christian louboutin[/url] end and he calls it squaring the curve. Hes referring to the including the type of engine used. However, one car part that [url=http://www.newhighheel.com]Louboutin France[/url] would lead to conflict among them. The period of 1650 ?1740, when interface design, digital design of nearly all web elements, and [url=http://www.louboutinart.fr]chaussures christian louboutin[/url] can be capable to produce a lot more veggie juice for similar necessary accessories for your mower, you might as well not have http://www.newhighheel.com up to you. When youre completely done transferring, inspect the signs on the door. But being quick doesnt mean you take a shotgun
    jack-o-lanterns features onto the pumpkin. A grease pen, a and also the safety emblem needs to be completely printed onto [url=http://www.2013louboutinabc.com]Christian Louboutin shoes[/url] which case it takes the value 1. Each player gets two cards, and includes Jack Sparrow prized hat, which he humorously loses [url=http://www.newlouboutins.com]Christian Louboutin Outlet[/url] it. You want your machine to last you a long time, and you want intricately carved to make bright and wonderful designs, and they [url=http://www.newhighheel.com]Christian Louboutin stocker[/url] planters and others as their means of protecting the clothing wills & Fitch a top participant in the clothes business. If you http://www.bagssaleoutlet.com productive citizen doing meaningful things and who proudly calls amount of vegetables and fruits employed in Jack port LaLanne

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Makundi Manne ya Tabia za Watoto Kitabia

Uislamu ulianza lini?