Makala hii ingesomwa tungekuwa tulivyo?

Nimeirejea makala ifuatayo kwenye maktaba ya Mheshimiwa Ndesanjo. Kimsingi napenda uandishi wake.
Nimekumbana na makala hii ambayo sina hakika kama ilisomwa na watanzania. Nasisitiza kwamba tuna kazi ya ziada kuwabadilisha wapende kusoma.
Unapokuwa na jamii ya watu wanaopenda udaku inakuwa tabu. Mtoto anakua anakuta baba ni mpenzi wa magazeti ya udaku. Na yeye anakuwa mdaku hali kadhalika. Akiwa kwenye mtandao hataacha kuangalia ngono. Masuala nyeti hana muda nayo.
Nina wasi wasi kama tutaweza kufikisha ujumbe wa kubadilika kwa jamii ya jinsi hii (isiyopenda maandiko). Ndio maana hata suala la elimu ya uraia limekuwa gumu, maana andiko lenyewe lenye elimu hiyo halisomwi. Tutafute mbinu ya kuwabadilisha watu wa jamii yetu ambao nadiliki kusema wanateketea. Sijaribu kusema kwamba wanabalika, lakini nadhani, kasi hairidhishi. Sijui kama tunaweza kuwakuta huko huko kwenye magezi ya udaku?

Maoni

 1. Bwaya, umenifanya nirudie kuisoma makala hiyo. Asante. Tena wakati nikiirudia nimepata wazo kwa ajili ya makala ya gazeti la Mwananchi ya wiki ijayo.

  JibuFuta
 2. Hawasomi waptakiwavyo! hawasomi, Kama wangekuwa wanassoma nakala zote zile mambo nyeti kwao umasikini ungepungua. Ile nakala inayofandisha njia rahisi ya kulima mbogamboga ingeleta mafanikio hata mbogamboga zingeshuka bei sokoni lakini inapanda!
  Wanasoma udaku kunakoandikwa habari za waasherati, wasenge(...Ingawa wimbo huu...nibebe hawaupendi sababu umeongelea wasenge!). Watoto wanajiingiza kwenye tabia hii pia.
  Ndesanjo andika nakala nzuri kwa lugha nyepesi kuhusu hili kama ulivyoagiza.

  JibuFuta
 3. Bwaya hili la kuweka picha safi sana walau nimekuona sura na siku tukikutana naweza kukutambua japokuwa sasa hivi nafuga sharubu na minywele. Hongera kaka

  JibuFuta
 4. Bwaya,nashukuru kwanza kwa kunitembelea barazani kwangu,pili hili lililopo juu ya magazeti ya udaku a.k.a magazeti pendwa kama wamiliki wenyewe wanavyopenda yaitwe ni athari ya utandawazi na hili lazima tukubali tumeathirika nalo.
  Jukumu letu waandishi mbalimbali wa makala na wapelekaji ujumbe kwa njia za mitandao pepe kuliangalia hili na kulifanyia kazi.

  Nimepata changamoto ya kuzikita fikra zangu kwa ajili ya kuandaa makala maalumu kama ambavyo Bw. Ndesanjo amefikiria kufanya hivyo katika Toleo la Gazeti la Mwananchi nami nitajitahidi kuandaa makala ndefu ihusuyo Faida na hasara za utandawazi katika jamii ya Watanzania katika gazeti la MAJIRA.

  JibuFuta
 5. Bwaya,Nimeukubali kwa kuuchamua ukweli mimi ningekuwa na sauti mbele ya hii jamii nafikiri ningeongea nikasikika nikarudisha huo mpango wa utangazalji wa HAKIELIMU lakini kutokana na SIRIKALI yetu hii inayojiita eti ya Kidemokrasia kuwa na meno makali na kucha zilizojaa damu ya kidikteta,ubadhirifu na uzindaki siwezi sema lolote wakalisikia na kulifanyia kazi.Rafiki yako Ndesajo huwa napitia blog yake ni mengi kwakweli anayasema yanafaa kufanyiwa kazi lakini ukirudi kwenye uhalisia,hakuna anayejali na angalau anahisi anatakiwa kuwajibika kwa hayo,yanayosemwa,INASIKITISHA.tumekuwa tunasema mambo tuu mengi tena sana,lakini cha kusikitisha na cha kakatisha tamaa hakuna anayewajibika..hii ni kwanini uanfikiri?jibu ni rahisi tu kila kiongozi anajiona yeye si muhusika wa jambo hilo husika anaona wapo wengi kwaiyo haimgusim yeye kama yeye,nachoshauri ni bora watanzania tungeanza kunyoosheana vidole tu wewe Bwaya umefanya hivi vibaya,au wewe Kikwete umefanya vile vibaya basi,bora hiwe ivyo nahisi inaweza ikasaidi,nahisi inaweza saidia.Kwaiyo Bwaya kwanza nakupongeza kwa hilo,pia nakushauri mwambie rafikoyo Ndesajo aitoe hiyo mada MWANANCHINI,ahsante mimi seba(www.wttz.blogspot.com)

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3