Kama sio utumwa ni nini hiki?
Habari za siku ndugu msomaji. Binafsi sijambo. Nafurahi kurejea kibarazani baada ya heka heka za huko na huko. Itoshe kuhusu mimi, nikukaribishe tena humu ndani. Leo ningependa kukusimulia kisa kimoja. Nikuase kwanza, kwamba usilazimike kunielewa vibaya. Sijawa na tabia ya kuona makosa zaidi niwapo mahali ama nikutanapo na watu. Maana siamini kwamba binadamu ana kazi ya kushabikia makosa kuliko jema moja. Nisijitetee sana. Jumapili hii nilipata fursa ya kuhudhuria ibada kwenye kanisa la 'kisomi'. Washirika wa kanisa hili, wengi wao ni wale ambao umande haukuwazuia kuhudhuria shule. Wamesoma. Pamoja na ukweli kwamba wote walikuwa weusi kama mimi, lakini ilikuwa bayana kwamba kiingereza kilikuwa 'nguzo' ya ibada hiyo. Hilo halikuwa tatizo kwangu. Maana inaeleweka kwa wengi wetu kwamba, kusoma kunathibitishwa na umahiri wa kusema kiingereza. Nshazoea hili. Pamoja na ukweli kwamba kiuhalisia kiswahili ndicho kinachotawala madarasani lakini watu hatutaki kuukubali ukweli...

Nasikia hata mtu asemaje KUFISADI aka KULIA OFISINI bado ni rahisi zaidi hata kwa mafisadi ambao kabla hawajadaka ofisi walikuwa hawafikirii UFISADI kama moja ya njia ya kuwa TAJIRI!:-(
JibuFutaKwani KUWA TAJIRI au tu tu GROW RICH ni nini kama utajiri moja ya tafsiri yake ni kuridhika tu na skonzi wakati keki zipo ingawa kuna aridhishwaye zaidi na MAANDAZI?
Loooh!! unakisoma kwa mara ya pili mkubwa??? ngoja nami nirejee maktabani nipekuepekua walau mawili matatu, maana ile NADHARIA YA CHANGE YOUR FREQUENCY inanikuna sana. Pamoja sana mkubwa katika kuliendekeza libeneke la kusoma vitabu. amani iwe nawe daima
JibuFutaKinachosikitisha ni jinsi wengi katika jamii yetu wanavyoamini kuwa mafanikio watayapata kwa njia za kishirikina, badala ya kuzingatia elimu inayopatikana vitabuni.
JibuFuta@Mkodo, Kufisidi ni tabia unayoweza kuibaini mapema tu.
JibuFuta@Marcus, nimefurahi kusikia umekisoma! Naomba pendekezo la unachokisoma hivi sasa.
@Profesa, pengine tumelelewa kishirikina.
Pesa unaipataje, unaweza ukaokota, ukiokota kuna kapoteza umadhulumu/fisidi. Ukaamua kufanya kazi, ukapata mshahara, je katika dhima nzima ya kufanya kazi hukuwahi kutega...lazima kutakuwepo na uzaifu fulani, umepata kitu/mshahara lakini ndani yake kuna ufisidi...au sio
JibuFutaUmefanya biashara, ukauaza na kupta faida kubwa, je hiyo faida ina uhalali , kuna kukwepa kodi, kuna kudanganya kuwa ni kizuri kumbe siku mbili tatu kibovu...umefisidi..
Lakini kuna ufisadi wa dhahii, mkubwa sana, unafisidi nchi nzima, mama yangu...hata yule asiyejiweza, hata yule asiye na baba wala mama, hata ....mungu wangu utasema nini mbele ya muumba!
Nimewaza tu mkuu!
@Emu three ufisadi, kwa kadri ya maelezo yako ni sehemu ya utamaduni. Je, twaweza kujinasua?
JibuFutaKinatakiwa kuwepo katika maktaba za shule na hasa zaidi katika ile ya Bunge la Tanganyika
JibuFuta