Pedagogy of the oppressedPaulo Freire katika sura ya pili ya kitabu chake "Pedagogy of the Oppressed" anazungumzia dhana inayosisimua anayoiita "the banking concept of education" kama chombo kinachotumika kuwakandamiza wanyonge. Kwamba katika hayo yanayoitwa madarasa, wapo waungwana wanaojichukulia kuwa wanajua, hulipwa kwa kuwajaza wenzao "elimu" ambayo kimsingi ni chombo cha kuwakandamiza raia wanaoonewa.

Freire anadhani hii si sawa kwa binadamu mwenzako kujiweka juu sana kiasi cha kuamua usome nini, na uache kipi (bila kujali mahitaji yako halisi). Anatoa mfano pale mwalimu anapoweza hata kupendekeza kwamba kitabu fulani kisomwe kuanzia ukurasa wa 10 hadi wa 15! Na eti anadhani anamsaidia mwanafunzi!

Kwa mujibu wa Freire, elimu hii haiwezi kumkomboa mnyonge.

Je, elimu yetu ina tofauti? Wanafunzi zaidi ya asilimia 50 "walishindwa" mtihani hivi majuzi, ni kweli walishindwa ama ni namna nyingine ya kuwakandamiza vijana wasio na hatia?

Maoni

 1. Bwana Bwaya, asante kwa kutukumbusha juu ya udhaifu wa SYSTEMS (???mitindo???) tunaotumia kwelimisha watoto wetu.


  Lakini mimi kutokana labda nakwamba sijasoma yakutosha mawazo ya akina [Paul Frere] nafikiri kwamba hata ikitumika falsafa gani katika elimu, hamna matokea mazuri kama


  MZAZI-TAJIRI

  Atampeleka nakwenda kumchukua kwa gari mtoto wake ikiwa nyumbani ni chini ya kilometa mbili kwenda shuleni. Mtoto apate lini mazoezi ambao tiyari tunajua yasadia kumwongeza mtoto akili?

  MZAZI-MASKINI

  Ataendelea kumshawishi mtoto wake kwa kila kitu "sukari katika chai, sukari katika uji, na pipi kula sana ukiwa na hela mwanangu" wakati huku tumekwishaambiwa waziwazi sukari jinsi tunavyotumia inamadhara yake katika ubongo na jinsi akili inavyofanya kazi hasa kwa watoto (TEENAGERS).  Kiujumla nasema: embu tujitulize kidogo juu ya uchunguzi wa shule, walimu au Wizara zetu! Wacha tuangalie sasa WALIMU WAKWANZA WA MTOTO YOTE YULE NA TUULIZE: "JE, MTOTO SISI KAMA WAZAZI NA WALIMU WAKE WA KWANZA TUNAMJENGEA MAZINGIRA NA DESTURI NZURI KIAKILI ILI ATAKAPOFIKA SHULENI RASMI YUKO TAYARI KUJIFUNZA ZAIDI? AU TUNAFIKIRI JENGO LA SHULE NI TIBA KIBOKO HATA TUKIWA SISI WAZAZI TUMEMHARIBU NAMNA GANI MTOTO KIAKILI"?

  JibuFuta
 2. Umeniwazisha na bado nawaza!:-(

  JibuFuta
 3. Idd Simba aliwahi kusema wasomi wetu hawawezi kujifikirisha kwa kuwa walikosa lishe bora utotoni.Je hii haiwezi kuwa sababu ya vijana wetu wa kidato cha nne kufanya vibaya?

  JibuFuta
 4. @Ndugu Phiri, hoja zako zinaelimisha. Tatizo linaweza kuwa pana kuliko tunavyofikiri. Kwamba hata mazingira ya nyumbani yanachangia kuvia kwa akili za watoto. Kumbe badala ya kuilaumu tu serikali na walimu, ni vyema na busara zaidi kuchunguza namna tunavyowalea wanetu hovyo hovyo.

  @Kitururu, kuwaza ni sehemu muhimu ya maisha ya mwenye busara.


  @Anony, inawezekana lishe nayo ni tatizo! Kufeli kunaonekana kutokana na sababu nyingi nyingi nyingi. Ipo haja ya kuzipitia sababu hizi kwa utulivu.

  JibuFuta
 5. simple one of the best books i have read. even the style of narration is simple and straight

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Pay $900? I quit blogging