Wangapi huzitazama tabia zetu kwa jicho la mabadiliko?

Mwanzo wa mwaka huwa na matumaini tofauti na wakati mwingine wowote wa mwaka. Ni wakati ambapo watu hujisaili, na kutazama wanakoelekea kwa mwaka unaoanza. Ni wakati ambapo watu hujipanga namna ya kupiga hatua katika maeneo muhimu ya kimaisha.

Hata hivyo, ni wangapi wetu huweka maazimio ya kubadili tabia zetu? Ni wangapi wetu tunao uwezo wa kuzitazama tabia zetu kwa jicho dhati la mabadiliko?

Kwa mfano. kuamua kwamba mwaka huu ninapambana na tatizo la kutokusoma? Kuamua kwamba siwezi kuendelea kuwa mtu nijuaye kusoma lakini sisomi?

Ni wangapi wetu hisia hizo za matumaini mapya tunazokuwazo mwanzo wa mwaka, huishia kwa matumaini yayo hayo mwisho wa mwaka?
Kwa nini malengo mengi huishia kuwa malengo ya mwaka unaofuata? Kwa nini watu wengi humaliza mwaka kwa masikitiko –wakati wanapojikuta na hali ile ile ama mbaya zaidi ifikapo mwisho wa mwaka?

Kumbuka uamuzi wa kufanya badiliko dogo, ambao unauhakika wa kuendelea nao kwa miezi kumi na miwili, ni wa muhimu kuliko kufanya maamuzi kumi yatakayoishia katikati ya mwaka.

Kuendelea kukumbuka azimio kwa hisia zile zile ulizokuwa nazo siku ulipoliweka, ni hatua muhimu katika kutekeleza.

Niendelee kukutakia mafanikio kwa mwaka mpya!

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Pay $900? I quit blogging