Padre karugendo na mijadala ya Imani


Kitabu hiki nilikisoma mara ya kwanza mwaka jana. Yeye mwenyewe alinielekeza mahali pa kukipata baada ya kuwa amesoma mjadala uliomhusu kwenye blogu hii baada ya kusemekana kuwa Padre Karugendo alikuwa "amevuliwa" upadre.
Nilijifunza mengi kuhusu dini.

Pengine unaweza kujiuliza; Kwa nini aliandika kitabu hiki?

Pamoja na kukieleza kisa kizima kilichosababisha yeye "kufutwa" upadre kupitia tangazo la gazetini, Padre Karugendo anasema katika uk. 22: "...lengo zima la kutafakari kwangu na kukushirikisha wewe msomaji, ni kutaka kujenga utamaduni kama ule wa kule zilikotoka dini hizi za kigeni. Utamaduni wa kuamini kitu unachokifahamu vizuri, unachokitafakari, kinachogusa maisha yako ya jana, leo na kesho. Imani inayojenga historia yetu - historia ya Mungu na watu wake wa taifa la Tanzania!"

Pamoja na hilo, Padre karugendo anasema kwa sauti kubwa kabisa kwamba, "Si haki Maaskofu kukemea ufisadi ndani ya serikali na kuacha ufisadi unaoendelea ndani ya makanisa yao. Mtu anayekumbatia matendo ya kifisadi hawezi kukemea ufisadi. Ni lazima kanisa lijisafishe kwanza, ndipo liweze kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya jamii yetu."

Kimechapishwa na Shule & Company (2009) na kinauzwa kwa bei ya Tsh 4500. Kipate ukisome, kisha utafakari kimya kimya!

Maoni

  1. Mara nyingi ukweli unauma, na wale waliokalia kiti hawapendi kuambiwa kuwa kiti walichokalia kimelegea kinaweza kikamwangusha, ..kwanini hawataki huo ukweli, kwasababu wanachelea kuwa wakiondoka, watakalia wengine, na huenda wakakitengeneza hicho kiti vyema na wasipate tena nafasii ya kukikalia!
    Imani za dini zipo wazi, ila waliojaliwa kuzisoma, wanakuwa `wachoyo' hasa linapokuja swala la udadisi ili kujua zaidi `kwanini...'!
    Sijui kwanini waogope kujibu hilo swali `kwasababu'...ndio hiyoo ya kuogopa kuwa kiti kitatengenezwa na ukweli utadhihiri...na mwisho wa siku...!
    Hongera sana mkuu kwa kuwa msomi na huna uchoyo wa kuwaeleza wengine nini umekisoma na kimekusaidiaje na kitasaidiaje wengine...hiyo ndiyo elimu na huo ndio usomi.
    Ukisoma ukajua , ukabakia na elimu yako kichwani, bado kuna mashaka na elimu yako, lakini kama umesoma na ukiitumia elimu yako kwa faida yako na kwa wenzako pia, hayo ndiyo matunda ya elimu na huo kwangu mimi nauona kama ndio `usomi'

    JibuFuta
  2. Asante sana, Mkuu, kwa mijadala kama uliotuletea leo.

    NAMNUKUU PADRE KARUGENDO: "Si haki Maaskofu kukemea ufisadi ndani ya serikali na kuacha ufisadi unaoendelea ndani ya makanisa yao..."


    SWALI LA MANYANYA PHIRI: Anajuaje yeye Padre kwamba wanaacha kukemea ufisadi unaoendelea ndani ya makanisa yao?


    Pili: Hata wakiwa wanakemea kila siku, yeye Padre anafikiri kweli itakuja hiyo siku wakati wote wale watenda-dhambi waliojumuika kanisani za maAskofu ila kusafishwa na damu ya Yesu wawe wasafi siku moja kwa kila mmoja wao?


    Kama hiyo siku haitakuja [mpaka Yesu mwenyewe kurudi], waanze lini sasa Maaskofu kukosoa serikali zetu ikiwa Tanzania, Afrika Kusini au nchi yoyote ile duniani?


    Mimi binafsi sipendi dini ingawaje naikubali na vile kuiheshimu; lakini ninachokana ni mambo yasiyokua na mawazo yenye kueleweka kama alivyonukuliwa yule Padre... (THE PADRE'S LOGIC IS BANKRUPT).

    JibuFuta
  3. good article, thanks for sharing

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?

Pay $900? I quit blogging