Ninachokisoma sasa...

Maoni

  1. naona umedhamiria kuwa BIG. sie wengine tutapenda kutafsiriwa kwa vitendo. kila la heri katika kuchota maarifa.

    JibuFuta
  2. Hiki ni kitabu maarufu kimojawapo ambacho nilikumbanaa nacho huku ughaibuni miaka michache iliyopita. Ni kati ya vitabu vinavyohamasisha mtazamo wa maisha ambao ungepaswa uwemo katika vichwa vya watoto wetu, vijana wetu, na wengine kwa ujumla.

    Kitu kimoja kinachosikitisha katika jamii ya waTanzania ni hii dhana ya kukata tamaa. Utasikia, kwa mfano, eti vijana wetu, wanakaa vijiweni, wanavuta bangi, na kadhalika eti kwa sababu wamekata tamaa.

    Wangesoma vitabu kama hivi, wangekuwa na mtazamo tofauti. Tatizo jingine ni uongozi. Angalia huku Marekani, kwa mfano. Hata kama nchi inakabiliwa na matatizo makubwa kiasi gani, utamsikia Rais Obama akitoa hotuba ya kuwatia watu moyo sana.

    JibuFuta
  3. Kusoma kuzuri jamani...nini kama elimu katika `mtizamo, malengo na mafanikio?' sijui. Elimu haiji kwa kuongea tu, ...`kusoma'
    Soma, kila kitu , soma mpaka macho yapofuke kwa maandishi, kwani mwisho wa siku utajua jinsi gani ya kuyatibu hayo machoo yasipofuke!

    JibuFuta
  4. @Mwaipopo, napenda kujifunza zaidi maarifa ya nafsi (kujielewa, kujisaili upya, kujenga upya mitazamo, kuona nisichokiona na kadhalika). Nayapenda sana maandiko yenye mtazamo huo wa mabadiliko binafsi kwa kuamini kuwa hatuwezi kuibadili jamii bila kwanza kubadilika sisi wenyewe.

    JibuFuta
  5. @Yasinta, karibu sana!
    @Profesa asante kwa mchango wa uzoefu wako. Kuna umuhimu wa kubadili mitazamo hasa katika umri wa mtu kama mimi.

    @M3, mafanikio ni nini? maana vyovyote iwavyo sote twapenda kufanikiwa. Mafanikio huanzia kwenye mtazamo. Namna tunavyoyatazama mambo. Kusoma ni hatua ya kwanza. Ya pili, hufuata baada yake.

    Wataalamu wa elimu hudai, elimu huja vyema sana kwa kuongea. Unapoongea kile ukijuacho, unajifunza zaidi. Kisha utekelezaji unafuatia. Tusiache kujifunza.

    JibuFuta
  6. Namuunga mkono Prof Mbele kwa asilimia mia moja

    JibuFuta
  7. Aisha S.Rubama22/4/11 10:55 AM

    hongera sana kaka, kwani umeendelea...maendeleo yanaanza kwenye mtazamo, mtu anaelewa nini? uelewa wa mtu ndio silaha pekee ya kumtoa kwenye magumu yake...lakini uelewa unakuja kwa kusoma vitabu na hali nzima ya mtazamo wa upokeaji(human acceptance.nawasihi watanzania wenzangu tubadilike kwenye mtazamo mzima kuhusu maisha ndio mwanzo wa maendeleo...tujielewe(tuko wapi)tujitambue (sisi ni kina nani)tujifahamu(tunatakiwa kufanya nini kwa wakati gani)....hapo ndio tutaendelea...asanteni

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Mbinu za Kujenga Ujuzi wa Mwanafunzi