Kama tulivyoona katika makala yajuma lililopita , usaili ni hatua ya mwisho kuelekea kupata kazi. Sehemu kubwa ya usaili ni maswali na majibu yanayolenga kupima uwezo wako wa kukabiliana na changamoto halisi za kazi. Ingawa yapo maswali yanayoweza kukupa wasiwasi wa nia ya mwuulizaji, fahamu kuwa hakuna swali linaulizwa kwa nia mbaya au kwa bahati mbaya. Kila swali linaloulizwa linalenga kutafuta uthibitisho kuwa wewe ni mtu sahihi kwa kazi unayoomba.
WANAUME wengi wanaamini wanawake, kwa kawaida, ‘wanapenda hela.’ Kwamba ukiweza kumhakikishia mwanamke 'uhakika wa kiuchumi' unakuwa umemaliza. Ingawa hatuwezi kupuuza ukweli kuwa uhakika wa 'kiuchumi' ni moja wapo ya mahitaji ya mwanamke, lakini si sahihi kuamini kuwa moyo wa mwanamke unaweza kuthamanishwa kwa fedha. Fikra hizi walizonazo wanaume [kuwa anachokihitaji mwanamke ni fedha] zimeleta matatizo mengi katika mahusiano na ndoa. Kwa mfano, wapo wanaume ambao baada ya kuhakikisha wenzi wao wamepata mahitaji ya msingi, basi wanawatelekeza kihisia. Hali hii husababisha upweke mkubwa kwa wanawake hawa wanaojikuta hawana mtu wa karibu kuwasikiliza isipokuwa vitu.
SAIKOLOJIA, neno lililotoholewa kutoka neno la kiingereza psychology, si elimu inayoeleweka sana katika jamii yetu. Asili ya 'psychology' ni neno 'psyche' lenye maana ya nafsi. Katika makala haya, tunasaili kwa ufupi maana ya saikolojia kama taaluma na kuonesha nafasi ya taaluma hiyo ngeni katika jamii yetu katika kutatua matatizo ya kijamii na hivyo kuharakisha juhudi za watu kujiletea maendeleo yetu.
PICHA: thesouthern.com Siku moja nikiwa kwenye maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanafunzi wa shahada za awali waliingia kufanya mtihani wa muhula wa mwisho wa masomo. Wakati wanaingia, mmoja wao alijigamba kwamba hiyo ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kukanyaga maktaba tangu amejiunga na chuo hicho miaka mitatu iliyopita. Nilishangaa inawezekanaje mwanafunzi wa chuo kikuu kujisifia jambo la fedheha kama hilo.
Sipendi kutumia kiingereza kwa sababu kwanza ninadhani kiswahili kinanitosha kabisa kuelezea kile ninachotaka kusema. Hata hivyo najua pia matumizi ya kiswahili chetu hayajawa katika kiwango kile kilichokusudiwa. Kuna maneno mengi yasiyoeleweka vizuri katika kiswahili cha kitabuni. Moja wapo ya maneno hayo ni hili ninalolitumia leo hii. Haiba. Pengine niweke msisitizo kwa faida ya wale wasiolifahamu neno hili vizuri. Personality. Wengine wanasema maana ya hichi kinachoitwa personality ni utu kwa kiswahili. Ni bahati mbaya kwamba niliyakimbia masomo ya lugha siku nyingi. Ila nimejiridhisha kwamba haiba ndiyo tafsiri muafaka kabisa. Haiba ni nini? Watu wengine watafikiria tunazungumzia mwonekano wa mtu kimavazi. Lakini haiba ni neno pana zaidi ya mwonekano wa mtu kwa nje. Haiba ni jumla ya tabia za mtu zinazotokana na kile anachofikiri, anachopenda, anavyojichukulia yeye mwenyewe, anavyowachukulia watu wengine na kadhalika. Haya yote hujenga mwonekano wa mtu unaopimika (tabia) kama vi...
PICHA: Daily Maverick Moja wapo ya sababu nyingi zinazowasukuma wazazi kuwapeleka watoto wadogo kusoma shule za bweni ni mafanikio ya taaluma. Mazingira ya shule yanaaminiwa kuwa bora zaidi katika kuwasaidia watoto kufanya vizuri zaidi kuliko wanapokuwa nyumbani.
PICHA: Shutterstock Nakumbuka siku ya kwanza kusikia neno ‘cell’ nikiwa kidato cha kwanza haikuwa kazi rahisi kupata picha kamili. Mwalimu wetu aliandika ubaoni, ‘ cell is a basic unit of life .’ Niliduwaa. Sikujua anamaanisha nini zaidi ya kutazama kamusi kujua maana ya maneno aliyoyatumia. Mwalimu alirudia maneno hayo hayo kuweka msisitizo, na kisha akatafsiri kwa Kiswahili. Alisema, ‘maana yake ni hivi kuna kitu kidogo kisichoonekana kwa macho kwenye miili yetu kinachofanya tuishi. Mmeelewa?’ Kwa kweli hatukuwa na namna nyingine zaidi ya ‘kuelewa’ na tukaitikia, ‘ndiyo!’
waswahili walinena, "Ukiona kobe kainama ujue anatunga sheria"
JibuFutaMchoko wa Dowans.....
JibuFutaMoja ya Mtazamo:
JibuFutaWamevaa suti nzuri kweli !:-(
Duuh, heri mimisijasema...!
JibuFutaHivi Waziri Mzima unapolala kwenye mkutano (ambao nauli na per Di Em inalipwa kwa kodi za wananchi) pembeni kabisa mwa bosi wako maana yake nini?
JibuFutaNaunga mkono usemi wa Mwaipopo.
JibuFutaakitoka hapo anasaini mkataba......yaliyomo sasa utajiju
JibuFuta