Wafilipino Wauliza ‘Rais Yuko Wapi?’ Wakati wa Majanga ya Kitaifa?

"RETWEET if you think PNoy should've attended the arrival of honors instead of that Car Plant event. #NasaanAngPangulo" tweets @BobOngWords.  
"TWITI TENA kama unadhani PNoy alipaswa kuhudhuria mapokezi ya heshima badala ya tukio la Kiwanda cha Magari. #NasaanAngPangulo" alitwiti @BobOngWords.

Alama habari #NasaanAngPangulo, yenye maana 'Rais yuko wapi' katika lugha ya Kitagalog, ilikuwa mada maarufu zaidi kwenye mtandao wa Twita duniani wakati Wafilipino walipokuwa wakionesha hasira zao kwa Rais Noynoy Aquino kufuatia  kukosekana kwake kwenye mapokezi ya heshima ya miili ya polisi waliouawa wakiwa kwenye operesheni maalum.

Aquino alihudhuria kuzinduliwa kwa kiwanda kipya cha magari cha kampuni ya Mitsubishi huko Laguna (jimbo lililo kusini mwa Manila) badala ya kuhudhuria mapokezi ya miili ya polisi. Majeneza yaliyobeba mabaki ya miili ya polisi hao yaliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Villamor baada ya kusafirishwa kutoka Mamasapano, mji ulio kusini mwa Ufilipino, Maguindanao.

Askari arobaini na wanne wa Jeshi la Polisi la Ufilipino - Kikosi Maalum (PNP-SAF) waliuawa kwenye operesheni ya kupambana na ugaidi mapambano yaliyochukua masaa 11 kati ya vikosi vya serikali na waasi wa Moro wanaotaka kujitenga na wanaofanya shughuli zao kwenye eneo la Mamasapano.

Marehemu hao walikuwa sehemu ya askari 400 waliokuwa wametumwa kumkamata mtu anayedaiwa kupanga matukio ya milipuko ya mabomu ya Bali mwaka 2002 anayesemekana kujificha eneo hilo. Serikali ya Marekani ilitoa kiasi cha dola za Marekani milioni tano kama zawadi kwa atakayetoa taarifa zitakazowezesha kumkamata mtuhumiwa Zulkifli bin Hir alias Marwan.

Mfululizo wa ujumbe uliokuwa ukienea kwa kasi kudhihaki kukosekana kwa Rais Aquino kwenye mapokezi hayo ulizunguka kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na Twita.

Wafilipino watumiao mitandao walikumbushana namna Rais Aquino alivyokuwa mwepesi kutoa muda wake kuhudhuria shughuli za zinazoandaliwa na makampuni makubwa wakati akikosekana kwenye majanga mengi makubwa yaliyoliathiri taifa.

Wengine walikumbushia jinsi rais alivyowahi kusema, "Sihudhurii shughuli za watu nisiowajua" alipoulizwa kwa nini hakuhudhuria maziko ya Jennifer Laude, aliyedaiwa kuuawa na mfanyakazi wa Marekani mwaka uliopita.

Mwandishi Katrina Stuart-Santiago alijaribu kufananisha umuhimu unaooneshwa na wakuu wengine wa nchi kwenye kutoa heshima zao kwa watu wanaoolifia taifa na kutokuonekana kwa rais Aquino kwenye mapokezi ya mashujaa hao kwenye bandiko lake la Facebook:
Wakati miili ya waathirika wa ndege ya MH17 ilipowasili nchini Uholanzi, Mfalme wa nchi hiyo Willem-Alexander na Malkia Maxima, na pamoja na familia karibu yote ya kifalme, wakiambatana na maafisa wa serikali walikaa na kutazama na kulia na kuomboleza na taifa wakati majeneza yaliposhushwa kutoka kwenye ndege. Hakuna kilichokuwa muhimu zaidi ya kuwaenzi marehemu hao.

Rais Aquino alitoa hotuba wakati ibada ya mazishi ya polisi waliouawa  siku moja baada ya majeneza kuwasili. Lakini wakati huo kwa mara nyingine alisemekana kuchelewa na kufanya shughuli zingoje mpaka atakapowasili.

Hotuba ya Aquino wakati wa ibada hiyo iligeuka kuwa kituko mtandaoni kwa kusemekana kuzungumzia mambo yake binafsi kuliko marehemu. Utani uliokuwa ukisambaa mtandaoni ulionesha namna Aquino huanza hotuba yake kwa maneno ya George Lucas wa Star Wars.

Msemaji wa rais ametetea kutokuwepo kwa rais katika mapokezi ya miili ya polisi, akisema kwamba hiyo haikuwa sehemu ya ratiba yake. Pia alikejeli wakosoaji wake mtandao kwenye taarifa yake Ikulu, akisema kwamba ukosoaji huo ni mtazamo usiowakilisha maoni ya wengi.

Iliandikwa awali kwenye tovuti ya Global Voices.

Maoni

 1. Interesting article and I Banget Fill It Love
  Fraternal greetings from our.

  obat aborsi

  obat telat bulan

  jual obat aborsi

  JibuFuta
 2. PROMO DELIMA
  poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

  Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
  Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

  Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
  Livechat_____: delimapoker
  BBM__________: 7B960959
  Facebook_____: delimapoker
  Phone number_: +85595678845
  pendaftaran___

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3