Kwa nini watu hatutulii kwenye fani tulizonazo?

Kwa nini watu wengi hutumia sehemu kubwa ya maisha yao kumangamanga huku na huko, wakibadili kazi na shughuli kutoka ofisi moja kwenda nyingine?

Inakuwaje kijana aliyesoma kuwa mtaalamu wa kilimo, hataki kabisa kufanya kazi ya kilimo aliyoisomea na badala yake anatafuta kazi itakayompeleka mbali zaidi na kilimo?

Kwa nini mwalimu haridhiki na chaguo lake la awali la kutokotosha fikra za wanafunzi, na badala yake anatumia sehemu kubwa ya maisha yake kutafuta namna ya kuchomoka afanye kazi zisizohusiana na ualimu?

Tunatafsiri vipi kitendo cha daktari aliyesomea utabibu kwa miaka isiyopungua mitano, katika mazingira magumu ambayo hatma yake yanamfanya awatumikie wananchi wenzake kwa kuokoa maisha yao, anaachane na utabibu ili kuwa mwanasiasa wa majukwaani?

Ninachojiuliza ni hiki: Kwa nini hatutulii kwenye taaluma zetu? Kwa nini hatuzitumii taaluma tulizonazo ambazo zimetupotezea miaka kibao kuzipata? Je, ni aina ya elimu tunayopata? Je, tafsiri ya mafanikio tuliyokuzwa nayo tangu tukiwa wadogo ndiyo mzizi wa mahangaiko haya yote?
Mafanikio ni nini? Kuwa tajiri? Kuwa maarufu? Na uoza wa ufisadi uliotapaa kwa kila familia hivi sasa, si matokeo ya tafsiri ya mafanikio tuliyokuzwa nayo?

Si ajabu kuwa wengi tunazaliwa halisi (orijino) ila twafa tukiwa nakala tu (copy). Na hapo ndipo lilipolalia janga la kitaifa.

Maoni

 1. Hili swali ndiotunajiuliza sana, mie nimepoteza baadhi ya jamaa katika fani yangu na wameingia kupiga talalila za siasa.

  JibuFuta
 2. http://lnfaw.blogspot.com/

  JibuFuta
 3. Cha kwanza kabisa ni maslahi. Hiki ni kichocheo kikubwa kabisa. Maslahi hufikiriwa hata kabla mtu hajaingia kwenye fani husika.

  Kingine ni mfumo wa elimu. Hapa Tanzania mathalani, mfumo wetu wa elimu haumwandai mwanafunzi ktk fani mbalimbali kulingana na wito. Mara nyingi tunaangalia combination gani imebalance, then mtu anachepukia huko huko.
  Unakuta mtu anakipaji cha kuwa dactari lakini kwa bahati mbaya kwenye mtihani wa mwisho kulingana na mazingira ya mtihani, akafeli mtihani wa biology, ndio hivyo tena, atakuwa ameukosa wito kwa kiasi kikubwa, na kinachobaki ni kuangalia wapi palipo-balance. Baadae mtu huyu huyu akihangaika ktk kuutafuta udactari na kuikacha fani ya awali, basi atawekwa kwenye kundi la wakimbia fani, kumbe ndio anaitafuta fani iliyo kwenye damu.

  JibuFuta
 4. Bw. Bwaya. Swali lako ni zuri, japo watu wanaokimbiakimbia fani zao za awali si wengi kihivyo.

  Tunachokosa nchini Tanzania katika mfumo wa elimu ni kuwa na mtu anayeitwa 'Career Guide'. Huyu, kama alivyo mtu mwingine yeyote aliyesomea kazi ya kutoa ushauri ... hana budi kumwongoza kijana tangu awali akitazama mwenendo wake, vipawa vyake na uwezo wake darasani na nje ya darasa. Mtu wa aina hii hatuna katika mfumo wetu wa elimu. Kwa hiyo, watu wengi tunajiendea tu kiupofu upofu, matokeo yake ndiyo kama havyo ... leo mtu ni daktari kesho yuko kwenye siasa ... kesho kutwa keshabadilisha vyama zaidi ya vitatu vya siasa ... mwishowe tunabaki kuwa na nchi ya wasomi... lakini wasio efficient ... leo tuna maPhD holders kibao ... lakini ufanisi katika utendaji kazi mbalimbali ni wa viwango vya chini kuliko hata vile vilivyokuwepo kabla ya uhuru ambapo hatukuwa na maPhD holders wengi. Shame.

  JibuFuta
 5. Ni ulevi tu hakuna kingine

  JibuFuta
 6. wewe hakuna mtu ambaye amezaliwa na fani fulani mi nafikiri ni sahijhi kamawewe unaona uchungu sdana nenda ukasome ushughulikie nao na sio kuwalazimisha wenzako hiyo ni caree development baba

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Pay $900? I quit blogging

Fumbo mfumbie mwerevu