Hivi kama watu mnapendwa na wananchi, mabango haya yote ya kazi gani? Kama kweli ninyi ni chaguo la wananchi, inakuwaje mnatumia mapesa mengi hivi kuwashawishi wananchi hao hao?
i dont think km ugonjwa ndio sela.huyo mtu kaishiwa sela ndio maana kasema hivyo isijekuwa ukienda kumpima yeye ataoneka mgonjwa kuliko huyo anayemsema.
Mimi natafakali sana, hivi kama mimi nimefanya kazi ipasavyo kwa kutimiza ahadi zangu, kuna haja gani la kutumia nguvu na ahadi mpya nyingi huku mabango makubwa yakiuuza sura!!! Wewe tulia tumia nguvu kidogo kwa kuwa umelitumikia taifa kwa miaka mitano kwa mafanikio.
Padre Karugendo ameandika haya (kwenye Tanzania Daima) kumhusu huyo jamaa kwenye hilo bango
Naandika kutoa ushauri na hasa maoni yangu ambayo ni ya nia njema kwa taifa letu la Tanzania.
Hii ni aina ya barua ya wazi kwa wale wanaotamani kuendelea kutawala wakati miaka ya kustaafu inakaribia. Labda kuna haja ya kuongeza miaka hii ya kustaafu. Miaka sitini ya sasa watu wanakuwa bado wana nguvu na kutaka kuendelea kutumika au kula “utamu” wa uongozi.
Hakuna haja ya kusubiri kuzomewa na kugomewa hadi kufikia hatua ya kukulazimisha kujitoa. Hakuna haja ya kusubiri kufanyiwa maandamano na vikao vya kukujadili kama unafaa au hapana. Ni kweli kwamba Watanzania ni wasahaulifu; wengine hawakumbuki yaliyotendeka jana.
Lakini si kweli kwamba wote ni wasahaulifu; wachache hao wanatosha kuchochea moto kiasi cha kukufanya kujuta ni kwa nini hukujikalia kimya na kufanya mambo yako.
Vidonda bado ni vibichi, hata watoto wadogo bado wanaimba Richmond na wengine kwenda mbali na kuibatiza Rich Monduli. Atakaye kuambia hili limesahaulika, atakuwa hakupendi.
Kwa vile umekubalika kwa mzee wa kimila, tosheka! Washauri na kuwaelekeza ndugu zako huko na kuingia kwenye mtandao wa wazee mashuhuri ndani ya taifa letu.
Nakubali kabisa kwamba tulifurahi pamoja, tukadhalilishwa, tukaonewa na kusikitika pamoja, sasa tusonge mbele: Ushindi ni wetu! Sina matatizo na hili. Na kama ushindi wenyewe unalenga kumhudumia Mtanzania na kumsaidia kupiga hatua kuelekea maendeleo;
Kama hautakuwa ushindi wa kujilipiza kisasi, kuchota rasilimali kiasi cha kutosha na kuwatajirisha marafiki, ndugu na jamaa. Labda mimi ningesema hivi: Tulifurahi pamoja, tukadhalilishwa, tukaonewa na kusikitika pamoja, sasa tupumzike!
Tusifikiri kwamba bila sisi hakuna kitakachofanyika. Tutoke kwenye ndoto na malengo haya ya kutaka kufika tulikolenga miaka mingi bila ya mafanikio. Sote tuna malengo, lakini si yote yanafanikiwa.
Hata hivyo tunamshukuru Mungu, na kutosheka pale tulipo! Hata wale waliostaafu na kupumzika wana mchango mkubwa katika kuliendesha taifa letu la Tanzania. Si lazima mtu uwe rais, waziri, waziri mkuu au spika wa Bunge, ndio utoe mchango wa maana.
Binafsi ningeifanya kauli mbiu hii mpya iwe hivi:Tulifurahi pamoja, tulisikitika pamoja na sasa tusonge mbele hadi ushindi, na kuishi ya maisha ya hekima, busara na ushauri zaidi ya kuwa kauli mbiu ya siasa za kiwendawazimu.
Siasa zisizo soma alama za nyakati na kukubali mabadiliko yaliyosukwa na Vision, historia na bidii ya kufanya mabadiliko hayo; siasa za ili liende, heshima na utukufu na kuendelea kuutukuza umasikini kana kwamba sisi tuliumbwa tumelaaniwa.
Kaulimbiu mpya inahitaji watu wapya, mazingira mapya na ‘vision' mpya inayochimbuka ndani ya historia ya Taifa letu; historia inayokusuta pale unapotaka kujichanganya kuendeleza ndoto zako zisizo tekelezeka.
Lakini pia ni muhimu kwamba wale unaotaka au kutamani kuwaongoza wakukubali na kukupenda vinginevyo, itakutesa wewe na kuwatesa wale unaotamani kuwaongoza.
Mwezi wa tano ndio huu. Tarehe mbili leo. Kama ulikuwa hujapanga cha kufanya mwezi huu, ndugu, hujachelewa. ( Si unajua haipendezi kufanya chochote bila kupanga?) Tabia ya kusubiri mwisho wa mwaka ndio tuanze kufikiri kupanga mipango mingi ya mwaka mzima ( ambayo hata hivyo haitekelezeki) si nzuri sana. Nakukumbusha mipango yako ya mwaka huu: Ulipanga kufanya nini mwaka huu? Je, umefikia walau nusu ya mipango yako? Una mikakati gani na mwezi huu wa tano? Nusu ya mwaka ndo inayoyoma! Nakukumbusha kutafakari upya mambo yako mwaka huu, uone wapi umefanikiwa na wapi unahitaji kujipanga vyema zaidi. Nakukumbusha kutafakari changamoto ulizokumbana nazo katika sehemu ya kwanza ya mwaka huu, na ufikiri namna ya kukabiliana nazo vizuri zaidi kwa nusu iliyobaki. Na unapofanya hivyo, usiache kupitia hapa kuanzia juma hili kwa ajili ya vipande vya saikolojia na falsafa za kutafakari pamoja namna ya kujielewa. Niwatakieni wanablogu wote heri ya mwezi mpya wenye mafanikio (pamoja na uki...
Wiki hii mimi na familia yangu tulikuwa na kikao cha ‘halmashauri kuu’ ya mwaka. Kikao chenyewe kililenga kujitathmini sisi kama familia na kujiwekea malengo ya pamoja kwa mwaka 2023. Kikao hiki kinatarajiwa kufuatiwa na kikao cha 'Kamati Kuu.' Maandalizi ya kikao hiki cha 'banguabongo' yalifanyika kwa kupeana dondoo za kufanyia kazi agenda za kikao. Hatimaye siku ikawadia. Jioni ya Jumapili ya Desemba 25, 2022. Tukiwa eneo tulivu mbali nyumbani, baada ya mwenyekiti wa kikao kueleza kwa nini tumekutana, shughuli yenyewe ikaanza. Agenda ya kwanza ilisomwa na mtoto wetu wa kwanza, “Kitu gani ulichofanya mwaka huu kinakufanya ujisikie fahari?” Tukatakiwa kuandika kwenye vikaratasi vidogo tulivyokuwa tumegawiwa tayari. “Tumieni vikaratasi vya kijani. Mambo matano makubwa yaliyokufanya ukajisikia fahari kwa mwaka huu.” Baada ya kila mmoja kuorodhesha mambo yake matano yaliyomwendea vyema mwaka huu, mtoto wa pili akakusanya vikaratasi vyenye majibu na kuvibandika kwenye u...
WANAUME wengi wanaamini wanawake, kwa kawaida, ‘wanapenda hela.’ Kwamba ukiweza kumhakikishia mwanamke 'uhakika wa kiuchumi' unakuwa umemaliza. Ingawa hatuwezi kupuuza ukweli kuwa uhakika wa 'kiuchumi' ni moja wapo ya mahitaji ya mwanamke, lakini si sahihi kuamini kuwa moyo wa mwanamke unaweza kuthamanishwa kwa fedha. Fikra hizi walizonazo wanaume [kuwa anachokihitaji mwanamke ni fedha] zimeleta matatizo mengi katika mahusiano na ndoa. Kwa mfano, wapo wanaume ambao baada ya kuhakikisha wenzi wao wamepata mahitaji ya msingi, basi wanawatelekeza kihisia. Hali hii husababisha upweke mkubwa kwa wanawake hawa wanaojikuta hawana mtu wa karibu kuwasikiliza isipokuwa vitu.
WANAUME wengi wanapenda kuoa wanawake wanaowazidi sana umri. Ni nadra kukutana na mwanaume aliyezidiwa umri na mke wake. Kama hiyo haitoshi, wanaume wengi wanapenda kuoa wanawake wenye elimu ndogo zaidi yao. Ushahidi ni wewe unayesoma hapa. Ha ha haaha! Vilevile, wanaume wengi wanapenda kama ingewezekana, basi wapate wanawake watakaowategemea wao kiuchumi. Au wawe na ujira mdogo kuwazidi wao. Ni mara chache sana imekuwa kinyume. Swali: Je, hizi si dalili za kutokujiamini? Je, huu si ushahidi kwamba wanaume ni dhaifu, ndio maana wanatafuta mbinu za kujihami?
Haya ni maoni ya mdau asiyependa jina lake lijulikane. Nimeyatundika hapa kwa sababu ya uzito wa anachokisema. Tafadhali soma na kama unaweza changia maoni yako tuelimike. Nimshukuru sana kwa kutumia muda wake kuandika maoni yake na hapa namnukuu: MAKANISA ya Kikristo yanafunza ya kuwa Yesu Kristo si kama kuwa ni Mwana wa Mungu tu, bali hakika ni Mungu khasa. Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni mmoja. Watatu katika mmoja, na mmoja katika watatu. Wote ni wa milele, wote ni sawa. Yesu ni Mungu, na Mungu ni Yesu. Hiyo ni imani ya Kikristo, ambayo inaaminiwa na karibu Wakristo wote. Hebu tuifunue Biblia tutazame inasema nini katika jambo hili? Mt Paulo katika barua yake ya kwanza kuwapelekea Wakorintho aliandika: Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi. 1 Wakorintho 15.15 Juu ya kuwa Paulo anaambiwa ya kuwa akiamini kuwa Masihi (yaani Kristo) na Mwenyezi Mungu ni ki...
Unaweza kushangaa lakini ndio ukweli wenyewe kwamba upo uwezekano mkubwa kabisa wa kuanzisha na kuendeleza mahusiano na mtu yeyote bila kujali mwonekano wake, tabia yake na imani yake. Katika makala haya tunaeleza kanuni za kimaumbile zinazoongoza mahusiano ya watu wawili ambao mara nyingi watu hao hukutana kwa njia ya nasibu.
Kuna kitu ambacho huwa ninajiuliza kila mara, hivi mimi sura yangu ni ipi? Huwezi ukakubali kwa haraka hadi utakapojifanyia uchunguzi ndipo utakapogundua hauna sura moja. Unapokuwa unaongea na mpenzi wako unakuwa na sura gani? Unapokuwa unaongea na wazazi wako unakuwa na sura gani? Unapokuwa umefurahi unakuwa na sura gani? Unapokuwa umekasirika unakuwa nasura gani? Unapoongea na bosi wako Je? Unapoandika email au kuchangia maoni je? Haya ni maswali ambayo huwa ninajiuliza mara kwa mara. Je sura yangu ni ipi na nifanye nini ili niijue sura yangu halisi? (c) Nuru Shabani, 2009
i dont think km ugonjwa ndio sela.huyo mtu kaishiwa sela ndio maana kasema hivyo isijekuwa ukienda kumpima yeye ataoneka mgonjwa kuliko huyo anayemsema.
JibuFutaMimi natafakali sana, hivi kama mimi nimefanya kazi ipasavyo kwa kutimiza ahadi zangu, kuna haja gani la kutumia nguvu na ahadi mpya nyingi huku mabango makubwa yakiuuza sura!!! Wewe tulia tumia nguvu kidogo kwa kuwa umelitumikia taifa kwa miaka mitano kwa mafanikio.
JibuFutaMpondela, hawawezi kutulia wanajua wakitulia imekula kwao.
JibuFutaPadre Karugendo ameandika haya (kwenye Tanzania Daima) kumhusu huyo jamaa kwenye hilo bango
JibuFutaNaandika kutoa ushauri na hasa maoni yangu ambayo ni ya nia njema kwa taifa letu la Tanzania.