Kwa nini wewe tena Oktoba hii?


Unatusumbua!
Kadiri siku zinavyosonga wajikomba sa-na
Salaamu mpaka unaboa!
Eti ‘mmeamkaje wapenzi wangu niwapendao…’
Fataki mkubwa wewe!
Ulikuwa wapi siku zote?
Kisa cha kumsalimia mtu barabarani?
Umejua maana yetu eh?
Hivi hukutujua siku za nyuma?
Unadhani tumesahau…


Sikia,
Tunakumbuka nyodo zako mara chache ulizokuja
Tunakumbuka kauli zako za maudhi
Eti sie wako tu iwe isiwe
Tukupe tusikupe haikusumbui
Ukasema hata ukiwa kule sie wa hapa ni wako
Sasa babu sikiliza
Mwaka huu ni wa hapa hapa


Wote ‘twajua huna uumini wowote
Unatafutaga nini kipindi hiki?
Ni hivi hivi tu waja majisidi?
Wenzio ‘twaswali weye unadipu
Kisa? Eti ule mpango wa mlo huko nje
Unachekesha…
Yaani mie mwenye njaa nikulishe wewe unayebeua!
Yaani unitumie fasta, kama kondomu sina maana tena?
Umesahau ulivyotufanyia siku zile?
Tumekupa ukala ukaondoka?
Shukrani yako sitasahau: vumbi la fo wili mjini
Kama hunijui vile…
Nashangaa umenirudia tena
Jua mapema Imekula kwako

Kwanza hatukujui umetokea wapi
Huna ulichoandikaga kutupa mwanga wa maisha yako
Tukujueje?
Mbona wenzako wanaandika?
Mbona wenzako hawakimbii maduka ya vitabu?
Hivi kazi yako haihusiani na vitabu tena?
Vitabu na mlo wako havihusiani?
Au ndio utamaduni wetu labda eh!
Kwamba hata ukindika hakuna wa kusoma?
Na’mashaka
Mbona hata kuongea huongei?
Na ukitaka kuongea unachagua wa kuongea nae! 
Kwa nini?


Hivi ninahitaji kuwa mzee na ajuza kuwa hadhira yako?
Sema tu nielewe!
Mpaka niwe na uwezo wa kukushangilia?
Ingekuwa poa kama ungekuja na “milimani”
Si imekuwa mingi siku hizi?
Kazi yake nini kama ‘wapaogopa?
Aende nani kama sio wewe?
Swahiba wanitia shaka
Weye wataka wajinga eeh?
Uwaaminishe kila kitu ‘afu wao makofi mfululizo
Kisa, hawajui kufikiri wala kuuliza
Sasa jielimishe: hatuliwi tena babu


Mbona kila ukipata fursa huitumii?
Kila songombingo mpaka ushinikizwe
Ukinikizwa watufanyia maigizo
Mnachopangilia mle ndani ni mshazari wa haya ya nje
Leo huyu kesho yule
Wapi bwana…ya Kaole haya
Mbona swahiba wajidai humwoni?
Kila siku eti ajali yam lo
Una bahati bongo kila mtu na lwake
Hata umwage pumba barabarani…
…kesho “ah, mzee jana alikuwa anatania”
Na kweli yanaisha
Ubwabwa wapumbaza kula
Kanga fulana ongeza kopo la mbege…
Miaka mitano unayo
Hii ndiyo bongo bwana
Kila mtu na lwake
Kila mtu na ufukara wake


Lakini kwani jamani?
Ukikaribia uchaguzi “…aah sipigi kura mie…”
Kura moja itabadili nini?”
Tunakomoa gari kwa kulisukuma tukiwa ndani sio!
Mnaboa, mnachosha, mnakera
Nimemaliza

Maoni

  1. Umenena kaka!

    Waambiye wajue utamu wa kuwa ndumilakuwili na kutojitambua/kutotambua tamani na sababu ya wao kuwa duniani!!!!!

    JibuFuta
  2. Kaka naona umeshuka mistari kama ya Siti Binti Saad....LOL

    No.... nadhani itakuwa ni kama ya Shaaban Robert

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Makundi Manne ya Tabia za Watoto Kitabia

Uislamu ulianza lini?