Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 2

Katika makala yaliyopita tuliona maeneo manne muhimu ya kuzingatia unapoingia kwenye usaili. Kwamba pamoja na maswali mengine, unaweza kuulizwa maswali kuhusu uzoefu wako wa kikazi huko ulikotoka. Tuliona kuwa unapoulizwa maswali kama hayo, lengo ni kupima namna unavyoweza kuwa mkweli.

Usikimbilie kumponda mwajiri wako wa zamani kwa kutoa sababu za kutokuridhika na mshahara, migogoro ya kazi uliyokuwa na mwajiri wako, kutokuelewana na wakubwa wako wa kazi au watu uliokuwa unawasimia.Ukifanya hivyo utaonekana wewe ni mtu wa matatizo.

Badala yake, toa sababu chanya zinazoleta picha ya mtu mkomavu kazini. Mfano, unaweza kuonesha kuwa uliacha kazi uliyokuwa nayo kwa sababu ulipata fursa ya kutumia vipaji vyako vizuri zaidi kwingineko, au kwamba  kazi uliyoipata ingekupa kukua kiujuzi zaidi.

Katika makala haya, tutatazama maeneo mengine manne unayohitaji kujiandaa ili kushinda maswali utakayoulizwa kwa mafanikio.
 
PICHA: moving2canada.com
Matarajio yako kwa mwajiri

‘Unadhani tukulipe mshahara kiasi gani?’

Hili swali linatafuta kujua vipaumbele vyako uwapo kazini. Ni kweli unatafuta kazi ili upate fedha uboreshe maisha yako. Lakini kuonesha kuwa ari na kujituma kwako kazini kunategemea na kiasi cha pesa unacholipwa ni kosa la kiufundi. Kosa hili linaweza kuwa kikwazo cha kukupa kazi.

Unahitaji kuonesha ukomavu kwa kuelewa kuwa taasisi bora [kama hiyo unayotaka ikuajiri] zina utaratibu rasmi wa kuwalipa wafanyakazi wake. Mtu hulipwa kwa sifa alizonazo. Kwa uelewa huo, utapata alama za ziada.

Hata hivyo, pamoja na majibu hayo wapo wasaili wanaweza kukubana uwaambie matarajio yako. Fahamu kuwa kujadili mshahara wa kazi ambayo bado hauna uhakika nayo, haiwezi kukusaidia.

Ikiwa utalazimika kutaja tarakimu, inatarajiwa kuwa tayari utakuwa umeshafanya utafiti wa taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na viwango vya mishahara. Taja kiwango ambacho hakitaonesha huna thamani, lakini pia usitaje kiwango kitakachoonesha kujikweza kupita kiasi.

Uelewa wa mambo na ujuzi wa kazi

Unaweza kuulizwa maswali yanayopima uelewa wako wa kawaida kwa mambo yanayofahamika. Lakini pia unaweza kuulizwa masuala ya moja kwa moja yanayohusiana na kazi unayoomba.

Wakati mwingine, baadhi ya wasaili hutumia mtihani wa kuandika kujaribu kuthibitisha kama kweli una uwezo na ujuzi uliouonesha kwenye wasifu wa kazi.

Maswali yanayoulizwa yanaweza kupima moja kwa moja utaalam uliousomea darasani au namna unavyoweza kutatua changamoto halisi za kazi. Jiandae ipasavyo kwenye maeneo muhimu.

Kilicho muhimu ni namna unavyoweza kutafsiri nadharia zako katika mazingira ya kazi.
Kwa mfano, unaomba kazi ya uhasibu msaili mmoja anakuuliza, ‘Chukulia ofisini kwako kumetokea wizi wa fedha. Utachukua hatua gani?’ Au unaomba kazi inayohusika na utawala, ‘Chukulia kama kiongozi umesikia wafanyakazi wa chini yako wana mpango wa kugoma. Utafanyaje?’

Hayo ni maswali ya uchokozi. Usitumie muda mrefu kutafuta masuluhisho yasiyokuwepo. Jibu kwa ujasiri kuwa hutarajii kuwa matatizo ya namna hiyo yatajitokeza. Lengo ni kuonesha una uwezo wa kuikinga taasisi yako na changamoto kama hizo.


Malengo yako ya baadae

‘Unajiona ukifanya nini baada ya miaka 10 ijayo?’
‘Una malengo gani ndani ya miaka mitano ijayo?’
Hapa unahitajika kuonesha ari ya kukua kiujuzi na kiweledi. Ongelea mipango ya kujifunza zaidi kufikia kwenye malengo makubwa yanayoendana na malengo mapana ya kitaasisi. Kuzungumzia malengo yasiyoendana na kazi unayoomba kutakupunguzia alama.

 ‘Umeomba kazi kwingine?’
Wanahitaji kuwa na uhakika na maamuzi yako. Ni kweli inawezekana utakuwa umeomba kazi maeneo mengine. Lakini utaonekana mkomavu ukiweza kuonesha kuwa kazi hii unayosailiwa ndio chaguo la kwanza.

‘Utafanya kazi na sisi kwa muda gani?’
Hapa wanataka kujua kama wewe ni mpitaji au la. Inawezekana kweli unaweza kuwa na mpango wa kufanya kazi kwa muda mfupi na utafute njia nyingine.

Lakini kuonesha wazi kuwa unapita wakati hata kazi hujapata si busara. Onesha ungependa kufanya kazi kwa muda mrefu kadri utakavyohitajika.

‘Unaota kufanya kazi gani nzuri baadae?’
Ukitaja kazi nyingine mbali na hiyo unayoomba, unaleta wasiwasi kuwa hutaridhika na kazi unayoomba. Ongelea mazingira ya kazi bila kutaja kazi mahususi. Mfano, kazi inayokufanya utumie vipaji vyako na ujuzi ulionao. Kazi inayokufanya ukue kiujuzi na kiuzoefu.

‘Uko tayari kuanza kazi lini?’
 Kama huna kazi, ukisema uko tayari kuanza kazi mara moja inaonesha utayari ulionao. Lakini kama unabadilisha kazi, kuonesha utahitaji muda mfupi wa kukamilisha taratibu za kukabidhi majukumu uliyonayo na kuaga itakupa alama.

Fursa ya kuuliza swali

Kwa kawaida, baada ya kuulizwa maswali mengi,  kikao cha usaili kitahitimishwa kwa kukukaribisha kuuliza swali. Kama tulivyosema, kila swali lina maana. Unapoulizwa, ‘Je, una swali ungependa kuuliza?’ lengo ni kutaka kujua ulivyo na ari ya kufanya kazi na taasisi hiyo.

Usipouliza swali lolote, maana yake ama huna uelewa wa mambo mengi au huna ari ya kutosha. Uliza swali kuhusu taasisi hiyo. Waliuze wanatarajia nini kwa mtu atakaye pata kazi hiyo. Kadhalika, waweza kuulizia mambo yanayohusiana na fursa wanazoweza kutoa kukuza ujuzi wako kama mfanyakazi wao.


Epuka kuuliza maswali ya kimaslahi. Kuuliza, ‘Mnanilipa bei gani?’ ni kuonesha huna mtazamo mpana na kazi. Unaweza hata usijibiwe au ukajibiwa jibu litakalokunyong’onyeza. 

Maoni

 1. thanks for your sharing. i think this article must be share to other people.
  GALERIQQ.COM

  JibuFuta
 2. Yuk Buruan ikutan bermain di website http://sahabatpoker.poker
  Sekarang SAHABATPOKER Memiliki Game terbaru Dan Ternama loh...
  => Bonus Refferal 15%
  => Bonus Turn Over 0,5%
  => Minimal Depo 20.000
  => Minimal WD 20.000
  => 100% Member Asli
  => Pelayanan DP & WD 24 jam
  => Livechat Kami 24 Jam Online
  => Bisa Dimainkan Di Hp Android
  => Di Layani Dengan 5 Bank Terbaik
  Ayo gabung sekarang juga hanya dengan
  mengklick Poker Online
  PIN BB : 2B13CFDA

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Pay $900? I quit blogging