Inaanza na wewe...

TUMEKUWA maarufu kwa kuwalaumu watu wa mabara mengine kwa umasikini wetu. Tunatumia muda mwingi kuorodhesha visingizio.

Kwamba ni ukoloni ndio umeyatenda yote haya, huo ndio umekuwa wimbo wa kurithisha vizazi na vizazi.

Sitetei wakoloni. Lakini hebu na tufikiri. Kama matatizo yetu yanauhusiano na ukoloni huo, mbona, miaka hamsini baada ya kile kinachoitwa uhuru, hali imebaki pale pale?

Kama kweli umasikini wetu una harufu ya ukoloni, mbona leo hii, tunausomba ukwasi tulionao kuupeleka ughaibuni? Halafu baadae tunaufuata huko huko kwa jina la misaada ya hisani? Linaelezekaje hili?

Miaka hamsini ya kujitawala, bado waafrika weusi hawataki lugha zao. Wanafundishana mambo ya hao wanaowalaani kwa lugha za hao hao! Wanaongea wao kwa wao kwa lugha za kuazima!

Ndugu zangu, sababu ya umasikini wetu ni akili zetu.

Maoni

  1. Bwaya; ukisoma "msahafu" wa Walter Rodney - How Europe Underdeveloped Africa - utaziona hoja nzito kuhusu jinsi Afrika ilivyosikinishwa na Ulaya. Na kama ulivyosema, ni kweli walitusikinisha nasi tukawatajirisha. Lakini tutatumia kisingizio hiki mpaka lini? Hata ufisadi, uzembe, ukosefu wa uongozi imara tuendelee tu kuwalaumu wao? Bill Cosby aliwasha moto hapa Marekani alipowaambia weusi wenzake kwamba wakati sasa ulikuwa umefika wa kuacha kuwalaumu wazungu kwa madhambi ya utumwa waliyowatendea na kujibidisha katika elimu na malezi bora ya watoto wao. Hata sisi nadhani wakati umeshafika wa kuacha kulaumu ukoloni kwa kila kitu. Matatizo yetu mengi ya leo ni "self-inflicted"

    Suala la lugha (kwa vile ndiyo uwanja wangu hasa) pamoja na mchakato mzima wa elimu yetu ni jambo la kusikitisha sana. Niligusia kidogo jambo hili katika makala yangu mojawapo katika gazeti la Kwanza Jamii na unaweza kuisoma hapa: http://matondo.blogspot.com/2009/04/tutatukuza-vya-wengine-na-kudharau-vya.html

    JibuFuta
  2. Tanzania ni nchi tajiri saaaana! Wananchi wake tuliowengi ni masikini.

    Uzalendo babaaa! Uzalendo hakuna kabisa!

    Hata sisi wenyewe tunaukaribisha umasikini. Mtu anafanya kazi na kukusanya kiasi fulani cha pesa, anazitumia kwa starehe, kesho anaamka akiwa hana kitu.Anakwenda kutafuta tena na mchezo ni ule ule.

    Kanuni ya HIARI na LAZIMA mtu haijui kabisa.

    JibuFuta
  3. Mimi sina cha kuchangia hapa,ila tupo pamoja.

    JibuFuta
  4. fred katawa1/6/09 8:34 PM

    Bwaya sijakupata vizuri unaposema hali ni ile ile yaani ya leo na miaka 50 iliyopita.

    Mimi naona mabadiliko yapo tena makubwa.Miaka ya 60 nchi ilikuwa haina mafisadi lkn leo wamejaa tele.

    Nchi ilikuwa haina vibaka lkn leo kila unayekutana naye anaweza kuwa kibaka au tapeli.

    Kulikuwa na makanisa machache sana labda hayakuzidi kumi.Leo kila baada ya nyumba tatu kuna kanisa na yote yameleta habari za wokovu na upendo kutoka Israel ingawa waumini hawapendani wao kwa wao.

    Tuna ghala za mabomu ya kutosha toka nchi zilizoendelea.
    Nchi ina mashangingi ya bei kubwa yasiyopungua 800.

    Posho ya mbunge kutwa ni 135,000 na mshahara wa mwalimu kwa mwezi 130,000.

    Kiongozi mkuu anaweza akasafiri mara tatu kwa mwaka kwenda Ulaya na Marekani kumsalimu mkuu mwenzake huku akiongozana na watu wasiopungua ishirini,halafu bwaya unasema tuko pale pale?

    JibuFuta
  5. Mzima Bwaya?

    Sijui mengi kuhusu Tanzania kwa hivyo sitaingilia mjadala wa umasikini :D
    Nitakalo sema ni kuhusu lugha... siku hizi 'globalization' imetufanya tusahau kidogo lugha zisizozungumuzwa na wengi... tunazidi kuwa kama jamii moja kubwa na inabidi kuelewana, tuwafuate wengi. Sio kumaanisha tusahau lugha zetu, ila afadhali kujifunza nyingi panapo uwezekano.
    Ni hayo tu.

    JibuFuta
  6. Naam ndiyo maana naandaa kitabu, nimeshaandika muswada wangu tulieni niwe hai.

    SWALI: NCHI ZILIZOENDELEA MAANA YAKE NINI? NCHI ZINAZOENDELEAA MAANA YAKE NINI? KAMA ZIMEENDELEA KWANI WANAKWAMUA?

    JE AFRIKA ITAENDELEA? JE TUNAJUA KUNA MAENDELEAO YA VITU NA MAENDELEO YA WATU? KAMA POSHO NI MAENDELEO YA VITU, KWANINI WASILETE MAENDELEO YA WATU?

    JE AFRIKA HATUJAENDELEA?

    JibuFuta
  7. Kaka Bwaya u mzima kwani sasa kimya kimezidi twakumiss.

    JibuFuta
  8. Nimependa maoni ya wadau,sababu nyingine ambayo nimekuwa nikiiona kwetu sisi huwa ni unyimi wa habari tulionao wenyewe kwa wenyewe.Ile tabia ya kutopenda kumfaidisha mwenzako imetufanya tubakie nyuma SANA. Mfano...utakuta mtu amefanikiwa ktk kitu fulani au nafanya kazi fulani ukimuuliza kafanya vipi au naifanyaje kazi hiyo atakupiga chenga mpaka utakata tamaa.Mpaka tukibadilisha mitazamo yetu vinginevyo wenzetu wataendelea kwenda Mars na sayari nyingine sie bado tunatambaa na kulaumu .

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Pay $900? I quit blogging

Heri ya mwezi mpya!