Fujo huanzishwa na 'wenyenguvu' si wanyonge

Hakuna mahali katika historia (labda niambiwe vingine) panapoonesha kuwa matumizi ya nguvu - mapigano na vita, huanzishwa na wanyonge.

Ni hivyo kwa sababu wao wenyewe (wanyonge) ni matokeo ya ' maguvu' ya wenye nguvu. Ni hivyo kwa sababu pasingelikuwapo watu wanaoitwa wanyonge, bila hao wanaojiona wana nguvu kuzidi binadamu wenzao, wenye haki kama wao.

Hivyo, mapigano huanzishwa na mabwana wakubwa wao wenyewe, kwa kiburi chao cha kugoma kuwatambua na kuwasikiliza wenzao kama binadamu pia. Mapigano huwa hayaanzishwi na wale wanaoonewa, wanaonyonywa na wasiotambuliwa na kuheshimiwa.

Wasiopendwa huwa hawasababishi chuki, bali wale wasiopenda wenzao ambao hujipenda wao wenyewe. Si wasiojiweza - waathirika wakuu wa ugaidi - huweza hata kufikiri kuanzisha ugaidi, bali wenye maguvu ambao hutumia maguvu hayo kupunja haki za wenzao kwa kuwahesababu kama watu wawezao kuondoshewa uhai wao wakati wowote ule. Si waliodharauliwa huweza kuanzisha visasi, bali wale wenye dharau wenyewe. Si wale ambao utu wao unakanwa hudharau wenzao, bali wale wasiojali utu wa wenzao.

Hata kama kuna mahali inaonekana kama vile wanyonge huanzisha mapigano na mfumo fulani, tunachotaka kusema hapa ni kwamba, mapigano hayo huwa yameanzishwa na wenye nguvu wenyewe. Je, mwenye nguvu apishwe azidi kuonea, kunyanyasa na kudharau wenzake kwa sababu ya maguvu yake?

Mchana mwema.

Maoni

 1. Vita, utumwa duniani ya hivi karibuni ilianzishwa na wajeuri. Hebu soma jeuri yao. Kisha elimisha.
  Kumbuka kaka wataalamu wa dunia hii ni hatari. Utadhani kuwa ubadhilifu na ufisadi wote uko hapo tza tu, lakini ukweli ni kwamba umeenea kote. Waenezao haya ni wachache tu duniani. Na haya yalianza zamani.
  Ingia website hizi uone.
  http://judicial-inc.biz/slave_traders_.htm,
  http://judicial-inc.biz/b.lood_diamonds.htm,
  http://judicial-inc.biz/J_oran_va_der_sloot_supplement.htm,
  http://judicial-inc.biz/thersea_heinz_kerry_bio.htm,
  http://judicial-inc.biz/1.osephardim_of_curacao.htm,
  http://judicial-inc.biz/j_history_caribbean_jews.htm,
  http://www.blacksandjews.com/Jews.of.Black.Holocaust.ag.html,
  http://sunray22b.net/slavery.htm,
  www.jewwatch.com, www.erichufschmid.net, www.iamthewitness.com, www.prothink.org.

  JibuFuta
 2. Asante kwa viunganishi. Kuna mengi ya kujifunza ambayo naona ninahitaji kujifunza zaidi.

  Nashukuru kuwa na wasomaji wanaoelimisha kama wewe. Karibu tena!

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mbinu za Kumfundisha Mtoto Kusoma Akiwa Nyumbani

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Fumbo mfumbie mwerevu

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)