Wacha CNN watudhalilishe...!

Sijui kwako. Huenda hili halikusumbui na pengine kinachonishangaza mimi hakina uzito stahiki kwako.

Lakini binafsi huwa najisikia fedheha Afrika inapotangwa vibaya na vyombo vya magharibi vikiongozwa na CNN.

Pamoja na kulaani ushabiki mbaya unaofanywa na vyombo hivyo, bado kuna kila dalili kwamba huenda tunavyotangazwa ndivyo tulivyo. Hebu tuone mifano michache.

Inakuwaje anapopita mzungu, watoto mtaa mzima wanachokikumbuka cha kwanza ni '...mzshungu naomba hela...'?
Tumewaleaje wanetu? Kwamba ipo ngozi yenye kumaanisha hela kuliko nyingine?

Na hii si kwa watoto tu, hata watu wazima wenye elimu kubwa, wanapokutana na rafiki wa kizungu, kwao hiyo ni fursa muhimu ya kutengeneza fedha. Rafiki mzungu ni 'dili' uswahilini na ukionekana una ukiongozana naye watu wanakuona 'umeula'. Nenda Moshi na Arusha uone waswahili tunavyojidhalilisha. Jamaa wanawalazimisha wazungu kununua kitu wasichokitaka kwa kiingereza cha kuunga-unga na kamba. Mzungu wa watu ataghasiwa na kusukwasukwa kisa kuna watu wanamwabudu!

Unapohitaji huduma mahali, kwa mwafrika mwenzio, akatokea mzungu mahali hapo, anayesikilizwa zaidi huwa ni yule mzungu. Nini maana yake?

Kwa nini inaonekana kila kilichokizuri ni cha kizungu? Ukitunza muda, unaitwa mzungu. Ukiishi shaghala baghala unaitwa mswahili. Je, hii si ni kusema kwamba kila kilicho cha hovyo ni 'uswahili'?

Tunasubiri nani atuheshimu kama sisi wenyewe hatujikubali? Tunapojidharau wenyewe, halafu tukatarajia wengine watuheshimu, tunakuwa wanafiki. Tunakuwa tunajidanganya wenyewe.

Haianzii CNN. Inaanzia kichwani kwako!

Maoni

 1. Jamani kuna haka kamchezo wa kuigiza aliwahi,nimeupata kutoka katika iliyokuwa blogu ya Ndesanjo Macha.Nimeuweka bila idhini yake ila nadhani nitakuwa sijakosea kwa umuhimuhimu wa hii mada itasaidia

  SEHEMU YA KWANZA:
  Mchina mfupi, mdogo kwa umbo, na sura yake kama paka anaonekana anamkimbiza Mtanzania. Mtanzania anakimbia kwa mbio zake zote huku anageukageuka nyuma kuangalia kama atadakwa. Mchina anaongeza kasi. Mtanzania maskini wa MUNGU kasi inapungua kadri anavyozidi kukimbia. Hatimaye Mchina anamkamata Mtanzania.
  Wakati huo huo wa kumkimbiza Watanzania wengine wanakimbilia nyuma. Siyo kwamba wanakimbilia kumdhibiti Mchina isipokuwa wanakimbilia kuona kibano atakachopewa Mtanzania na Mchina.

  SEHEMU YA PILI:
  Mchina kamkamata mwizi wake (Mtanzania). Wote wawili wanahema kwa nguvu kwa sababu ya kukimbia. Mchina anamkunja shati Mtanzania. Watanzania wengine wamefika kwenye tukio wanasubiri kuona cha mtema kuni atakachokipata Mtanzania mwenzao. Mchina anaanza shughuli ya kumuadabisha Mtanzania kwa vibao. Kwa kila kibao anachopokea Mtanzania analia "..mama!.." "..ang'i!.." "..mama!.."
  Wakati huo Watanzania wengine wanashabikia "..Kula eeeh.." "..kula eeeh.." "..k...mae wallai Wachina siyo mchezo cheki anavyopiga kunfuu.." Mchina anaona anaumiza mkono wake kwa sababu jamaa ni sugu sana anachukua chuma anaanza kumbonda nalo kichwani kama anaua nyoka. Mtanzania damu zinamchuruzika kwa majeraha. Watanzania wengine wanaacha kuangalia wengine wanaangalia huku wakisema "..Mchina akikasirika hatari.." "..hawa jamaa huwa hawaongei lakini 'usiwauzi'..Maanake wakikasirika jasho litakutoka.." Mchina anaendelea kubonda kichwa na nondo. Paa la uso linapasuka. Mtanzania sasa halii tena bali anaguna tu kila pigo la nondo likitua "..mmgh.." Pigo jingine "..mmmgh.." na jingine tena "..mmgh.." na jingine tena "..mmgh.." na jingine tena hakuna sauti inayotoka Mtanzania kishapoteza fahamu. Mikono, viatu na nguo za Mchina vimetapakaa damu ya Mtanzania. Mchina anamuangalia mtuhumiwa wake anaridhika na kisago alichompa.

  ONYESHO LA TATU
  Mchina na wenziye wanachumpa ndani ya gari yao kwenda kunawa na kubadilisha nguo. Watanzania waliokuwepo kwenye tukio wanaondoka wasije wakakutwa na polisi wakatakiwa kutoa ushahidi. "..haroo, yaani yule Mchina arikuwa kakasirika bwana..Maanake arikuwa anampiga kwa nguvu kama nini.." "..Mshikaji tukijikate mandata wasije wakatukuta hapa tukaitwa kwenye ushahidi.." "..Lakini jamaa kajitakia mwenyewe sasa kwa nini aliiba?.." ".unajua mimi nilianza kuwaona tangu wanamkimbiza, nikajua tu leo jamaa ataipata.." "..Hivi arifikiri anaweza kumshinda mbio Mchina..Wachina wanafanya mazoezi ware tangu wadogo.." "..Mimi nirikuwaga nawaonaga wakati wanajenga reri ya tazala, tujamaa tudogo rakini tunabeba mataruma ya reli kama kanabeba rura ya kupigia mistari.."

  ONYESHO LA NNE
  Mtanzania mmoja mzalendo aliyekereheshwa na kitendo kizima anakwenda kuita polisi baada ya tukio kuisha. Polisi wanakuja na mwandishi wa habari mmoja. Polisi wanampinduapindua maiti. Halafu wanawaamrisha watu "..Hebu sogeeni mbali mnatunyima nafasi.." Polisi mmoja anachapa chapa virungu watu wanasogea mbali kidogo. Wengi wa watazamaji wa tukio ni wanaume vijana na watoto wadogo. Watoto wengine wanamtazama maiti huku macho yamewatoka kama wanatazama sinema ya dracula. Polisi wanampindua marehemu kutoa kitambulisho mfukoni ili kumjua jina lake. Kwa bahati nzuri ana kitambulisho. Wamemtambua jina. Halafu wanampasia mwandishi wa habari kitambulisho. Mwandishi anachukua jina halafu anamrudishia ofisa. Maiti anaokotwa anawekwa nyuma ya Land Rover anapelekwa hospitali. Watanzania wanatawanyika. Eneo la tukio linaachwa na damu halafu polisi wamesahau kuokota nondo iliyotumika kumpigia marehemu. Msamaria mwema anaiokota anaitupa jalalani huku akisema "..Isije ikaua mwingine.."

  MWISHO
  Mchina anapigiwa simu aende kituoni akatoe maelezo ya tukio. Kituo yupo ofisa upelelezi kesi za jinai. Kiingereza chake siyo kizuri sana kwa hiyo stetimenti ataiandika Kopla Masanja kwa sababu anaongea Kiingereza kizuri zaidi. Mchina anafika kituoni masaa kadhaa baada ya tukio. Stetimenti inaandikwa. Mchina anaambiwa itabidi alale ndani jioni ya leo. Baada ya siku mbili tatu suala linakuwa kati ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Ubalozi wa China nchini Tanzania. Kwa sababu za kidiplomasia Mchina anakuwa 'dipotedi' Kesi imekwisha.

  Watanzania hivi sivyo inavyokuwa? Kama nimekosea kutengeneza onyesho niambieni! Sawa?

  JibuFuta
 2. Swala la muhimu unalozungumuzia Bwaya. Lazima tujiheshimu... mbona ukiwa uzunguni wasimamishwa foleni na wala huishwi njia maanake umgeni?

  JibuFuta
 3. Daima huwa nafika Tanzania na wazungu ambao ni wanafunzi wangu. Suala hili unaloliongelea linajitokeza. Mwaka juzi, kwa mfano, tukiwa kwenye hoteli ya kitalii katika hifadhi ya Tarangire, mhudumu mmoja, Mtanzania, alinijia na kuniuliza kama mimi ndio dreva wa wale wazungu. Kazi tunayo.

  JibuFuta
 4. @Nuru asante kwa nukuu murua ya Ndesanjo.

  @Serina ni kweli tunahitaji kujitambua.

  @Profesa Mbele karibu sana kwenye ukurasa huu. Inafedhehesha kwamba mwanafunzi mweupe anaweza kupandishwa hadhi zaidi ya Profesa wake eti kwa sababu ni mweusi. Tuikatae hali hii kwa kubadili 'mind-set' za wanetu.

  JibuFuta
 5. DUH!
  ya Prof. Mbele ni makubwa, pole sana mkuu.
  tunahitaji juhudi kubwa kujikwamua kutoka katika huu utumwa wa kiakili.

  JibuFuta
 6. Hii yote inatokana na malezi mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.kaka Bwaya na wengine wote ni kweli kuwa pamoja na mzungu "Afrika" Tanzania ni usumbufu sana. Kwa sababu hapo watu wanafikiri wewe pia ni mzungu na wanataka hela nk. Tusipowahi sasa kuirekebisha kizazihiki basi na kizazi kijacho kitafikiri vivyo hivyo. ni hayo tu

  JibuFuta
 7. ndo upuuzi nilioukemea kule kwa mbele na kwa yasinta wa kwenda utumwani a.k.a uzunguni, wakaona kila kitu ni bora tuige kwa sababu tu kafanya mudhungu!!!!

  ndio wasomi wetu kutoka ulaya wanaokuja wakimbariki mzungu na upuuzi wake wote kisa? aliwasomesha na nawalisha.

  hii huanzia mbali sana sio bure washikaji. ndo yaleee hutumwa.

  eti yasinta na mbele wanashangaa pia. mamaaaaaaaaa

  JibuFuta
 8. Kamala wewe na mbele na yasinta'why?'

  JibuFuta
 9. Mie nafikiri malezi bora,elimu na kuwafundisha wanetu kuwa unaweza ukafikia ngazi uitakayo ukifanya bidii toka wakiwa wadogo ili wakiona mtu kama Prof. na wanafunzi wake wajue inawezekana yeye kuwa kiongozi wa msafara (Pole Prof.).Pia tuwe mifano bora kwa maneno na matendo maana watoto hujifunza KWANZA toka kwa wazazi na pia kwa jinsi hiyo utaaminika na utaheshimika.
  Pia tujaribu kupanuka kimawazo kuona kuwa kila mtu anaweza kitu fulani kwa mfano kuna watu wanatend kufikiri kuwa wasichana hawawezi kujitegemea wakajijengea maisha mazuri wenyewe!,siku moja mtu alishawahi kubisha hodi nyumbani kwangu na swali la kwanza alilouliza ni mzee nimemkuta?Nikamwambia Mzee ndio mimi.Inabidi tubadilike!
  Mwisho kaka yangu Kamala mie nafikiri kuishi Ulaya sio utumwa ni sawa na kuishi Dar,Mwanza Mtwara au Bukoba wakati kwenu ni Tanga,Moro au Kigoma.
  Kaka Bwaya kazi nzuri!

  JibuFuta
 10. @ Kamala kwa nini unafikiri Yasinta na Profesa Mbele wanashangaa ulichosema?

  @ Sophie karibu sana. Nimecheka sana ulipomjibu huyo mgeni "...mzee ndio mimi!...". Ni kweli kwamba tunahitaji kubadilika.

  JibuFuta
 11. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

  JibuFuta
 12. Prof Mbele kumbe nawe unaweza kumuongezea mtu maisha kwa kumsababishia kicheko. Nimeupenda mfano wako ni rahisi na wa ukweli. Kweli wewe ni mwalimu!

  JibuFuta
 13. Ni kweli kabisa Bwaya na wachangiaji waliotangulia, hali inatisha. Nakumbuka kuna siku BBC walifanya coverage ya dada zetu ambao wana wapenzi wa kizungu au walioolewa na wazungu na wengi walikuwa mombasa na Dar es salaam, ilisikitisha kusikia wakisema kwamba wanadhalilika sana "lakini sasa watafanyaje na wanataka kuondokana na umaskini!" Jamani, tuna kazi. na kama tunashtuka sasa basi hili tulifanyie kazi ya ziada.Nawasilisha.

  JibuFuta
 14. Play Casino tyuueooru
  http://stonewalljacksoncarnival.org/ - Casino Bonus
  3.
  [url=http://stonewalljacksoncarnival.org/]Casino Game[/url]
  You can enjoy online casino simply by getting connected to the Internet.
  Casino Gambling Game
  2.

  JibuFuta
 15. Free Online Casino tyuueooru
  http://stonewalljacksoncarnival.org/ - Best Casino
  So you can have a wonderful gambling experience with the comfort at your home.
  [url=http://stonewalljacksoncarnival.org/]Free Casino Play[/url]
  There are several advantages of playing online casino and some of them include: 1.
  Casino Gambling
  It?s obviously due the comfort and easiness arriving with the online casino that many people, at present, are choosing to stick with online casino rather the traditional land-based casinos.

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Pay $900? I quit blogging