Nani hushaurika kikweli kweli?

Kila mtu anayo misimamo na imani ambayo kwayo huiishi. Misimamo hii ambayo kimsingi ni falsafa, hujengeka kadiri tukuavyo kulingana na aina ya watu na matukio tunayokumbana nayo.

Falsafa hizi ndizo hutawala namna tunavyoishi na watu, tunavyoyachukulia mawazo yao na hata namna tunavyojichukulia sisi wenyewe.

Inasemekana, katika umri fulani wa makuzi, falsafa hizi huwa hazibadiliki tena. Tunaposhauriwa jambo, kwa mfano, kabla ya kulikubali, hulipambanisha na falsafa zetu. Ikiwa litashahabiana, hulipokea/assimilate na ikiwa litapingana na falsafa zetu, hulipuuza.

Ndio maana kabla hujajitosa kumshauri mtu lolote, chunguza falsafa yake kwanza. Vinginevyo utakuwa unateketeza muda wako bure kumpa 'vidonge vyake' wakati ni wazi hatavielewa hata kama ni kweli unaweza kuwa sahihi kuliko yeye kwa vigezo vyako.

Kimsingi, watu huwa hawashauriki, ila hutafuta kuungwa mkono kile wanachowaza.

Maoni

 1. Nakubaliana nawe hasa wazazi ila sio wote, sijajua bado kwa nini hawataki kupokea ushauri wa watoto wao. Imeshajengeka katika akili zao kuwa ni wao tu ambao wanaweza kutoa ushauri.

  JibuFuta
 2. Nakubali kabisa !

  Na ukitaka kupata mfano angalia ni Wakristo wangapi waliozaliwa na kukulia katika mazingira ya kikristo unaweza KUWASHAURI wageuze DINI wawe Waislamu, na ni Waislamu wangapi unaweza kuwageuza wawe Wakristo ambao wamezaliwa na kukulia kwenye kweli yao kama waitambuavyo yenye misingi ya KIISLAMU.

  Of course kuna EXCEPTIONS , lakini STATISTICALLY ni asilimia kiduchu uwezayo kuibadili KWA KUISHAURI IKUBALIANE NA KWELI YAKO , na katika mfano huu hapa, naongelea hata kama unaowalenga ni WAKRISTO au WAISLAMU ambao kwenye dini zao ni INACTIVE.

  NI MFANO TU ambao unaweza ukawa sio mzuri sana katika kuainisha jinsi navyokubaliana na wazo lako MKUU BWAYA!

  [Samahani pia kwa kuingizia ung'eng'e wakati nashuka neno hapo juu!:-(]

  JibuFuta
 3. hapa nawakumbuka wahenga kwa ule usemi wao kuwa samaki mkunje angali mbichi, sijui ilikua ni mbinu tu ya kuwafanya watoto kuamini wazazi wako sawa wakati wote(ingawa wakati mwingi ndivyo) ama ni mbinu mbadala ya kujenga jamii bora ijayo. mmh, bado nipo ukurasani nawasikiliza wadau

  JibuFuta
 4. Great blog!!
  If you like, come back and visit mine: http://albumdeestampillas.blogspot.com

  Thanks,
  Pablo from Argentina

  JibuFuta
 5. Na kwakuwa tunakubali kushauriwa, basi tunajikuta tunakubali ushauri hata kama kuna makubaliano ya kutofuata ushauri....lakini mimi na wew tunashaurika kwani ni mimi na wewe tunashauriana. Lol....

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3