Dini ni ajali ya kuzaliwa

Wengi wetu hatukuchagua kufuata dini tulizonazo. Tumejikuta tunarithi dini za wazazi ambazo leo tunatoana nundu kuzitetea.

Tumezivaa dini bila maamuzi na tumezishikilia utafikiri tunazijua.

Na ajabu tunaamini kuwa dini nyingine zilizobaki kuwa haziko sahihi wakati kama tungezaliwa na wazazi wengine pengine ndizo zingekuwa zetu!

Mkristo (ambaye ni mrithi wa dini ya baba yake) anaamini dini zote zilizobaki zimekosea. Mwislam naye (ambaye kajikuta mwislam kwa kuzaliwa) anaamini wote waliobaki ni 'makafri.'

Kinachosikitisha ni kwamba tumejengewa uzio wa kutuzuia kujifunza dini za wenzetu.

Na tunapojifunza dini hizo, kimsingi hutafuta kasoro na mapungufu yatakayotupa kuridhika kuwa dini zetu ndizo sahihi.

Tungelijua kuwa dini ni ajali, basi ikiwa ni lazima, tungezipitia zote ili kuchagua moja au mbili.

Vinginevyo tunabaki vipofu jeuri wanaojua kuelezea mkia wakidhani ndiye tembo.

Maoni

  1. Kaka kwanza habari za siku nyingi.
    Nakubaliana na wewe katika mada hii, ni ukweli usiopingika kuwa wengi tumejikuta tuikiwa klatika dini au dhehebu fulani kwa sababu ya wazazi wetu ambao nao walijikuta wakiwa humo kutokana na wazazi wazazi wao, mnyororo ni mrefu sana kwani hata hao mamabu zetu walilazimishwa kuacha dini na mila zao za asili na kulazimishwa kufuata dini hizi za mapokeo iwe ni kwa nguvu au kwa hiyari.

    JibuFuta
  2. Kaka, nimejaribu kuwa sambamba nawe, sambamba na Nautiakasi na Mkristo pia.
    Mi nadhani ukweli ni ukweli hata kama watu wengine hawapendi kuukubali.
    Tumezaliwa kwenye familia zenye dini tulizonazo.
    Lakini hata hizo tulizozaliwa nazo hazikuwa zetu. Zililetwa na wageni kwa maslahi yao kiuchumi.

    JibuFuta
  3. namna hii, swali langu halijapata majibu yoyote narihamishia hapa,

    kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...
    sipendi kuwa kama wale wanaoshikilia upande mmoja wa mambo. labda swali langu ni je! uisilamu nini na ukkristo ninini na mwisilami ninani pia mkristo ninani? tafuteni maana ya maneno haya kwanza harafu mlete ubishi wenu wa kiakili!

    nautiakasi,

    hivi wewe unaamini kkuwa koran ilitoka mbinguni? itakuwaje leo kama ikishushwa nyingine au unauhakika gani kama haikuwahi kushushwa? je ni kitabu gani tunapaswa kukifuata? hivi tunavyochapwa viboko kuvikariri au kingine muhimu ambacho hatukioni kwani kimo ndani mwetu?

    wapi muhimu kama sio ndani mwetu? kwa nini tusi- 'tahajudi' (meditate) na kuuona ukweli mkubwa zaidi badala ya vijitabu hivi????

    JibuFuta
  4. Kamala,

    Masuali yako yako yanahitaji majibu. Naamini wale wasomaji wetu (nautiakasi, mkristo na wengine) watarudi kuchangia mawazo yao ili twende kwa mwendo mzuri.

    Sikuwa nimeona maoni haya wakati naendeleza mjadala huu. Majadiliano yanaweza kufanyikia kokote hapa, au ukurasa wa kwanza.

    Asante Kamala, Mtanga na wengine kwa ushiriki-endelevu.

    JibuFuta
  5. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  6. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  7. VIGEZO VYA YESU KUWA MUISALAMU NI DHAIFU, KWANI HAVIONYESHI UPEKEE (haviko katika dini moja tu)

    Hoja amabazo hutumika kudhibitisha ya kwamaba yesu ni muislamu na sio mkristo huwa zinanishanagza sana. kwa mfano; Kutawadha, Kusujudu, Kuingia katika msikiti, kuingia katika masinagogi. sababua zinazonifanya nishangae ni kama zifuatazo. Kusema msikiti (sinagogi) ilikuwa nyumba ya ibada kwa dini ya kiislamu tu.

    Ikiwa waumini wa Kiyahudi waliabudu katika masinagogi ambamo kristo nae alaibudu kwa nini tusiseme alikuwa muumini wa dini ya kiyahudi kwa sababu waumini wa kiyahudi huabudu katika msikiti?. Je ikiwa wayahudi walitawadha kwa nini tusiseme yesu alikuwa muumini wa dini ya kiyahudi?. ikiwa tunasema yesu hakuingia kanisani kama hoja ya kumtenganisha na ukristo kwa kutoa mfano wa hekalu, na kwa sababu mabudha husari katika Mahekalu. Je ni hahalali kusema yesu alikuwa budha eti kwa sababu mabudha huabudu kataki mahekalu?. Toeni vigezo au sababu za msingi zenye kuonye upekee wa yesu kuwa muislamu sio hizi mtoazo kwa sababu vigezo mnavyo tumia hata dini nyingine wanavigezo hivyo.

    JibuFuta
  8. Religion never saved anyone, Jesus saves! Karibuni kwa Yesu ndiye njia ya kweli na uzima!

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Makundi Manne ya Tabia za Watoto Kitabia