Tujichunguze kabla ya kumshutumu Michael Jackson


Watu wengi wanamshutumu Michael Jackson utafikiri hawafanyi alichofanya. Walipewa nywele pilipili, wanazikaanga ziwe kama za Michael Jackson. Wana vyuso nyeupee lakini miguu myeusi tii. Eti nao wanamlaani Michael Jackson.


Tumekuwa vipofu. Wengi wetu hatukufikia hatua ya kuchonga pua, kwa sababu tu hatukujaliwa pesa za kufanya hivyo!

Nilimwambia dada mmoja hivyo, nusura anitoe ngeu. Lakini meseji senti.


Wengi wetu hatuna tofauti na mzungu Michael Jackson. Halafu tunajidai kumshambulia.


Je, huu ni uungwana kweli?

Maoni

 1. Well!! Wengi wa wanaoonya hata hawajui maisha aliyopitia na yalioelekeza kufanya alichofanya. Kulikuwa na usiri wa hali ya juu katika maisha yake na sasa yaonesha kuwa ni machache sana yaliyokuwa yakifahamika kumhusu. Lakini tukubali ama tukatae, kuna wengi ambao tunawaheshimu na kuwapenda ambao maisha yao ni mabovu zaidi ya huyu ambaye tunamhukumu sasa. Watu wanahoji mengi kumhusu Michael na hata watu wengine kwa kuwa ya kwao hayajawekwa wazi. Kwa walio hapa Marekani watatambua hili zaidi kwa kuwa tumewaona na kuwasikia na kuwasoma viongozi wengi wa kisiasa (hasa hawa wahafidhinba wa Republican) wakisema na kuhimiza kuhusu MISINGI YA KIFAMILIA NA NDOA na wengi wao sasa wamekamatwa na kashfa za UZINZI na hata WIZI WA PESA. Ni kati ya watu ambao wakiwa wanaongelea matatizo ya jamii na namna ambavyo jamii inastahili kushikilia nguzo za kifamilia, utadhani wamewekewa PASSWORD YA MAOVU lakini wanapokuja "kudabuliwa" na maovu yao wanakuwa wadogodogo na wenye aibu tele.
  Ni hali hiyohiyo ilivyo kwa wengi wetu. Tunasema tusemayo kwa kuwa yetu hayako mwangani.
  Namsikiliza saana Lucky Dube na katika wimbo wake huu alisema "the things you say today will come and hunt you tomorrow, the things you do today will come and hunt you tomorrow. IF YOU CAN'T SAY SOMETHING GOOD ABOUT SOMEBODY, JUST SHUT UP"
  Na ni ujumbe huu huu ninaoutuma kwa wote wajionao watakatifu kuwa, kama kuna utakatifu ndani yenu, na muendelee kuishi kitskstifu huku mkiwasaidia wasio nao kuupata bila kujitangaza. Na hakuna haja ya kujisifia kwani watenda mema hujulikana. Pia hakuna haja ya kusema mabaya kwani haisaidii lolote hasa kwa aliyekwisha uvua utu.
  Kwa hiyo, kama huna la kusema, ama huna zuri la kusema kuhusu mtu mwingine, JUST SHUT UP

  JibuFuta
 2. Nakubaliana kabisa na Mkuu Bwaya na Muzee wa CHANGA VOLKANO.

  Ila samahani kwa Muzee Changa Volkano miye nimejipa UTAKATIFU mwenyewe nimechoka kumsubiria PAPAA BENEDIKTO.:-)

  JibuFuta
 3. Mzee wa changamoto asante sana kwa mchango ulioshiba. Nimesoma maoni yako kwa tafakari kubwa na nimejifunza mapya.

  Mtakatifu Mkodo, habari za siku? Nshakutumia e-mail bila mafanikio. Pole na majukumu mkuu!

  JibuFuta
 4. Mimi nadhani kuchonga pua, kubadilisha nyeti, n.k hii ndio balaa ya kumtafuta Mungu maneno, lkn kukaanga nywele, kupaka kucha ina,kupaka lipstiki,n,k si makosa hata kidogo na haya hayapaswi kuzungumziwa.

  Ina maana hata kunyoa nywele ni yale yale ya wako jako?
  Hatukuzaliwa na Nguo, wala viatu, hayo nayo ya kiwako jako?
  Kwa nini tulipewa utashi?

  Hivi wanaofanya plastic surgery wana hatia kwa Mungu?

  JibuFuta
 5. Kwa maoni yangu urembo sio kujichubua lkn kuwa msafi ni jambo jema! Nawahurumia sana watu wanaopenda mambo hayo.

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Pay $900? I quit blogging

Fumbo mfumbie mwerevu