Kura nipige mimi, kula wale wenyewe?

Niko saluni jioni Jumamosi. Kuna vijana wanne. Umri wao wote ni kati ya miaka 20-30.

Kinyozi: (Huku akininyoa baada ya kimya kifupi)…Ee bwana watu wengine noma.
Mie: Imekuwaje?
Kinyozi: Hapa watu karibu wapigane kisa Simba (timu ya mpira wa miguu) kafungwa mbili na Azam kitimu kidogo...
Mie: Kwani tatizo ni nini?
Kinyozi: Tatizo ni kwamba wanaopigana hata kadi za uanachama hawana.
Mie: Labda ushabiki si unajua tena…au wewe hushabikii mpira?

Kinyozi: Mi hata sifuatilii sana mambo ya kijinga haya. Mi nafuatilia mambo yangu bwana.
Mie: Kwa hiyo mpira hufuatilii kabisa?
Kinyozi: Hata mara moja bosi wangu. Upuuzi mtupu. (Akalalamikia uongozi mbaya wa
timu zetu kwa zaidi ya dakika tano kisha…) Mi labda timu za Ulaya. Napenda Aseno. (Akatumia dakika kadhaa kuifagilia)
Mie: Una kadi ya Aseno?
Kinyozi: (Akicheka) Sina ila sipigani wakifungwa
Mie: Sasa hapa home unafuatilia nini?
Kinyozi: Bongo nifuatilie nini hapa pamechoka hivi… kwanza ningekuwa na uwezo ningezamia meli…
Mie: Pengine mambo yanaharibika kwa sababu hatujihusishi nayo…
Kinyozi: Hii nchi imeoza…(akatoa mlolongo wa shutuma kwa viongozi wa nchi hii)
Mie: Hivi unajua kuwa unaweza kuwatoa madarakani hao jamaa wanaokukera kiasi hicho?
Kinyozi: (akadakia) Hakuna. Utawatoaje hawa mafisadi? Hii nchi ina wenyewe bwana?
Mie: Piga kura…
Kinyozi: (akionyesha kunishangaa)…Kura? Sitakaa nipige. Mamaaa! Kura?...(Akamgeukia mwenzake) Eti wewe unapigaga kura?
Jirani wa 1: Hata siku moja. Kura uwapigie wale wenyewe njaa yako inabaki palepale.
Kinyozi: (Akidakia) Kazi ya kuwafaidisha watu mimi sifanyi…
Mie: Kipi bora kupiga kura ilete mabadiliko ama kuacha ili mambo yaende yalivyo?
Jirani wa 1: …bora yaende ivo hivyo. Kura yangu moja haiwezi kubadili chochote
Mie: Sasa kila kijana akiwaza unavyowaza wewe hayo mabadiliko tunayoyataka yataletwa na nani?
Jirani wa 2: Wacha wapeane wenyewe na watoto wao (akitukana matusi ya nguoni)…
Kinyozi: Na kweli. Kura ni ufala (akimaanisha ujinga) cha maana tubebe bunduki…
Jirani wa 1: (Bila hata kustushwa na pendekezo la mwenzake) …Kama Kenya pengine mafisadi watashika adabu…yanalindana.

Tukaagana.

Maoni

  1. Hakika mambo hay si ya kupuuza hata kidogo hata mimi ninakumbana nayo kila siku vijana wamekata tamaa ya kuishi katika nchi yao

    JibuFuta
  2. Hakika mambo hay si ya kupuuza hata kidogo hata mimi ninakumbana nayo kila siku vijana wamekata tamaa ya kuishi katika nchi yao

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Pay $900? I quit blogging