Hivi watoto 'wa mitaani' wakikua huenda wapi?

Mimi sikuwahi kujiuliza swali hili. Baada ya kuisoma makala ya Ayoub Ryoba katika Gazeti la kila wiki la Raia Mwema nilifikiri mara mbili mbili: Hivi kweli hawa watoto tuliowabandika majina mengi ya fedheha kama eti watoto wa mitaani huenda wapi wakikua? Hapo tu. Hawa watoto ambao wengi wetu hatuna habari nao, si wanakua? Je, wakikua 'wanaishiaga' wapi?

Ni watoto waliokata tamaa. Hawana amani. Wanaiona jamii kama inayowaonea. Wana kisasi. Je, wanapokuwa huishia kuwa akina nani?

Hii ni changamoto ya aina yake. Namshukuru mwandishi huyu kwa kutukumbusha eneo hili kwa uzito unaostahili. Fikiria watu kama wabwia unga. Majambazi sugu. Makahaba na kadhalika. Uone mzunguko wa aibu tunaoujenga katika jamii. Kama unadhani kuwa matatizo yao hayakuhusu, tafakari kwa bidii.

Tunaweza kupunguza tatizo hili la kuwa na watoto wengi wa aina hii, amabo wakiisha kukua wanaturudia kwa mlango wa nyuma kwa kuacha tabia ya hovyo ya kupenda kuzaa bila kuhesabu gharama.

Maoni

  1. Ni swali nzuri nadhani sio wewe tu kuna wengi ambao tunasahau swali hili. Lakini inawezekana labda hao watoto wa mitaani ndio marais, mawaziri pia walimu wa taifa la kesho nani anajua.

    JibuFuta
  2. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  3. amani kaka,nadani wote tukijaribu kupost articles kuhusu jumuwata nadhani tutakuwa tumefanya kitu cha muhimu sana.

    amani kaka.

    JibuFuta
  4. Yasinta ni kweli inawezekana tukawa na watu muhimu wa baadae ambao sasa tunawaona kama kero flani hivi. Ni muhimu kwetu sisi kuangalia namna ya kulitokomeza tatizo hili kwa jamii yetu.

    Asante Yasinta kwa maoni. Tuwe pamoja.

    JibuFuta
  5. Luihamu nakuunga mkono. Tunawajibika kuihuisha/kuifufua jumuiya yetu. Na ufufuo huu unafanywa kwa juhudi za kila mwanablogu pasipo kusubiri viongozi. Nitalifanyia kazi pendekezo lako.

    Ingependeza kama kila mmoja wetu angetamani ile siku ya blogu Tanzania inawepo mwezi Novemba kama ilivyowahi kupangwa mwaka juzi.

    Mbiu yako inayo umuhimu mkubwa katika hili.

    JibuFuta
  6. Bwaya ni kweli jambo hili sio wengi ambao tunajiuliza.Umekifanya kichwa changu kiingie katika kuwawazia hawa watoto.Kwanza malezi yao hawa watoto ni nani anayehakikisha wanakuwa ktk misingi iliyobora?Shime ndugu zangu jukumu ni letu sote kuwaangalia hawa watoto.Sina hakika wako wa ngapi maaana hata idadi yao haijulikani.
    Lui habari ya siku?

    JibuFuta
  7. Nuru,

    Tujipange kuona tunawasaidiaje watoto hawa. Wajibu huu ni wetu sote kwa nafasi zetu.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?