Siri ya mwandiko wako (2)

Kama tunavyoweza kumwelewa mtu kwa maneno anayoongea, pia twaweza kumwelewa kwa kuuangalia mwandiko wake. Unapoandika kwenye karatasi, ukweli ni kwamba unatupa dodoso kuhusu tabia zako. Hebu na tuangalie mifano michache ya aina za miandiko na tabia zinazojidhihirisha kupitia miandiko yenyewe:

1. Mwandiko wa kukandamiza: Maana yake akiandika nundu nundu za herufi zinaonekana upande wa pili wa karatasi. Ni dalili ya fikira chanya, kujiamini (hata kunakozidi mipaka) jeuri saa nyingine, majigambo.

2. Kuandika juu juu kwa kuparua: Kutokujiamini, na tabia ya kufikiria mambo kinyume. Yaani kufikiria ubaya, udhaifu wa jambo zaidi.

3. Mwandiko unaolalia kulia: Mwandishi anafikiria anakoenda zaidi, anafikiria mbele. Mara nyingi hana muda wa kutafakari makosa yaliyowahi kumtokea kwenye maisha yake.

4. Mwandiko unaolalia kushoto: Hufikiria jana na yaliyopita. Hujilaumu kwa makosa aliyowahi kuyafanya.

5. Mwandiko unaoongozeka ukubwa kadiri unavyoandika: Mwandikaji ni mbunifu, mkali, hujua kutumia fursa zinazojitokeza. Kama mwandiko unangezeka sana kadri anavyoandika basi kuna uwezekano wa kuwa una tabia ya kuingilia mambo yasiyokuhusu. Kujipenda zaidi (ubinafsi) na kiburi.

6. Mwandiko unaopungua ukubwa wa herufi kadiri unavyoandika: Tabia ya kuishi kama wanavyotaka wengine ama kwa maoni ya watu wengine, kukubali wanachosema wengine, kwa sababu ya kutokuweza kuanzisha mambo mwenyewe. Mtu aliyekata tamaa.

7. Mwandiko usiobadilika kadiri unavyoandika: Uwezo wa kuendana vyema na mazingira yako, mkweli, lakini hata hivyo kukosekana kwa uanzishaji mambo.

8. Herufi kubwa kubwa zenye urefu na upana sawa: Dalili za mwandishi mwenye akili, uwezo wa kuchambua mawazo, uwezo wa kuzingatia, sayansi, ana hisia za juu.

9. Herufi kubwa ndefu nyembamba: Mwenye aibu, Kufikiri kwa juu juu, kutokuangalia jambo kwa kina, hapendi sayansi, walau anavutiwa na siasa kiasi kidogo, anahitaji kichocheo kikubwa kufanya maamuzi.

10. Herufi pana fupi (nene): Mkimya, haongei ongei, ila anajua kupenda, anaishi vizuri na watu.

11. Mwandiko mdogo: Uwezo mzuri wa kuchunguza jambo kwa makini, uwezo mzuri kiakili, Umakini, kumbukumbu safi hivyo anaweza kukariri mambo mengi kwa wakati mmoja, anaheshimu watu wengine hata kama wanatofautiana naye. Ila sasa ukiwa mdogo sana utafikiri sisimizi, maana yake mwandishi hajiamini, anajiona duni flani akijiinganisha na wengine.

12. Mwandiko mkubwa (Jiandiko): Uwezo mdogo wa kuchunguza undani hasa wa jambo, tabia ya kuchukulia mambo katika ujumla jumla zaidi, kutokuwajibika, na utegemezi kwa wengine, kutaka sana ushauri hata kwa mambo yasiyohitaji kushauriwa. Kusikiliza zaidi wanavyosema wengine

13. Mwandiko unaogeuka geuka, mkubwa mara mdogo nk: Hisia zisizotabirika, ‘mudi’ inayobadilika badilika, mchanganyiko wa kujisikia salama na kukata tamaa, tabia ya kufanya mambo kulingana na unavyojisikia. Uwezo mzuri katika muziki na sanaa.

14. Mwandiko unaopungua ukubwa kadiri unavyoandika: Watu wachache wana mwandiko huu, na mara nyingine hutokea mtu napokuwa katika msongo wa mawazo.

Hata hivyo, ni vyema kukumbuka kuwa mwandiko wa mtu huwa na sifa zaidi ya moja katika hizo kumi na nne tulizoziona.

Je, una maoni gani?

Maoni

  1. kwanza nimestaajabu sana maana nilikuwa sijui kama mwandiko unaweza kuwa na maana kama hizo. Asante sana nitajaribu kuangalia nina mwandiko gani ili nijue mimi ni nani?

    JibuFuta
  2. Haha haaaaa Yasinta ututangazie matokeo au sio?

    JibuFuta
  3. Haya hizi sifa yawezekana ni kweli kwani mimi ninamwandiko mdogo ambao kila mtu akisoma huwa anasema kuwa ninmwandiko mdogo.

    Mwandiko wangu uko wima ila unalalia kushoto kidogo sana ukiangalia vizuri ndio unatambua.

    JibuFuta
  4. asante bwaya kwa kutusaida kuelewa uhusiano uliopo kati ya mwandiko wetu na tabia zetu.Yasinta tunangoja matokeo.
    Je kuna uhusiano kati ya kutembea kwa mtu na tabia yake?

    JibuFuta
  5. Swali la muhimu Nuru. Nimevutiwa na swali lako, ngoja nilipandishe ukurasa wa kwanza kwa ajili ya mjadala.

    JibuFuta
  6. Kazi nzuri kijana. Mbona kama sijaona mwandiko wa kucharaza na ule wa kuumba herufi? Au hizi nazo aina za miandiko. Tafadhali Bwaya

    JibuFuta
  7. ......" inakuwaje kwa mtu anaye andika miandiko ya aina nne?....kulala kushoto, kulia, wakusimama.....na wakugandamiza?

    JibuFuta
  8. Ww jamaa genius coz imepatia

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Makundi Manne ya Tabia za Watoto Kitabia

Uislamu ulianza lini?