Nadharia ya kuwaelewa wenzio

Bila shaka umeshawahi kugombana. Kupishana na mtu. Kushindwa kuelewana na mwenzako. Kupishana maana yake ni wawili ninyi kushindwa kuelewa kila mmoja wenu anataka nini. Pengine tuanzie hapo. Kuwaelewa wengine. Je, tunaweza kuwaelewa watu wengine? Na tutajuaje kuwa tunawaelewa?

Kuelewa mawazo ya mtu, imani yake, matakwa, nia na kadhalika ni jambo la muhimu. Na pengine si tu kuelewa mtu mwingine anawaza vipi, bali vilevile kutumia uelewa huo ili kutafsiri ya kile kinachosemwa na kufanywa na mtu mwingine.

Pengine tunaweza kukubaliana kwamba ni kushindwa kuwaelewa wengine ni upungufu mkubwa katika masha ya kimahusiano. Upungufu wa kuwaelewa wengine kujionyesha katika dalili zifuatazo:

o Kutokuguswa na hisia za watu wengine.
o Kutokuweza kuzingatia wanachojua wengine
o Kutokuweza kusuluhisha mambo kwa kuitazama nia ya mtu mwingine wakati alipokosea
o Kushindwa kuelewa ikiwa anayekusikiliza anavutiwa na unachosema ama unaongea tu kwa sababu una mdomo
o Kushindwa kubashiri maana iliyokusudiwa na msemaji
o Kutokujali watakavyokuchukulia watu kupitia unachokifanya
o Uwezo mdogo wa kuelewa kutokueleewana (migororo)
o Kushindwa kudanganya ama kuelewa unapodanganywa
o Kushindwa kuelewa sababu zilizonyuma ya anachotenda mtu
o Kushindwa kuelewa uelewa ama mtazamo wa wengine
o Kutokuweza kuelewa namna tabia zinavyoathiri mtazamo na hisia za watu
o Kutokuelewa tofauti kati ya ukweli halisi na ukweli wa kuhisiwa, ma ,emhine mengi.

Watu wengi tuna shida ya kutokuwaelewa watu wengine, hudhani kile tunachofikiri na kufanya, ndicho kinachotakiwa kuhisiwa na kufanywa na kila mtu. Hushindwa kuelewa kuwa watu wengine wanaweza kuwa na mawazo mbadala. Na huweza kutuwia ngumu kuuelewa mtazamo mbadala unaoletwa kwetu na watu wengine.


HATUA 3 ZA KUWAELEWA WENGINE:


HATUA YA 1: Ni pale tunapoweza kuainisha kile anachofikiri mtu mwingine katika tukio husika.

HATUA YA 2: Ni pale tunapoweza kuelewa kwa yakini kile ambacho mtu mwingine anafikiria kuhusiana na mawazo ya mtu mwingine.

HATUA YA 3: Ni pale tunapoweza kufikiri namna ambavyo watu wengine wanavyofikiri kuhusiana na kile tunachofikiri sisi mwenyewe

Kinachofuata baada ya kuandika hayo, ni kumwuliza huyu anayesoma sentensi hii, “ Uko kwenye hatua gani?” Tunawezaje kujua kuwa tunawaelewa wenzetu katika hizo hatua tatu? Nimeandika kukushawishi ujielewe ikiwa unajielewa kwa kuwaelewa wengine. Kwa sababu huwezi kujielewa bila kuwaelewa wenzako.

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mbinu za Kumfundisha Mtoto Kusoma Akiwa Nyumbani

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Fumbo mfumbie mwerevu

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)