Je kuna uhusiano kati ya kutembea kwa mtu na tabia yake?

Nuru shabani ni mchangiaji mzuri katika kibaraza hiki. Michango ya msomaji huyu ama kwa hakika kuleta mawazo mapya na yenye faida. Asante sana Nuru Shabani.

Kuna swali ameliuliza na nadhani kwa sababu blogu hii ni uwanja wa kujadili mambo yanayohusiana na tabia zetu, swali hili lipo mahali pake. Nimeona ipo haja ya kuliweza wazi kwa ajili ya tafakari za wasomaji wengine wanaopenda mijadala ya aina hii. Yeye anauliza: " Je, kuna uhusiano kati ya kutembea kwa mtu na tabia yake?"

Karibuni kwa michango ya maandishi kupitia kisanduku cha maoni kwa faida ya wasomaji wengine. Je, anavyotembea mtu, kunaweza kutafsiri anavyowaza/tabia yake?

Asante Nuru Shabani kwa usomaji wenye faida.

Maoni

  1. Sabalheli shehe.Inawezekana mwendo ama mikogo ya mtu ikashabihiana na mtu. mathalani tumekwishasikia mara kadhaa watu wakisema jamaa anatembea kibabe. Ukimchunguza huyo jamaa utakuta anatabia za kibabe ama kupenda kunyenyekewa ama kuogopwa. Sie tusio na vimo huwa hatutembei kibabe, labda mbele ya wafupi wenzetu maana tusije tukakong'oliwa.

    JibuFuta
  2. Mwaipopo karibu tena. Nilikukosa muda mrefu kwenye blogu.

    Sasa mbona nshaona wafupi wasiotembea kibabe ila ni wababe. Hapo?

    Hata hivyo naona kuna ukweli flani kwenye hili swali la Nuru. Labda tungeanzia kwenye mcanganuo wa aina za miondoko. Halafu hapo tuangalie zinavyohusiana na tabia zetu. Mwenye kufahamu anajisikie huru kutufahamisha.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Makundi Manne ya Tabia za Watoto Kitabia

Uislamu ulianza lini?