"...Umaafuru wa kitabu hiki (Rich Dad Poor Dad) nilianza kuusikia huku Marekani, miaka michache iliyopita. Ni kati ya vitabu vingi ambayo vinasomwa na hao wenzetu, wakati jamii yetu ya Tanzania inaendelea kuzama katika giza au tunangojea kiongozi wa nchi au serikali ituletee maendeleo, na tukijitahidi sana, tunatumia ushirikina. Tuko tayari kulipa laki nyingi kwenye mambo ya ushirikina, eti tupate mafanikio, badala ya kununua vitabu na kuvisoma. Sasa basi, pamoja na vibuyu vyetu, wenzetu wa-Kenya, ambao wamezingatia elimu tangu zamani, wanaingia nchini mwetu na kujichukulia ajira au kuanzisha miradi. Sisi bado tunahangaika na vibuyu badala ya vitabu. Tutakoma, maana wahenga walisema kuwa asiyefunzwa na mamake hufunzwa na ulimwengu. Na bora iwe hivyo, labda hatimaye tutapata akili. Uzembe ulivyokithiri miongoni mwa wa-Tanzania, utawasikia wakilalamika mbona kitabu hiki hakijaandikwa kwa ki-Swahili? Wakishauliza hivi, wanaamini wametoa hoja nzito, badala ya kutambua kuwa wana...