Machapisho

Ndivyo walivyoboresha Elimu?

CCM inajigamba sana kwamba imepanua elimu katika nchi yetu. Katika ilani yake ya uchaguzi, CCM inatuambia kwamba shule za Sekondari zimeongezeka kutoka 1745 mwaka 2005 mpaka shule zipatazo 4102 mwaka jana. Kwamba wanafunzi wanaosoma sekondari katika nchi yetu, wameongezeka kutoka 401,598 mwaka 2005 kufikia 1,401,559 hivi sasa! Kwa mtu anayehesabu mafanikio kwa kuangalia vitu na idadi, haya yanaweza kuonekana kuwa ni mafanikio makubwa sana kuwahi kufikiwa katika nchi yetu. Lakini tukitazama aina ya hao wanaoitwa wanafunzi wanaodaiwa kuwa mashuleni kwa wingi, utashangaa! Katika wanafunzi hao ni asilimia 17.8 tu ndio hufaulu kwa daraja la I. II na III. Umati mwingine unaobaki (yaani asilimia 82.2) wanaishia kupata daraja sifuri na lile la IV. Kwa maana nyingine, kwa kila wanafunzi 10 wanaofanya mtihani wa Taifa, ni wanafunzi wawili tu hupata angalau daraja la III. Hiyo ni elimu ya Sekondari hata baada ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari. Ukija kwenye elimu ya msingi ambayo n...

Kuvunjika kwa koleo...

Picha
Hivi kama watu mnapendwa na wananchi, mabango haya yote ya kazi gani? Kama kweli ninyi ni chaguo la wananchi, inakuwaje mnatumia mapesa mengi hivi kuwashawishi wananchi hao hao? (picha kutoka Kijiji cha Mjengwa)

Cheka na utafakari kwa bidii!

Hii ni kauli mbiu ya mdau mmoja kwenye jukwaa la majadiliano pale Jamiiforums . Yeye anasema: Usifanye kosa kuchagua RAIS MGONJWA tukaingia hasara ya kurudia uchaguzi! Nimecheka kwa sababu nilihitaji kucheka asubuhi hii. Ila nimeikopi nikitafakari. Jumamosi njema wadau!

Ethics na somo la maisha yetu

Nimefuatilia kidogo mfululizo wa tamthilia ya 24. Kuna mhusika mkuu anayeitwa Jack Bauwer. Huyu kwake kilicho muhimu ni matokeo ya kile anachokifuatilia. Na katika kuthamini matokeo, huyu bwana hujikuta matatani sana. Kwake mbinu si jambo la maana sana hata ziwe haramu lakini mwisho (matokeo) ndicho kilicho muhimu. Na kweli huzitumia mno hadi kumfikisha kwenye matokeo aliyoyataka ambayo ndiyo yanayokuwa jawabu kwa wote. Kwamba haramu imekuwa halali kwa sababu tu mwisho umekuwa mtamu. Jack ananifanya nitafakari maisha yetu vile yanavyoelekea kubadilika ghafla. Kwamba kwa nini tunachoanza kukijali kama taifa ni mwisho (matokeo) bila kujali mbinu? Kwa nini tumeanza kuwa watu wa kutizama matokeo kwa mbinu zozote? Why? Je, ninapopata mafanikio makubwa kimaisha kwa gharama ya uhalifu wa kimaadili kwa jamii, nami tuseme nitakuwa nimefanikiwa? Vipi ninaposhinda uchaguzi kwa matumizi wa zile zinazoitwa siku hizi "siasa za maji taka" yaani kuwachafua washindani wangu ili nifaniki...

Kujifunza katika upana wake!

Nimesoma majadiliano kati ya Mubelwa Bandio na msomaji wake. Nimejifunza maana ya kujifunza. Labda na wewe utajifunza. Tafadhali bonyeza hapa kusoma mazungumzo hayo niliyoyapenda sana huenda ukajifunza kujifunza. Asante Mubelwa kwa changamoto hiyo.

Tumefinyangwa kuwa wakimbizi wa kudumu

KADIRI siku zinavyosonga mbele, ndivyo waswahili tunavyozidi kuwa watu tusiojitambua. Namaanisha kutokujifahamu sisi ni akina nani na tunatofautianaje na wasio watu wengine waliobaki katika uso wa dunia. Tunashindwa kuyaelewa mazingira yetu na thamani ya ustaarabu wetu ambao (huenda) ni ushenzi kwa wengine. Badala yake tunageuza ushenzi wao kuwa ndio ustaarabu rasmi wa jamii yetu. Tunashindwa kujua mwelekeo wetu kama watu wenye ustaarabu wao ambao ndio unaoleta maana ya maisha yenye alama ya Utanzania. Matokeo ya haya matatu ni kurudi nyuma katikati ya hayo yanayoonekana kuwa ni maendeleo. Hapo ndipo tunapogeuka kuwa mazuzu wenye vitu ambavyo babu zetu hawakuwavyo lakini bado tukiishi hovyo kuliko hata walivyoishi wao. Kwa maana nyingine, tunakuwa watu wenye “zaidi” kwa habari ya vitu, lakini wenye “ukosefu” kwa habari ya thamani ya kweli ya utu wetu. Swali tunalojiuliza hapa ni iwapo ni busara kung’ang’ania kuyatafuta maendeleo (kwa maana ya vitu na huduma) pasipo kwanza kuubaini ...

Sisi ni nchi ya kaulimbiu?

Nimekuwa nikijiuliza: Hivi raia wa Tanzania tunatambulishwa kwa kitu gani hasa? Tuna mawazo gani ambayo tunaweza kusema, haya ndiyo mwelekeo wa Watanzania? Ni masuala yepi ambayo nje ya vyama vya siasa yanaongoza mwelekeo wa taifa letu? Maslahi ya taifa (ambayo si lazima yafananane nay a chama kimoja kimoja) ni yepi? Je, tunawafundisha nini wanafunzi wetu ambacho kinawafanya wajitambue kama Watanzania? Utamaduni wetu kama raia wa Tanzania ni upi? Tunajipambanuaje kama wananchi mahsusi wa Tanzania katikati ya bara zima la Afrika? Hivi falsafa hasa ya taifa letu ni ipi? Je, ni kasi zaidi na ari zaidi? Je, tumekuwa nchi ya "miaka mitano mitano"? Kwamba baada ya uchaguzi, viongozi wanajiandaa kwa uchaguzi ujao? Tumekuwa nchi ya kauli mbiu? Nchi yetu inaongozwa kwa mwelekeo upi? Ni nini ambacho kiongozi yeyote akishika mamlaka ndicho atakachopaswa kutusaidia tukifikie? Hakuna kitu kibaya sana kama kuishi bila dira. Hakuna ugonjwa mbaya sana kama ule wa kutokujua unakokwend...

Kwa nini watu hatutulii kwenye fani tulizonazo?

Kwa nini watu wengi hutumia sehemu kubwa ya maisha yao kumangamanga huku na huko, wakibadili kazi na shughuli kutoka ofisi moja kwenda nyingine? Inakuwaje kijana aliyesoma kuwa mtaalamu wa kilimo, hataki kabisa kufanya kazi ya kilimo aliyoisomea na badala yake anatafuta kazi itakayompeleka mbali zaidi na kilimo? Kwa nini mwalimu haridhiki na chaguo lake la awali la kutokotosha fikra za wanafunzi, na badala yake anatumia sehemu kubwa ya maisha yake kutafuta namna ya kuchomoka afanye kazi zisizohusiana na ualimu? Tunatafsiri vipi kitendo cha daktari aliyesomea utabibu kwa miaka isiyopungua mitano, katika mazingira magumu ambayo hatma yake yanamfanya awatumikie wananchi wenzake kwa kuokoa maisha yao, anaachane na utabibu ili kuwa mwanasiasa wa majukwaani? Ninachojiuliza ni hiki: Kwa nini hatutulii kwenye taaluma zetu? Kwa nini hatuzitumii taaluma tulizonazo ambazo zimetupotezea miaka kibao kuzipata? Je, ni aina ya elimu tunayopata? Je, tafsiri ya mafanikio tuliyokuzwa nayo tangu t...

Kanisa Katoliki na ushirikina...

Nasikitika kwamba sijawa na muda wa kutulia kuendelea na mijadala ya imani ambayo nimekuwa niiendesha huko nyuma. Mijadala hiyo imenipa uzoefu mpya ambao mwanzoni sikuwa nao. Mijadala hiyo imenifanya nishangae inakuwaje watu wenye imani ama dini kumtukana mtu anayejaribu kuhoji masuala yaliyo ndani ya dini yake. Mtu akikuonyesha upungufu wako kwa hoja, si ni bora kumshukuru? Pengine ndiyo hulka ya dini: Waamini hujadili kwa kuongozwa na ushabiki na hisia zaidi na sio hoja. Katika blogu ya Strictly Gospel ambayo ni blogu maalumu kwa mijadala ya Kikristo, nimekutana na mjadala ambao pamoja na kuwa bado haujapata wachangiaji wa kutosha, nadhani utakuwa mjadala moto moto huko mbeleni. Mjadala wenyewe unahusu uchawi wa kanisa Katoliki. Hebu bonyeza hapa kushiriki mjadala huo . Muhimu sana kushiriki kwenye mijadala. Na unaposhiriki kubali kujifunza. Ujue tumedanganywa vingi. Tumezungukwa na uongo. Katika familia zetu. Katika shule zetu. Katika siasa zetu. Dini. Na kadhalika. Na katika...

Strictly gospel na mijadala ya kiimani

Nimekuwa mfuatiliaji wa karibu wa blogu maarufu ya Strictly Gospel . Tofauti na blogu nyinginezo, wachangiaji wengi wa blogu hii nawafahamu kwa sura ingawa mmiliki wake sijawahi kuonana naye. Japo mara nyingine nashindwa kushiriki mijadala hiyo ya kiimani moja kwa moja kama ambavyo huwa nashindwa kublogu humu ndani, ni karibu kila siku lazima napita pale kuona namna mijadala ya kiimani inavyokwenda. Hapa nimeupata huu hapa mmoja. Bonyeza hapa kuusoma na bila shaka utajifunza mengi. Unayo maoni yoyote? Tembelea blogu nzima hapa .

Bongo inaumwa kisichoonekana (2)

TUMEKWISHA kuona namna nchi yetu inavyopiga hatua kubwa za kimaendeleo. Na sina shaka kwamba msomaji atakuwa amebaini kwamba hizo zinazoonekana kuwa hatua za kimaendeleo zina walakini. Aidha, tulikuwa tumeishia katika kuyatazama hayo yanayoitwa maendeleo katika sekta ya elimu yanavyolisaidia taifa. Muunganiko wa muhimu ukawa ni kwa vipi rasilimali watu ambayo taifa halikuwa nayo miaka iliyopita, inatusaidia katika kusukuma “maendeleo” mbele? Hapa tungependa kudodosa namna ambavyo ukuaji wa taaluma katika maeneo mbalimbali unavyosukuma mbele maendeleo yetu ili kujaribu kuona ulikolalia ugonjwa wa taifa. ******************************************************* Tumekuwa tukifundisha wanasheria kwa miongo kadhaa sasa. Hawatoshi, lakini wapo na wnafanya kazi zao katika maeneo mbalimbali nchini. Je, watu hawa wametusaidiaje kuondokana na unyanyasaji wa kisheria tunaoupata katika jamii zetu? Taaluma ya sheria imegeuka kuwa mashindano ya kupangilia hoja ili kushinda kesi zisizo na tija....

Bongo inaumwa kisichoonekana

Ni wazi kuwa nchi ya Bongo ya miaka kadhaa iliyopita, si hii ya leo. Mambo mengi ya msingi yanabadilika na kwa kweli yanabadilika kwa kasi kubwa. Hata hivyo, ningependa kuonyesha kwamba tatizo tunalokabiliana nalo katika nchi yetu limejificha katikati ya haya tunayoyaona kama maendeleo. Tatizo hilo haliwezi kutatuliwa kwa kusogeza zaidi maendeleo kwa wananchi wala wala kwa kuanua demokrasia zaidi wala kukusanya kodi zaidi wala kwa kuongeza wasomi zaidi. Tatizo hilo linaweza kutatuliwa kwa kupembua upotofu wa aina ya maendeleo yetu tunayoonekana kuyataka zaidi na tukiyapata tunayatangaza kupitiliza. Tutazame maendeleo katika sekta ya mawasiliano. Nchi hii haijawahi kushuhudia maendeleo yaliyofikiwa hii leo katika teknolojia ya mawasiliano. Tuko juu katika nyaja ya mawasiliano baada ya kuwa tumefungua milango yote miaka ya tisini. Yapo makampuni kibao yenye wateja wanaokaribia milioni ishirini kati ya raia milioni arobaini. Na wote hao wanapigiana simu na kuandikiana ujumbe mfupi wa m...

Kwa nini wewe tena Oktoba hii?

Picha
Unatusumbua! Kadiri siku zinavyosonga wajikomba sa-na Salaamu mpaka unaboa! Eti ‘mmeamkaje wapenzi wangu niwapendao…’ Fataki mkubwa wewe! Ulikuwa wapi siku zote? Kisa cha kumsalimia mtu barabarani? Umejua maana yetu eh? Hivi hukutujua siku za nyuma? Unadhani tumesahau… Sikia, Tunakumbuka nyodo zako mara chache ulizokuja Tunakumbuka kauli zako za maudhi Eti sie wako tu iwe isiwe Tukupe tusikupe haikusumbui Ukasema hata ukiwa kule sie wa hapa ni wako Sasa babu sikiliza Mwaka huu ni wa hapa hapa Wote ‘twajua huna uumini wowote Unatafutaga nini kipindi hiki? Ni hivi hivi tu waja majisidi? Wenzio ‘twaswali weye unadipu Kisa? Eti ule mpango wa mlo huko nje Unachekesha… Yaani mie mwenye njaa nikulishe wewe unayebeua! Yaani unitumie fasta, kama kondomu sina maana tena? Umesahau ulivyotufanyia siku zile? Tumekupa ukala ukaondoka? Shukrani yako sitasahau: vumbi la fo wili mjini Kama hunijui vile… Nashangaa umenirudia...

‘Vijana waache kutumiwa’

Picha
JINA LA KAMALA si geni kwa wanablogu wengi. Yeye ni mwendeshaji wa blogu maarufu inayojadili (pamoja na mambo mengine) masuala ya kiutambuzi. Bonyeza hapa kuitembelea . Ndugu Kamala anajulikana pia kwa namna yake ya utoaji maoni huru katika blogu anazozitembelea ambayo hufikirisha na mara nyingine kuibua mijadala zaidi. Blogu hii ilipata fursa ya kuzungumza naye siku chache zilizopita kuhusu falsafa zake, blogu, dini, siasa na mambo yake binafsi. Karibu kujua zaidi kuhusu mwanablogu huyu anayeblogu kutokea kanda ya ziwa. ________________________________________ Ndugu Kamala, nashukuru kwa kukubali kutumia muda wako ili tuweze kujadiliana masuala mawili matatu. Labda tuanze na falsafa yako binafsi. Unaamini nini katika maisha ambacho ndicho kinachobeba utambulisho wako kama Kamala? Naamini katika utu, ubinadamu, upendo na umoja. Napenda kuelewa vitu na kudadisi na ndio maana natumia majina ya kihaya tu ninayoelewa maana yake na kwa nini yawepo… napenda kuacha maisha yaende na kuf...

Mazungumzo na Kamala Luta

Siku chache zilizopita nilipata bahati ya kufanya mazungumzo mafupi na Bw. Kamala Luta, mwanablogu machachari ambaye si mara moja amewahi kuibua mijadala mizito kupitia maoni yake huru ama makala kwenye blogu yake. Kaa mkao wa kula. Nitayachapisha mazungumzo yake mapema sana namalizia kuweka koma, nukta na funga semi.