Saa nyingine usipende kuamini unachokiona

Umewahi kumwona kunguni anavyokimbia? Sasa ndugu msomaji huwezi amini spidi yote ya kunguni kumbe anakokwenda ni nyuma ya godoro!?

Usipende kuamini unachokiona. Hoji. Tafakari. Utaona kisichoonekana katikati ya mistari.

Maoni

  1. labda! shabaan Robat alituandikia kwamba, usione ukadhani.

    ndio maana siku huzi huwezi kumuuoa mtu mpaka muonajane kwa sababu anaweza kuonekana hendisamu au biutifulu, kumbe kusini mwa jangwa la majani hakuedeki hata kidogo, sasa wewe ukiona sura tu na maumbile unadhani umeona!\

    ofcourse, usichokiona chaweza kuwa muhimu saana kuliko unachodhani unakiona. ndio maana huwezi kumuona mungu. eti kizazi cha leo kinamuona kristo wakati alikufa kabla ya video na kamera kuzaliwa, usipende kuamini jua majamaa yanakupiga changa la macho tu! pweeeeee

    usipende kumwona papa kavaa nguo nyeupe ukadhani na roho yake ni nyeupe, usiende kuona padri haoi ukadhani hajui utamu wa ngono hasa zile za wizi wizi!!!!

    usipende kuona dini zinajifanya kumjua mungu kumbe ndo chanzo cha machafuko duniani.

    usipende kuona bwaya anablogu ukadhani ni mwandishi wa habari. usipende kuona kamala naandika hapa ukadhani yu pamoja nawe

    usipend kuona kikwete anaendeshwa kwenye magari ya fahara ukadhani karidhika, usipende kuona, usipende kuona, usipende kuona, we ona to, lakini kila ukionacho, usione ukadhani na wala usikose kutazama.

    bora kuwa na jicho moja ukaona ya maana kuliko kuwa na mawili ukaanza kuziba moja ili ule chabo kwa .....

    thanx, sipende kuona, napenda kutazama

    JibuFuta
  2. @Bwaya &Kamala: Siutani!:-(

    JibuFuta
  3. Kamala, una kichwa kinachofikiri.

    JibuFuta
  4. Bwaya umenikumbusha sana mwl.wangu wa kemia,alikuwa akipenda kutoa swali ubaoni kisha akasema wale wenye macho ya ndani ndiyo wenye uwezo wa kuuona mtego.Hapa ana maana ni kwa wale wenye kutafakari tu.
    Ni kweli wengi huamini kwa kile tukuonacho bila ya kutafakari.
    Kamala umenena.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Kikao cha tathmini na mipango ya familia

Uislamu ulianza lini?