Kwa nini ndoa za siku hizi hazidumu?

Napenda kutazama kipindi cha Longa Mwanamume kinachorushwa na kituo cha luninga cha ITV kila Jumatano saa tatu usiku. Mzee Barnabas Maro anakiweza.

Pamoja na kwamba mara nyingi wanaume wamekitumia kipindi hicho kuonesha mabavu yao kwenye mahusiano, lakini si kipindi kinachofanana na mavipindi mengine ya nchi za nje yasiyohusiana na utamaduni wetu. Longa Mwanamume ni kipindi kizuri.

Jana ulikuwepo mjadala wa ndoa. Swali lilikuwa: Kwa nini ndoa za siku hizi hazidumu?

Nilifurahia majadala huo. Wazungumzaji walitaja sababu nyingi ambazo ni za kweli.

Nami kama ningeweza kuchangia, ningesema ndoa za siku hizi hazidumu kwa sababu vijana huanza kujuana kimwili kabla ya ndoa. Na kufanya hivyo hujenga tabia ya kutokuaminiana na mwisho wake ni kuvunjika kwa ndoa.

Wewe ungesemaje?

Maoni

 1. Bwaya hiyo ni sababu moja,ila kuna sababu nyingi zenye kuchangia kuvunjika kwa ndoa
  1.Kutokupata muda wa kuelewana vizuri
  2.kutaka kumbadilisha mwenzako awe wewe.
  3.kushindwa kuwajibika
  4.tamaa
  5.kutokuwa wavumilivu
  Hii kwa nionavyo mimi jamani

  JibuFuta
 2. Swala la unafiki tokea watu wakiwa wachumba huwa linachangia sana.

  Wachumba hujaribu kuficha makucha yao ili kila mmoja amkubali mwenzake.Pindi tu wanapoingia kwenye ndoa,basi kila mmoja anaishi atakavyo.

  Hapa huwa kuna tatizo sana kwani mwanaume atataka afanye anachokitaka yeye na mwanamke afuate anachoambiwa yani aishi kwa kadiri ya atakavyo mwanaume na wakati huohuo mwanamke naye anataka mwanaume aishi kwa kadiri ya yeye anavyotaka,
  Hali hii husababisha mgongano ndani ya ndoa na mwisho wake huwa ni kuachana.

  Pia vijana wengi wanaingia ktk maisha ya ndoa wakiwa hawajui namna sahihi ya kuhandle maisha ya ndoa.

  Kumpenda mtu kwa sababu ya kitu alichonanacho mtu huchangia sana kuvunjika kwa ndoa.Kwa mfano mwanadada anayempenda mwanaume kwa sababu ya mali alizonazo,siku mwanaume akifilisika ni dhahiri shahiri kuwa ndoa itakuwa mashakani.

  Ni hayo tu.

  JibuFuta
 3. Ndoa hazidumu? swali zui lakini nashindwa kujibu sawasawa nagojea Koero alijibu kwanza sababu alisema ndoa ni msamiati mgumu kwa wanaume

  JibuFuta
 4. ndoa hazidumu? wewe ulipenda zidumu mpaka lini? kuna ndoa gani iliyoweza kudumu duniani? nafikiri zote ni za muda tu kwa sababu lazima tufe tuziache.

  majibu ya Nuru ni mazuri kiasi. Kissima analaumu unafiki nk, sio unafiki, kumbuka hatuna mfumo wowote wa kufundisha mambo ya mahusiano, kujamiiana (socialization) na ngono. wewe ukitaka kuendesha gari, unajifuza kwa muda, unaendesha, unajaribiwa na kurudishwa darasani, mwishowe unapewa cheti na lesseni.

  ili uwe ijiniam unasoma miaka kibao, unajaribiwa na kuwa injinia. lakini kwenye ndoa, ni wewe tu na demu wako mnaishi pamoja kwa kupewa cheti cha ndoa bila mafuzo ya kueleweka ya ndoa, sasa zitadumu vp wakati wenye ndoa mna vyeti ambavyo hamjavisomea?

  JibuFuta
 5. Ni kweli hazidumu siku hizi au wanandoa wa sasa wamekuwa too open?Ni kweli hawajuani vizuri kabla ya ndoa au binadamu hubadilika hata kama mmejuana vya kutosha na kupendana asilimia zote?????Mie nimekua(grew up) naona familia za karibu yangu,namaanisha ndugu au rafiki wazazi wametengana vyumba au wanalala mzungu wa nne.For the sake of children.SAsa siku hizi wenye ndoa wakitofautiana wanaamua kuwa wa wazi haiwezekani kuendelea pamoja.Tofauti na wazazi wetu walikuwa wanaamua kuishi watoto wakue ndani ya wazazi wote lakini ukweli utakuta hata hawasemeshani,wamenuniana na hata kulala hawalali pamoja tena,watoto mnabaki mnashangaa yanayoendelea.mama anaenda kulala chumba cha mabinti zake wakubwa au baba anaacha chumba anaenda kulala na vijana wake.sidhani kama siku hizi ndio wanaachana sana kuliko zamani.Nionavyo mie
  tchanga

  JibuFuta
 6. Kamala, kudumu kunakozungumziwa ni hadi kifo. Ni wazi kuwa tukifa ndoa hazibaki. Zinakufa na sisi. Ni kweli vilevile kama unavyosema, inawezekana tatizo ni kukosa elimu ya ndoa kabla ya ndoa. Hii ni changamoto nzuri.

  Tchanga, wazo lako limeleta changamoto nyingine. Kwamba siku hizi pengine ni uwazi wa wanandoa unaonyesha tofauti ambayo wazee wetu wanadai hawakuiona.

  Je wanandoa wanawezaje kukabiliana na mabadiliko ya miili yao yanayoweza kuathiri namna wanavyojichukulia wao wenyewe na wenzao?

  JibuFuta
 7. Wanandoa kabla hawajafikia hatua ya kuhalalisha uhusiano wao,kawaida huwa wanachunguzana,wengine hutumia mwaka mmoja,wengine nusu mwaka,wengine miaka saba n.k,sasa kaka Kamala lengo la kuchunguzana nini? Mimi nadhani hali hii inachangia ndoa kuvunjika.Labda uniambie wanandoa wanapokutana na matatizo haya ya unafiki wa mmoja wao huwa wanashindwa namna ya kutatua.Hivi unafikiri ni kwa nini mwanandoa aseme "hivi alitoka wapi na mume au mke wa sampuli hii?" inamaana angegundua tabia fulani pengine wasingeoana.

  JibuFuta
 8. kissima, siku zoote ukimchunguza mwenzio, huwezi kumuuoa kwa sababu sisi kama binadamu tmekamilika lakini hatuko perfect na lengo lolote la kuchunguzana nikutafutana madhambi na ukiyatafuta siku zoote utayapata!!

  msichunguzane jamani, pokeananeni na kuwakubali wenzenu kama walivyo na hivyo mtaushinda uvujaji wa kuvunja ndoa zenu.

  JibuFuta
 9. Kamala ninachelea kukubaliana na ushauri wako.

  Kuchunguzana kwa watu wanaotarajia kuishi pamoja haina maana ya kutafuta 'madhambi' ya mwenzako. Na wala haisaidii kuyajua madhambi hayo.

  Nia ya 'kuchunguzana' ni kuelewa haiba/personality ya kila mmoja. Kujua haiba/tabia ya mwenzako inakusaidia kujua unaenda kuanza maisha na aina gani ya binadamu.

  Vinginevyo, unafikia maamuzi ya kuahirisha tukio ikiwa uchunguzi utaleta uwezekano wa walakini huko mbele ya safari.

  Sasa ukipiga marufuku 'uchunguzi' naona kama unaongeza uwezekano wa miparaganyiko ya mahusiano maana kila jambo linakuwa sapraiz ndani ya mahusiano.

  Na kuvunjia kwa ndoa si habari njema kwa yeyote mwenye hisia zilizo hai.

  JibuFuta
 10. Kuchunguzana hapa tunamaanisha kufahamiana vizuri.Kama wale wanaotarajia kuwa wanandoa hawatafahamiana vizuri hapo baadae maneno kama "laiti ningejua" ,mwanaume/mwanamke wa jinsi gani hii" ,"ama kweli halikuwa chaguo langu" "bora ningeishi mwenyewe" "nina kwetu yanini kuteseka"

  Kwa mfano ukigundua kuwa mpenzi wako ni malaya,na ukajaribu kumrekebisha na hakuweza kubadili tabia, hivi mtu huyu atafaa kuwa mwanandoa? Hivi kama hutagundua mapema unafikiri maisha ya ndoa yatakuwaje?

  Mtu wa dizaini hii kama utamsoma vizuri ni kwamba:

  1. Hashauriki
  2. Atakuwa anakwamisha mambo mengine mengi ya kifamilia

  3. Imani ktk swala la malove utakuwa mdogo
  4. Msongo wa mawazo na kumkosesha raha mwenzie.
  5. Ndoa haitadumu na itaishia kuvunjika.

  Kwa hiyo kaka Kamala swala la kuchunguzana ili kufahamiana ni muhimu sana,kama kaka Bwaya alivyotangulia kusema. Kumbuka kwamba kumchunguza mtu ni kwa lengo la kufahamiana vizuri, kwani utaratibu huu ndio utakufanya uridhike na ufikie maamuzi ya kuingia ktk maisha ya ndoa na umpendae.
  Hivi kweli wapenzi ambao kwa mambo mengi hawasikilizani,kweli wanaweza kuja kuwa wanandoa?
  Ni muhimu sana watafutane wanaopatana,wanaoendana,wanaoelewana,wanaokubaliana, na hii inawezekana vipi,si kwa kuzoana tu, bali kuchunguzana na kufahamiana vizuri. (Rejea ufafanuzi wangu wa rafiki ni nani ). Wanandoa wanaokidhi vigezo hivi hapo juu,wataepuka kwa kiasi kikubwa sana ktk swala la kuvunjika kwa ndoa yao.

  JibuFuta
  Majibu
  1. Mungu atusaidie maana kumchunguza mpenzi wakati unampenda mimi naona ni kazi ngumu kama kuchunguza uzuri wa maji na msosi kwenye ukame, ama hamjui kupenda na kupendwa ni tendo la nasibu tu na kwamba mtu akishapenda ama akizidiwa/akiguswa kunako na akiwa na namna yoyote ile hawezi acha bila kumpata hata kinguvu? au hamjui kama penzi la dhati hata kama la mmoja ni ugonjwa uathirio kichwa na mwili kama magonjwa mengine? mi naona kuhitilafiana ni kawaida ila aliyependa kweli lazima akubali kuendeshwa na mwenzie hasa yule aliyetongozwa ndo anatakiwa azingatie mkataba aliopewa la hawezi ni luksa mwenye uwezo apewe nafasi hiyo. hakuna haja kumwabudu binadamu.

   Futa

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Pay $900? I quit blogging

Fumbo mfumbie mwerevu