Dunia mbili katika nchi moja?

Nilikuwa nikifuatilia namna watuhumiwa 'wetu' wasiohesabika wanavyopata dhamana. Kweli nchi hii ina mambo.

Wakati kila mtuhumiwa anaweza kutoa hati ya nyumba (soma hekalu) lenye kukaribia shilingi za kitanzania bilioni moja, asilimia kubwa ya watanzania waliobaki hawana hata uwezo wa kupata milo miwili iliyotimia kwa siku.

Wakati kuna wenzetu wachache (hata kama hawana hatia) wanaouwezo wa kujiwekea dhamana ya mabilioni ya shilingi, idadi kubwa ya watanzania waliobaki hawana hata ndoto ya kujenga pango lenye chumba kimoja.


Hali hii inatupeleka wapi watanzania? Dunia mbili katika nchi moja? Kwamba katikati ya umasikini huu, wapo wenzetu wachache wanaoogolea ukwasi wa kutisha? Mabilionea hawa wana raha ipi ikiwa wamezungukwa na mafukara pande zote?

Tafakari.

Maoni

  1. Wakati wa mapinduzi ya Ufaransa malkia Marie-Antoinette aliuambia umma wa watu wa kawaida uliokuwa umefurika ukilalamikia njaa na kukosekana kwa mikate "kama hakuna mikate kuleni keki" Hakujua kwamba hali ilikuwa ni mbaya kiasi kwamba hata hizo keki hazikuwako. Matokeo yake tunayafahamu. Matabaka yaliyofumuka na kustawi kwa kasi yanatisha na hayatoi mustakali mzuri wa nchi yetu nzuri iliyojaliwa kwa kila kitu. Hatusemi kwamba watu wote wawe sawa (hakuna jamii ya hivyo hapa duniani na hata wanyama wa George Orwell katika Shamba la Wanyama walijaribu wakashindwa) lakini inabidi tuhakikishe kwamba angalau wale wa tabaka la chini wanaweza kupata mahitaji yao ya lazima. Sasa tumefikia hatua hata ya kuwakoromea wasipate elimu ya juu. Tunategemea nini huko mbele? Watu ni sawa kutajirika kwani utajiri ni jambo zuri lakini wasitajirike kwa kuwaibia (tena waziwazi) hawa ambao hawajui kesho watakula nini na watasomeshaje watoto wao. Siku wakisema kwamba sasa yatosha na liwalo na liwe itakuwaje? Naamini kwamba tunaye kiongozi ambaye angalau anajaribu lakini akiwa peke yake katika mfumo huu ulioota mizizi sidhani kama atafanikiwa. Baba wa Taifa pamoja na umakinifu wake na uchungu aliokuwa nao kwa nchi yetu hakufua dafu mbele ya mafisadi na mwishowe alimwaga manyanga. Ni wazi kwamba tunakoelekea si kuzuri. Mungu aibariki Tanzania yetu tuipendayo!

    JibuFuta
  2. uwepo wa matabaka laweza kuwa suala la binafsi zaid kuliko la kijumla.

    ni lazima mtu ajibague ili aonekane kuwa tabaka fulani.
    kuna wanaoitwa masikini eti kwa sababu tu hawana ela mifukoni, wakati ni binadamu wamekamilika. kuna wanaitwa wajinge eti kwa sababu hawajui a, e, i, o, u wakati wanaelimu lukuki za utu, umoja, upendo nk.

    kuna wanaoitwa wajinga eti kwa sababu wafanya vitu tofauti na wengine kwa mkabala wao.

    kuna wanaoitwa vilema hata km akili zao nitimamu, kuna wanaoitwa vichaa hata kama hawjui shida, wao ni kufurahi tu ni kila tukio au jambo kwao ni jema kama isemavyo biblia. kuna wanaoijiita wakristo wana wa \mungu na kuwabagua wengine eti ni watenda dhambi.

    kuna makafiri, kuna walevi, kuna wajinga nk.

    tabaka ni lazima ulitengeneze kwanza kichwani wewe mwenyewe au liiingizwe na ukilikubali linakuwa lako.

    yesu hakuwa na tabaka lakini wakristo wa leo wana matabaka nk, nk.

    bwaya, wewe uko tabaka gani?

    wwewe ni mkristo na wakristo mnasema mtu hataishi kwa mkate tu, sasa wewe unag'ang'nia uchumi (mkate) ili iweje?

    JibuFuta
  3. hodi hodi mwenywewe haya nitarudi kwenye ndo kwanza nimerudi

    JibuFuta
  4. @ Masangu nakushukuru sana kwa maoni yako. Ni sawa watu wakitajirika. Tatizo ni ikiwa hivyo kwa gharama ya walio wengi. Karibu tena.

    @ Kamala umesema sawa. Kwamba mtu hataishi kwa mkate 'tu'. Maana yake anahitaji mkate na vitu vingine. Yaani anahitaji zaidi ya mkate. Sasa ikiwa zinaonekana juhudi za makusudi za kutunyang'anya hata hako kamkate kadogo (ambacho hatuna hata hakika nacho) ni lazima tuseme ili ikiwezekana wastuke kama kweli bado wana ubinadamu.

    @ Yasinta karibu tena. Habari za kijijini? Tulikosa mambo pale kwenye 'maisha' kwa kipindi kirefu. Sasa nafurahi umerudi.

    JibuFuta
  5. Asante kaka bwaya kijijini ilikuwa bomba sana. Nami pia nafurahi kurudi hapa kijijini karibu sana "maisha" ni hayo tu

    JibuFuta
  6. sasa kama hawana ubinadamu wana unini? si bado wanaishi ndani ya miili yao?

    niendapo kijijini kwetu, hakuna umeme wala pesa, lakini watu wanamazao tele shambani. hawalimi kuuza, bali wanalima kula na kushiba. hawaoni umuhimu wa kwenda shule wala kukpeleka pesa benki kwani hawana hofu na wanauhakika wa kula hata kama hawana pesa kwa mwaka mzima.

    wanawinda, wanakula matunda, wanavua samaki.
    kwa tafsiri zenu ninyi wasomi, hawa jamaa ni masikini, lakini wao hawajui umasikini nini! kazi yenu kujaza magari ya ulaya na kujipulizia pafyumu na kula aisi kilimu. wao wana mihogo nk

    JibuFuta
  7. Maskini ni maskini awe anajua ama hajui. Maskini hawi tajiri eti kwa sababu hajui kwamba ni maskini.

    Mtu yeyote asiyepata mahitaji ya msingi ya binadam, ni maskini hata kama haoni kama tafsiri hiyo inamstahili. Kufikiri kuwa mwanakijiji anayekula viazi na matunda mwitu si maskini kwa sababu tu 'hana haja' na tafsiri nyinginezo za umaskini ni ufinyu wa mawazo.

    JibuFuta
  8. jamaa kahukumu tayari wakati hakuna mwenye kesi hapa. anngalieni ubskrantism jamani

    JibuFuta
  9. Usijistukie, sijahukumu. Nimeyachunguza maoni yako si zaidi ya hapo. We are not fighting the individuals here

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Kikao cha tathmini na mipango ya familia

Uislamu ulianza lini?