Fikra zimepitwa na wakati?


Jenerali Ulimwengu ameandika kuzungumzia dhana ya obsikuranti, yaani "... mtu yule anayeshikilia anachodhani kwamba anakijua na akaking’ang’ania kwa nguvu zake zote, na akawa tayari hata kwenda vitani kutetea ‘ujuzi’ wake huo. Ni mtu anayeamini mambo ambayo yanaweza kuwa yamepitwa na wakati, na maarifa ya kuonyesha hivyo yanapatikana, lakini hataki hata kusikia wala kuona jambo lo lote linaloweza kuyumbisha au kuteteresha ujinga wake..."

Anasema "...tumezaliwa katika jamii zenye imani kadhaa zilizoandamana na maelekezo pamoja na makatazo kem kem. Tumejamiishwa (socialised) katika imani, sheria, kanuni na taratibu hizo, kimsingi bila kuwa na fursa ya kuhoji ulazima wa kufanya hivyo. Kwa jinsi hii, hata yale maelekezo yaliyo na faida, au makatazo yenye manufaa, tunayafuata na kuyatii bila kujua ni kwa nini tunafanya hivyo.

Jamii nyingi za Kiafrika haziruhusu watoto waulize maswali mengi, hasa kama maswali hayo yana mwelekeo wa kusaili misingi ya imani zilizozoeleka. Mtoto akitaka kujua kuliko anavyostahili kujua atachapwa, au ataambiwa ni mkaidi au mdaku, hana adabu, haheshimu wakubwa, na kadhalika.

Matokeo yake ni kwamba, katika medani nyingi, tumejenga jamii zetu juu ya misingi ya imani za kale ambazo hazina mashiko katika dunia ya leo, na wala haishangazi kwamba kimaendeleo tuko hivi tulivyo. Jamii zetu haziruhusu udadisi, na bila udadisi hakuna maendeleo"

Anahoji ikiwa tumefika mahala kama taifa fikra zimepitwa na wakati kwetu. Kwa nini? Bonyeza hapa kumsoma gwiji huyu wa maandiko yenye fikra pevu.

Nimeanza kumsoma Jenerali nikiwa kidato cha pili. Tangu miaka hiyo, huwa nisipomsoma najisikia kuumwa. Huyu mzee ni urithi wa vijana wa leo.

Maoni

 1. Kuwahoji siyo vema,
  Kwa mambo waliyosema,
  Wazazi watu wazima,
  Maana wametangulia.

  Tunarithi yale yote,
  Wewe hoji uipate,
  Watakusakama wote,
  Kuwa waharibikiwa.

  Haya mambo nashangaa,
  Mengine si manufaa,
  Lakini nikikataa,
  Wanaweza nichukia.

  JibuFuta
 2. huwa namsoma saana huyu muhaya. lakini huwa simuelewi sana kwa nini anaandika vile aandikavyo! naamini katka jamiiyetu hiii hatupaswai kuandika sana juu ya uzembe au ujinga wa viongozi wetu, tunapaswa kuwaelimisha wanachi wetu juu ya nini kifanike, tuwasaidie wtu kujitambua ili tujenge jamii imara. lakini kuwalaumu viohatari kwani hata wao wanatulaumu sisi.

  mimi naona kama ulimwengu anaandika ili aonekane anavyojua mambo badala ya kuelimisha na kuibadilisha jamii ndio maana niliupenda sana uandishi wa munga tehenan uliowabadilisha watu nikiwemo mimi!

  angalia vichwa vya habari vya gazet lake, mara mengi hajaoa tena, mara ufisadi, mara machafuko, kwanini tusiandeikiwe habari za kweli za kufikirisha badala ya shoking news?

  JibuFuta
 3. Tunayasemea haya,
  Tunayanyo'sha mabaya,
  Na kusema si vibaya.

  Tunanyoosha vidole,
  Tuwaseme watu wale,
  Hatupigi makelele.

  Nakubali Jenerali,
  Hupenda sema ukweli,
  Ni vema tuukubali.

  Namkubali Kamala,
  Ubongowe h'ujalala,
  Kaka zidi gangamala.

  Nilimisi kughani.

  JibuFuta
 4. Mtanga nilimisi ghani zako karibu sana.


  Kamala, kila mwandishi ana aina yake ya pekee ya uandishi. Ndivyo ilivyokuwa kwa Munga. Ndivyo ilivyo kwa Jenerali. Padre Karugendo. Ayoub Ryoba. Magid Mjengwa. Na wengine wachache.

  Hizi tofauti mimi naziona kama faida kwa maana ya kwamba tunapata maarifa kwa watu tofauti wenye dhima tofauti tofauti zinazotia kadha nzuri katika maarifa.

  Kwa nini unafikiri kwamba Jenerali anapoandika huwa anaonyesha namna anavyojua? Kwa sababu huenda anapoandika huwa hata hana wazo la kujionyesha anajua kama wanavyoweza kudhani wasomaji.

  Munga naye huenda kuna watu walidhani kule kuandika ili 'kuibadili jamii' ni kwamba alikuwa anajitia mjuaji wa saikolojia wakati watu makini kama Kamala wanaelewa kabisa hilo halikuwa lengo lake...!

  JibuFuta
 5. haya bwana, labda nisome tena pale ninaposema;

  angalia vichwa vya habari vya gazet lake, mara mengi hajaoa tena, mara ufisadi, mara machafuko, kwanini tusiandeikiwe habari za kweli za kufikirisha badala ya shoking news?

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Pay $900? I quit blogging

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?